Tatizo ni nini TANESCO? Umeme unashindwa hata kuwasha redio kwa baadhi ya maeneo

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,208
42,068
Hili jambo la umeme wa TANESCO kuwa mdogo na kukatakata likuwa likijirudia kila mara kwa nyakati tofauti na hili jambo limekuwa kama mazoea.

Majuzi Jumatano ilifika kipindi nikafikiri radio imeungua kabisa hii ni kutokana kwa umeme kuja gafla na kukata na baadae nilishangazwa umeme na uona lakini radio haiwaki kabisa yani nikafikiri imeungua kabisa pamoja na kuwa na stabilizer.

Baadae nikaja gundua kuwa shida ni Umeme mdogo na wengi wamekuwa wakikumbwa na hii shida maana ni wazi uanaweza kuunguliwa na vitu vyako kwa mtindo huu wa TANESCO!

TANESCO kuna shida gani?

Hapa naongelea jiji la Dar es Salaam!
 
😂😂😂 umeme unashindwa kuwasha radio asee hiyo nchi yenu mnashida sana
 
umeme unashindwa kuwasha radio asee hiyo nchi yenu mnashida sana

Yani nilishangaa sana hadi nikahisi radio imeungua kabisa ikabidi nianze kuchomoa vitu vyote nianze kuitest kila sehemu wapi...baada ya muda nikakumbuka niwashe fridge nalo hola.... taa kuwasha zinawaka ila mwanga mdogo hapo ndio machale yakaanza kunicheza....kuwa pengine umeme ni mdogo sana......

Yani kutoka nje nawauliza majirani zangu wananiambia umeme ni mdogo toka jana yake hauwashi hata radio labda taa na una kataka kata kila muda na kurudi wakashauri tuzime vitu vyote hadi baadae tuangalie........
 
Hili jambo la umeme wa Tanesco kuwa mdogo na kukatakata likuwa likijirudia kila mara kwa nyakati tofauti na hili jambo limekuwa kama mazoea.

Majuzi Jumatano ilifika kipindi nikafikiri radio imeungua kabisa hii ni kutokana kwa umeme kuja gafla na kukata na baadae nilishangazwa umeme na uona lakini radio haiwaki kabisa yani nikafikiri imeungua kabisa pamoja na kuwa na stabilizer.

Baadae nikaja gundua kuwa shida ni Umeme mdogo na wengi wamekuwa wakikumbwa na hii shida maana ni wazi uanaweza kuunguliwa na vitu vyako kwa mtindo huu wa Tanesco!

Tanesco kuna shida gani?

Hapa naongelea jiji la Dar es Salaam!
Kuna kipindi ulikuwa unawaka na kuzima mpk ukaniunguzia chaja yangu niliyonunua 80000 jana yake..Roho iliniuma sana aisee
 
Mmewajulisha tanesco

Shida itakuwa kwenye transformer yenu hapo

Ova
 
Back
Top Bottom