Tatizo liko wapi Rais wangu?

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
952
346
Wana JF,
Mimi ninatatizika na kwa nini hali ya mashaka inaendelea kujitokea?
Ni kweli Rais anakuwa anawafanyia watanzania siasa kwa makusudi au kuna tatizo mahali. Kama kuna tatizo mahali kwa nini tatizo hilo halitolewi au kuondolewa na aRais wetu akawa Rais kwa kila kitu? Rais anapo zungumza kitu na wewe ukakiona kuwa sio kweli hapo ni nini? kwa sura ya nchi na watu wake?

Mimi nimemusikiliza juzi akiwa Karagwe.
Baada ya Mbunge wa Karagwe kumpigia magoti ili Karagwe ipate maji alisema kama ifuatavyo.

Kwamba wamekopa mil 500 kutoka India na imetengewa miji 17 ya Tanzania kwa kupewa maji. Na kuwa mji wa Karagwe ni mmoja wapo.

Hivi ni kweli mheshimiwa hajui kuwa hakuna mji Tanzania unaoitwa Karagwe? Lakini katika utangulizi anajigamba kuwa Karagwe anaijua.

Anataja vijiji kadhaa lakini unakuta vijiji hivyo ni vya wilaya ya Kyerwa. Ni kweli kuwa Rais anatembelea sehemu bila na kuwa na tahadhari ya maeneo anayoyatembelea bila kuwa na uelewa kamili wa sehemu hiyo.

Mwisho inaonesha japo Rais anataja kiwango cha pesa zilizopelekwa Karagwe ni dhahiri Rais hakulielewa swali la mbunge.

Mbunge alimuomba maji kwa wilaya nzima ya Karagwe yenye vijiji mamia, kata makumi na miji mikuu ya wilaya hiyo ya Kayanga na Omulushaka.

Sasa hizo pesa anazozisema ni kwa kwenda vijijini au kwenda Kayanga makao Makuu ya wilaya? Kayanga tayari kuna maji kusiko na maji ni maili kadhaa ndani kama vijijij vya Mabira, Kwenda, Bukene, Kitwe, Kituntu, Ishozi, Nyakahanga, Rwambaizi nk ambapo watu wanatembea maili zaidi ya kilomita 10 kufuata maji.

Na suala kama hilo la maji lipo sehemu nyingi za nchi hii kama Rais anaruhusu watu wampigie magoti ili watengenezewe miradi ya maji tutafika?

Ina maana hamna mfumo wa nchi hii kufikishia watu wake maji?
 
Miradi ya maji ipo katika bajeti ya wizara ya maji ni suala la mbunge,mkurugenzi na watendaji wengine kufuatilia.

Nchi ina mfumo mzuri tu wa utendaji ili sisi ndiyo tuna complicate mambo bila sababu za msingi
 
Ila Mzee wetu huyu anazo matatizo wenda za malezi au kisasi rohoni, haiwezekani kila anapoongea na wananchi wake kazi kufoka na kutoa wrong data.
 
Wana JF,
Mimi ninatatizika na kwa nini hali ya mashaka inaendelea kujitokea?
Ni kweli Rais anakuwa anawafanyia watanzania siasa kwa makusudi au kuna tatizo mahali. Kama kuna tatizo mahali kwa nini tatizo hilo halitolewi au kuondolewa na aRais wetu akawa Rais kwa kila kitu? Rais anapo zungumza kitu na wewe ukakiona kuwa sio kweli hapo ni nini? kwa sura ya nchi na watu wake?

Mimi nimemusikiliza juzi akiwa Karagwe.
Baada ya Mbunge wa Karagwe kumpigia magoti ili Karagwe ipate maji alisema kama ifuatavyo.
Kwamba wamekopa mil 500 kutoka India na imetengewa miji 17 ya Tanznia kwa kupewa maji. Na kuwa mji wa Karagwe ni mmoja wapo.
Hivi ni kweli mheshimiwa hajui kuwa hakuna mji Tanzania unaoitwa Karagwe? Lakini katika utangulizi anajigamba kuwa Karagwe anaijua. Anataja vijiji kadhaa lakini unakuta vijiji hivyo ni vya wilaya ya Kyerwa. Ni kweli kuwa Rais anatembelea sehemu bila na kuwa natahadhali ya maeneo anayoyatembelea bila kuwa na uelewa kamili wa sehemu hiyo.
Mwisho inaonyesha japo Rais anataja kiwango cha pesa zilizopelekwa Karagwe ni dhahili Rais hakulielewa swali la mubunge.
Mbunge alimuomba maji kwa wilaya nzima ya Karagwe yenye vijiji mamia, kata makumi na miji mikuu ya wilaya hiyo ya Kayanga na Omulushaka.

Sasa hizo pesa anazo zisema ni kwa kwenda vijijini au kwenda Kayanga makao Makuu ya wilaya? Kayanga tayari kuna maji kusiko na maji ni maili kadhaa ndani kama vijijij vya Mabira, Kwenda, Bukene, Kitwe, Kituntu, Ishozi, Nyakahanga, Rwambaizi nk ambapo watu wanatembea maili zaidi ya kilomita 10 kufuata maji.
Na suala kama hilo la maji lipo sehemu nyingi za nchi hii kama Rais anaruhusu watu wampigie magoti ili watengenezewe miradi ya maji tutafika? Ina maana hamna mfumo wa nchi hii kufikishia watu wake maji?
Hujamuelewa, tumemuelewa, na huo ndo uelewa wako, usilazimishe ukawa uelewa wetu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom