Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
WATANZANIA WENGI NI LOW KEY KWENYE ISHU ZA MSINGI; HIGH KEY KWENYE UPUUZI. RAIS PANDISHA KEY
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Nimefurahishwa kwa kiasi kikubwa na mwanzo mzuri Rais, Mhe Samia Suluhu.
Uongozi wa Samia Suluhu unahitaji watu High Key ambao wanajitambua, wanaakili, macho ya kuona fursa, na uthubutu wa kuzichangamkia Fursa hizo.
Uongozi wa Samia Suluhu hautatofautiana kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Kikwete, pamoja na mwinyi. Hawa wote hupendelea kuongoza watu wenye High key.
Tofauti na uongozi kama wa Hayyati Nyerere, Mkapa na Magufuli ambao ulikuwa Unawaona watu kama Low Key.
Low key ni aina ya watu ambao wapo low kwenye mambo ya msingi lakini wapo High kwenye mambo ya hovyo.
Low Key hupenda kufanyiwa kila kitu na serikali, na hivyo kama serikali isipofanya basi watu Hawa nao hawatafanya. Low key kama wasipoambiwa na serikali wachimbe vyoo vya kujisaidia basi hawatachimba.
Low key hushabikia mambo Low zaidi yasiyo na faida kwao na watoto wao. Kama vile kushabikia mambo ya Udaku, muziki wa kipuuzi, Mipira, tamthilia na mambo mengine ya burudani, Sanaa na michezo
Sio kosa kufuatilia mambo hayo lakini shida ya Low Key wengi hujikita zaidi huko kwenye mambo ya Burudani na michezo na Udaku ambayo kimsingi mambo yanapaswa kupewa nafasi kidogo hasa muda wa mapumziko.
Ni ngumu sana kwa Low key kufuatilia mambo ya Maana kama vile Masuala ya Elimu, Tafiti, Technolojia, Siasa, Kilimo, Biashara na mambo yote ya kitaaluma yenye manufaa kwao na watoto wao.
Sishangai kwa nini Watanzania wengi wakiogopa Wakenya, sababu ni kuwa Wakenya ni High Key, wanafanana na Wanaijeria, Waghana, na mataifa ya Afrika ya Kaskazini.
Ni watu wasioitegemea sana Serikali yao hasa kwenye mambo binafsi kama kuchimba vyoo.
Kenya wapo Aggressive katika mambo ya msingi kama Siasa, Elimu, biashara, Kazi, Madini, utalii, miongoni mwa Fursa zingine.
Kenya walivyowajanja wametuachia tuwaongoze kwenye mambo yasiyo ya msingi kama vile Muziki, maigizo na udaku ambapo kiukweli fani hizo Watadhani tumefuzu na tunafanya vizuri.
Wote tunajua muziki hauna hela kivile, ndio maana wanamuziki wenye pesa hapa nchini ni wachache mno. Labda pesa za Kiki na ku-pretend na show offs. Sio ajabu hata nchi za USA 🇺🇸 muziki umeachiwa watu weusi kwa sehemu kubwa, hivyo ndivyo Wazungu walivyo wajanja.
Watanzania wanaogopa Wakenya kwa sababu ni Low Key.
Usione hata humu watu wakimshambulia Rais, Mhe. Samia ni kwa sababu ya tupo Low Keys
Mbona kwenye mambo ya kipuuzi hatuwaogopi hao Wakenya? Embu jiulize hata wewe.
Mbona kimuziki hatuwaogopi?
Mbona kiudaku Udaku hatuwaogopi?
Mbona kwenye ishu za ushilawadu hatuogopi?
Mbona ishu za kuandika ugoro mitandaoni hatuwaogopi Wakenya?
Mbona kwenye ishu za Kiki za kipumbavu hatuwaogopi?
Mbona hatuwaogopi na ishu za ushabiki maandazi wa simba na Yanga? Au CCM na Chadema?
Au ushabiki upuuzi wa Diamond Vs Ali Kiba?
Jibu ni kuwa hatuwaogopi kwenye mambo hayo kwa sababu tunayaweza na kuwashinda nayo.
Sasa mbona tunaogopa linapokuja suala la mambo ya kibiashara?
Mbona tunaogopa linapokuja suala la kazi?
Mbona tunaogopa linapokuja suala la Elimu?
Mbona tunaogopa linapokuja suala la kugombania Fursa Kitaifa na kimataifa?
Jibu ni kuwa Watanzania wengi ni Low key kwenye ishu za maana na manufaa.
Mtu hashindwi kubishana siku Nzima kijiweni habari za simba na Yanga wakati muda huo hajui atakula nini, hapo
Hajaoa hajui lini ataoa, hana pesa ya kununulia kitanda wala kulipa kodi, lakini anamuda wa kubishania Diamond VS Ali Kiba
Watanzania wengi ni Low key, tunapenda mambo yasiyo na maana yoyote kwetu na kwa watoto wetu.
Siku nzima upo kijiweni unakalia Udaku na majungu. Utakula majungu??
Watanzania wengi ni waoga wa vita vya kiuchumi kwa sababu ya uvivu na akili finyu.
Sio ajabu uchumi wa nchi umeshikiliwa na watu wenye asili ya Asia.
Muda wa kuendekezana umeisha.
Refa apulize kipenga mipaka ifunguliwe, vita iendelee.
Wakupigwa apigwe, wakushinda ashinde.
Serikali ikiendelea kusikiliza wapenda Udaku itatuchelewesha sana.
Ooh! Wakenya wakija watachukua ardhi yetu, jitu linalosema hivi hata kulima halitaki lipo mjini kazi kuvaa mitepesho
Oooh! Wakenya wakija Tz watachukua ajira zetu. Shenzi kabisa, jitu linalosema hivi utalikuta kila siku kijiweni.
Ni Muda wa kuchangamsha akili za Watanzania zipate moto. Kwa sasa wengi akili zimepoa kama panga lililolala nje.
Fungua mipaka tupasuane.
Serikali itoe passport watu wakachapane huko Duniani
Muda wa Low Key umeisha
Taifa likiwa na vijana wenye mambo ya kike, kukalia Udaku na ushabiki Mbuzi kamwe haliwezi kuendelea
Ndio maana wakitawala baadhi ya viongozi wanadanganya vichwa panzi.
Na Kwa vile ni Low key wanashangilia upuuzi.
Low key unanyimwa haki zako unachekelea kama Mpumbavu.
Low key atakuambia hafuatilii siasa kwa sababu hajui Siasa ndio maisha. Pumbavuu
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro