Tatizo letu Watanzania tupo Low Key kwenye ishu za Maana; High key kwenye upuuzi. Mama Samia pandisha Key

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,176
2,000
WATANZANIA WENGI NI LOW KEY KWENYE ISHU ZA MSINGI; HIGH KEY KWENYE UPUUZI. RAIS PANDISHA KEY

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Nimefurahishwa kwa kiasi kikubwa na mwanzo mzuri Rais, Mhe Samia Suluhu.

Uongozi wa Samia Suluhu unahitaji watu High Key ambao wanajitambua, wanaakili, macho ya kuona fursa, na uthubutu wa kuzichangamkia Fursa hizo.
Uongozi wa Samia Suluhu hautatofautiana kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Kikwete, pamoja na mwinyi. Hawa wote hupendelea kuongoza watu wenye High key.

Tofauti na uongozi kama wa Hayyati Nyerere, Mkapa na Magufuli ambao ulikuwa Unawaona watu kama Low Key.

Low key ni aina ya watu ambao wapo low kwenye mambo ya msingi lakini wapo High kwenye mambo ya hovyo.

Low Key hupenda kufanyiwa kila kitu na serikali, na hivyo kama serikali isipofanya basi watu Hawa nao hawatafanya. Low key kama wasipoambiwa na serikali wachimbe vyoo vya kujisaidia basi hawatachimba.

Low key hushabikia mambo Low zaidi yasiyo na faida kwao na watoto wao. Kama vile kushabikia mambo ya Udaku, muziki wa kipuuzi, Mipira, tamthilia na mambo mengine ya burudani, Sanaa na michezo

Sio kosa kufuatilia mambo hayo lakini shida ya Low Key wengi hujikita zaidi huko kwenye mambo ya Burudani na michezo na Udaku ambayo kimsingi mambo yanapaswa kupewa nafasi kidogo hasa muda wa mapumziko.

Ni ngumu sana kwa Low key kufuatilia mambo ya Maana kama vile Masuala ya Elimu, Tafiti, Technolojia, Siasa, Kilimo, Biashara na mambo yote ya kitaaluma yenye manufaa kwao na watoto wao.

Sishangai kwa nini Watanzania wengi wakiogopa Wakenya, sababu ni kuwa Wakenya ni High Key, wanafanana na Wanaijeria, Waghana, na mataifa ya Afrika ya Kaskazini.
Ni watu wasioitegemea sana Serikali yao hasa kwenye mambo binafsi kama kuchimba vyoo.

Kenya wapo Aggressive katika mambo ya msingi kama Siasa, Elimu, biashara, Kazi, Madini, utalii, miongoni mwa Fursa zingine.

Kenya walivyowajanja wametuachia tuwaongoze kwenye mambo yasiyo ya msingi kama vile Muziki, maigizo na udaku ambapo kiukweli fani hizo Watadhani tumefuzu na tunafanya vizuri.

Wote tunajua muziki hauna hela kivile, ndio maana wanamuziki wenye pesa hapa nchini ni wachache mno. Labda pesa za Kiki na ku-pretend na show offs. Sio ajabu hata nchi za USA 🇺🇸 muziki umeachiwa watu weusi kwa sehemu kubwa, hivyo ndivyo Wazungu walivyo wajanja.

Watanzania wanaogopa Wakenya kwa sababu ni Low Key.
Usione hata humu watu wakimshambulia Rais, Mhe. Samia ni kwa sababu ya tupo Low Keys

Mbona kwenye mambo ya kipuuzi hatuwaogopi hao Wakenya? Embu jiulize hata wewe.
Mbona kimuziki hatuwaogopi?
Mbona kiudaku Udaku hatuwaogopi?
Mbona kwenye ishu za ushilawadu hatuogopi?
Mbona ishu za kuandika ugoro mitandaoni hatuwaogopi Wakenya?

Mbona kwenye ishu za Kiki za kipumbavu hatuwaogopi?

Mbona hatuwaogopi na ishu za ushabiki maandazi wa simba na Yanga? Au CCM na Chadema?
Au ushabiki upuuzi wa Diamond Vs Ali Kiba?

Jibu ni kuwa hatuwaogopi kwenye mambo hayo kwa sababu tunayaweza na kuwashinda nayo.

Sasa mbona tunaogopa linapokuja suala la mambo ya kibiashara?
Mbona tunaogopa linapokuja suala la kazi?
Mbona tunaogopa linapokuja suala la Elimu?
Mbona tunaogopa linapokuja suala la kugombania Fursa Kitaifa na kimataifa?

Jibu ni kuwa Watanzania wengi ni Low key kwenye ishu za maana na manufaa.
Mtu hashindwi kubishana siku Nzima kijiweni habari za simba na Yanga wakati muda huo hajui atakula nini, hapo
Hajaoa hajui lini ataoa, hana pesa ya kununulia kitanda wala kulipa kodi, lakini anamuda wa kubishania Diamond VS Ali Kiba

Watanzania wengi ni Low key, tunapenda mambo yasiyo na maana yoyote kwetu na kwa watoto wetu.
Siku nzima upo kijiweni unakalia Udaku na majungu. Utakula majungu??

Watanzania wengi ni waoga wa vita vya kiuchumi kwa sababu ya uvivu na akili finyu.
Sio ajabu uchumi wa nchi umeshikiliwa na watu wenye asili ya Asia.

Muda wa kuendekezana umeisha.
Refa apulize kipenga mipaka ifunguliwe, vita iendelee.
Wakupigwa apigwe, wakushinda ashinde.

Serikali ikiendelea kusikiliza wapenda Udaku itatuchelewesha sana.

Ooh! Wakenya wakija watachukua ardhi yetu, jitu linalosema hivi hata kulima halitaki lipo mjini kazi kuvaa mitepesho

Oooh! Wakenya wakija Tz watachukua ajira zetu. Shenzi kabisa, jitu linalosema hivi utalikuta kila siku kijiweni.

Ni Muda wa kuchangamsha akili za Watanzania zipate moto. Kwa sasa wengi akili zimepoa kama panga lililolala nje.

Fungua mipaka tupasuane.
Serikali itoe passport watu wakachapane huko Duniani
Muda wa Low Key umeisha

Taifa likiwa na vijana wenye mambo ya kike, kukalia Udaku na ushabiki Mbuzi kamwe haliwezi kuendelea

Ndio maana wakitawala baadhi ya viongozi wanadanganya vichwa panzi.
Na Kwa vile ni Low key wanashangilia upuuzi.

Low key unanyimwa haki zako unachekelea kama Mpumbavu.
Low key atakuambia hafuatilii siasa kwa sababu hajui Siasa ndio maisha. Pumbavuu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,309
2,000
Kuna Mama mmoja wa Kitanzania nimemkubali Sana. Natamani angalau awe Waziri . Aliongea leo asubuhi hii pale kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara wa Kenya vs Tanzania kuhusu PPP integration kati ya sekta za kiserikali na zile binafsi.

Actually,tuna High keys wengi nje ya box la siasa chafu za nchi yetu!!
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,176
2,000
Kuna Mama mmoja wa Kitanzania nimemkubali Sana. Natamani angalau awe Waziri . Aliongea leo asubuhi hii pale kwenye Mkutano wa Wafanyabiashara wa Kenya vs Tanzania kuhusu PPP integration kati ya sekta za kiserikali na zile binafsi. Actually,tuna High keys wengi nje ya box la siasa chafu za nchi yetu!!

High wapo ila wamemezwa na Low key

Bahati nzuri wabongo tunajuana
 

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
363
1,000
Naam brother ... UMEONGEA kweli tupu tena ulio mchungu kama mwiba .
By the way ngoja nikupe kisa fulani hivi.
Kipindi nipo chuo fulani cha wakatoliki hapo moshi (mwenge) muda mwingi haswa jioni nilikuwa Bize sana kusoma vitabu mbalimbali maktaba maana mimi sio mtu wa kujirusha na ma parte na sina marafiki wengi kihivyo.

So vitabu vingi kati ya nilivyokuwa nasoma vilikuwa havihusiani na course niliokuwa nasoma kwa sababu mimi ni mpenzi wa vitabu sana kila ninachokikuta. Sasa kuna vitabu mfano hivi vya maswala ya psychology ,criminology ,world history n.k..

Sasa kama unavyojua kitabu ukishakisoma lazima kuna points au nondo muhimu na adimu unaweza kukutana nazo.. sasa kuna muda hizo nondo nilikuwa nafanya ku share na kwenye group la class .. sasa bana wana walikuwa wana ni dis sana huko inbox . Mara najidai mjuaji mara nasoma visivyo nihusu tuone utafika wapi... Oh mara tuone utafika wapi na vitabu vyako maana ajira hamna ... Kwa kifupi walikuwa ni wakatisha tamaa sana.

Mwisho wa siku nikaja kufanya hitimisho asilimia kubwa ya sisi wa tz hatumpendi mtu anayejua vitu vingi vya maana na vyenye kumpa mtu exposure mfano lugha, maswala ya sayansi , elimu n.k.
Hivyo you nailed it bro ROBERT HERIEL

MÊmENtO HoMO
 

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
363
1,000
Watanzania wengi hupenda mambo ya kipuuzi

Ukiwa msema upuuzi ni rahisi kuwa Na brandy kubwa kuliko msema ya maana

Ndio maana tunaogopa Wakenya achilia mbali Wahindi
Kabisa yaani... Mfano wanamuziki hawa wa bongo

MÊmENtO HoMO
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,987
2,000
Wale wa High key ni jukumu lenu kuwa outsmart mamburula na kugeuza mtazamo. Pambaneni sasa mmeshapata wa kiongozi
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,584
2,000
WATANZANIA WENGI NI LOW KEY KWENYE ISHU ZA MSINGI; HIGH KEY KWENYE UPUUZI.

Uongozi wa Samia Suluhu hautatofautiana kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Kikwete, pamoja na mwinyi. Hawa wote hupendelea kuongoza watu wenye High key. Tofauti na uongozi kama wa Hayyati Nyerere, Mkapa na Magufuli ambao ulikuwa Unawaona watu kama Low Key.
Kwa hiyo Watanzania key yao ilikuwa inabadilika kutokana na awamu husika? Maana nimeona umeanza kuwashutumu Watanzania, halafu baadaye ukaja kuainisha awamu, sasa sijui lengo lako ni kupeleka ujumbe kwa wananchi au kwa uongozi wa awamu mbalimbali
 

Iskariote

Member
Mar 18, 2021
39
125
Umeandika mambo mengi Ila ya maana hayafiki robo.Think beyond kuna watu Wana points humu tusiwabeze
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Umeongea mambo ya msingi sana mkuu Heriel. Kuna idadi kubwa sana ya wa tz wana looser mentality, kwenye kuna jitihada inayofanyika, badala ya kuangalia opportunities na posibilities, wa ni wasiwasi na lawama zisizo nankichwa wala miguu
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,349
2,000
Nchi imejaa viazi wengi hawajitambui wanawaza negative yaani wao wanawaza kupokwa ajira baada ya kuwaza jinsi gani watacompete kwenye soko?

Mimi wakenya nawajua wengi tu ni wazembe hawapendi kufanya kazi sema ni wajanja wajanja tu

So uwezo wa Ku compete nao tunao nimefanya nao kazi sana mpaka Leo nafanya nao kazi.

So nikiona watanzania wanaogopa me ndio mashangaa.
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,194
2,000
Naam brother ... UMEONGEA kweli tupu tena ulio mchungu kama mwiba .
By the way ngoja nikupe kisa fulani hivi...
Mfano mzuri ni hapa JF, subscribe uzi huu uone idadi ya wachanguaji, au anzisha uzi wa "dr. Bashiru aongezewa ulinzi" ulinganishe wachangiaji. Wabongo wengi tupo Low, ngoja nijifue niyoke kwenye LOW
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom