Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Yaani ni vigumu kufahamu ni wakati gani mtu anamaanisha kweli na ni wakati gani anafurahisha jukwaa na ni wakati gani anafunika kombe.Ni ngumu sana kwa kweli na si tu kwamba inaudhi lakini pia inakatisha tamaa.
Wakati mwingine mtu anaweza kujiuliza ni mara ngapi watu wameenza vizuri au wamekuja na mawazo mazuri, au wakaanzisha movement nzuri, wengine wakaamua kuwaunga mkono lakini katika hali isiyodhaniwa watu wakageukana njiani bila ya aibu wala kupepesa macho!
Ndio maana sasa hivi hata mtu akiwa na wazo zuri au akianzisha movement nzuri, kila mtu mwenye akili anajiuliza mara mbilimbili kwamba "kweli au?"
Unafiki, unafiki, unafiki tu! mtu anaunga mkono kitu/mtu hadharani, kimiani utasikia tu "bwege yule akafie mbali" au hadharani mtu anapinga kitu, akiwa pembeni kageuka tena anakitetea. Au mtu akifanyiwa kitu kibaya anapiga kelele kweli kweli na anatoa mahoja madhubiti vibaya mno ya kupinga, lakini naye akipata chance anawafanyia wezake mambo yale yale huku akijenga hoja madhubuti kutetea yale yale!. Yaani sijui imekuwa je kweli.
Unafiki ni adui namba moja kwenye maendeleo yoyote yale. Kweli nawaambia kama hatutoachana na unafiki hata atawale nani, au kitawale chama gani; hatutofika tunakotamani! hata kiama! hii ni kwa sababu hakutakuwa na mtu awe raia, kiongozi au hata taasisi ambayo itakuwa "certain" kwenye kitu chochote kile na hali hiyo daima hupelekea watu kufanya mambo ili mradi tu siku ipite.