denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,511
- 68,141
Salaam,
Nimekuwa nikiona mijadala mingi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia S. Hassan, kufanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya siku ya Jumamosi, tarehe, 19.06.2021.
Kabla wengi walikuwa wakilaumu uwepo wa hicho cheo cha Ukuu wa Wilaya kama kitu kilichopitwa na wakati kwani kimekuwepo toka enzi za ukoloni.
Lakini kinachonishangaza naona wengi sasa wameanza kujadili aina ya watu waliopata teuzi kwenye hizo nafasi kama wao ndio tatizo kutokana na historia zao za elimu, uwajibikaji, n.k. na kusahau hitaji letu la msingi.
Hivyo nimekuwa nikijiuliza; hivi tatizo letu ni ukuu wa wilaya kama nafasi? au ni wakina nani waliopo kwenye hiyo nafasi?
Najiuliza hivi ili nijue ni kipi hasa tunachokihitaji, inawezekana tunataka kitu kiondolewe kumbe kinaweza kutufaa hata sisi wengine mbele ya safari kama tukibahatika kuwa miongoni mwa wateuliwa.