Tatizo letu ; NI UFISADI USIOKUA NA NIDHAMU? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo letu ; NI UFISADI USIOKUA NA NIDHAMU?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Apr 26, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  salaam,

  Baada ya sakata ya report ya CAG gumzo mtaani limekua ni ufisadi unaotisha na kukosekana kwa uwajibikaji kwa viongozi wetu..tunajua kua ufisadi ni tatizo kubwa hapa nchini, lakini ufisadi pia upo nchi nyingi zilizoendelea, na zinazokuja juu kimaendelao. sasa kama ufisadi upo sehemu nyingine duniani kama vile Malaysia, Brazil, South Africa, Russia, Indonesia, Korea nk kwa nini hawa wenzetu wanapiga hatua ya kimaendeleo? jibu zuri nafikiri ni kungalia mfumo mzima wa utawala ambao unaachia hii mianya ya ufisadi na hapa naweza kusema nimeona wenzetu hawa wana ufisadi wa kinidhamu.

  tukitaka kujua huu ufisadi wa kinidhamu, lazima tungalie mfumo mzima wa utawala na hapa kuna kitu kinaitwa patron-client system.
  nchi nyingi haswa zile zisizokua na demokrasia imara, au taasisi za kitaifa makini zina kitu kinaitwa patron-clients networks (yaani kiongozi anaweka watu anaowaona yuko salama nao ili waendeshe serikali bila ya kua na mikwaruzo wala uoga wa kukosolewa au hata kuondolewa kwenye uongozi na hawa wenzake-mfano spika makinda ni client na Jk ni patron wake ili kulindana na kuendelea na uongozi).

  sasa hii patron-client network ili iwe na ufanisi inabidi iwe imehodhiwa na nguvu kubwa ya serikali kuu na wakuu wake wachache(centralized and top-down approach) hapa ufisadi utakua una mpango, utakua unafanywa na wachache kwa sababu lazima upate ruksa au ukabaliane na wakuu wako ambao ndiyo wenye udhibiti wa mfumo mzima wa uongozi na huu ufisadi. Hapa uwajibikaji unakua mwingi, viongozi wengi waandamizi wanakua na ufanisi, mali za umma hazipotezwi hovyo, na maendeleo kwa ujumla yanakuepo mfano ni hizi nchi za Malaysia, Indonesia, Thailand, brazil nk ambao wako juu kwenye list ya nchi zenye ufisadi, lakini wakiwa na ufanisi katika uongozi na maendeleo tofauti na nchi nyingi za Afrika.


  Hapa tanzania na nchi nyingine kama hizi tuna patron-client network isiyohodhiwa kati ,(yetu ni decentralized) ambayo ni loose, bottom-up approach ikiwa bila ya nidhamu-hapa sasa kila wizara, kila ofisa wa serikali, kila mkuu wa mkoa, wa wilaya, kata anaweza kutafuna hela ya nchi au kutumia madaraka na mamlaka yake kula kilicho mezani kwake kwa kua hamna mdhibiti mkuu au mmiliki wa mianya hii ya ufisadi.

  Ufisadi usiokua na nidhamu unaleta mazingira ya dharau ya viongozi kwa wananchi, kulindana kwa viongozi kwa sababu wote wanajuana kua ni wezi au wanahisiana kua ni wafujaji kwa sababu ya kutokua na mdhibiti mkuu (Ukiwa mwizi huwezi kuzuia wenzako wasiibe na huwezi thubutu kuwafukuza kazi). Hapa fedha za umma zinapotea kushoto, kulia, chini, juu, ndani, nje, usiku, mchana, yaani vurugu tupu na maendeleo yanakua ni ndoto za mchana.

   
Loading...