Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,554
Watanzania tuko hivi kwa sababu zifuatazo:-
Tulielezwa tangu uhuru kwamba maadui zetu ni watatu, ujinga - maradhi na umaskini. Hivi inakuwaje miaka zaidi ya 50 watu zaidi ya milioni hamsini tunapambana na maadui watatu wanatushinda? Na badala yake wanaibuka maadui wengine mara hoo mafisadi, mara wasiojulikana?
Kama taifa tujitathmini na tuanze mapambano ya pamoja; tuache tofauti zetu za kidini, kisiasa na kikabila / kikanda. Tujue moja tu ambalo linatuponza; tatizo letu moja ni hili ...
"Tatizo sio umaskini, bali ni mgawanyo mbovu wa rasilimali za taifa"
Leo hii utasikia mara hoo kingozi fulani alijilimbikizia mali na sasa zinapigwa mnada. Jambo la kujiuliza ni hili ... wakati anajilimbikizia mali hizo taasisi / vyombo husika vya kuzuia mtu asijilimbikizie mali vilikuwa wapi?
Au ni mpango mzima wa kujipatia kazi za kufanya kila baada ya kipindi fulani?
Tujitafakari upya!