JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
Habari wana jamvi,
Nimefuatilia kwa muda mrefu jinsi mambo yanavyo endelea nchini mwetu katika nyanja mbalimbali, nimegundua kuwa tatizo ni kubwa mno hasa kwasababu linaanzia kwenye mfumo wetu wa Elimu. Mwishoni nitajitahidi kufafanua.
Kifupi ni kwamba waliotakiwa kuongozwa ndio wanatuongoza. Wasio na maarifa wala ubunifu ndio waliopewa nafasi kusimamia maendeleo ya nchi yetu.
Watu dhaifu kwenye bongo zao na pengine kimwili ndio wamepewa dhamana ya kutupeleka Nchi ya ahadi. Tazama mfano wa hili nilisemalo. Bunge letu lina taratibu, kanuni na sheria nzuri tu kwa kiwango chake, lakini linasimamiwa na mtu dhaifu kabisa kiakili, kimwili na kiroho.
Matokeo yake tumetengeneza bunge dhaifu na kituko zaidi Duniani. Halistahili kuitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni bunge la Ndugai, mtu dhaifu kabisa kupata kutokea.
Tuna wabunge lukuki wanao ona fahari kumtetea Magufuli kuliko kutetea Nchi yao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tumefikishwa mahali ambapo serikali inanunua dawa za masangoma kwa fedha za umma na Bunge limebung'aa tu 'hawakei' ujinga huo. Baadae watawalazimisha wataalamu wa afya wakazigawe kwa wagonjwa? Doctor ataandikaje kwenye cheti cha mgonjwa? Au speaker wa Bunge na Kabudi watazigawa kwa wagonjwa? Kwa niaba ya aliyezinunua?
Hamuoni tunaongozwa na tulio takiwa kuwaongoza?
Tumefika mahali Polisi na pengine vingine vya ulinzi na usalama wanaona fahari kuilinda na kuitetea CCM badala ya Nchi yao! Tatizo hapa siyo watu ni mfumo wa Elimu.
Tumefika mahali watanzani wanaona fahari kumshabikia kiongozi dhaifu ilimradi analipwa fedha.
Naambiwa kuna chama kimeajiri vijana ili kukitetea mitandaoni kwa kuwalipa shs elfu saba. Alas! Graduate kabisa anakubali ujinga huo.
Kiongozi mkubwa ana vunja Katiba mara elfu moja na moja sisi tupo tu tunamshangilia. Kiongozi anatumia ofisi ya umma kujinufaisha bado hatujui kuwa hilo ni kosa.
Kuna haja ya kuufanyia ovehaul mfumo wetu wa Elimu ili wanao graduate wajitambue!