Tatizo la Yanga ni uongozi sio wachezaji wala makocha

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,047
2,000
Kusajili wachezaji bila kuwepo kwa kocha mkuu, kuondoka kwa Zahera na makocha wengine, kuondoka Molinga, Yondani, Ngassa, Carlinhos, Lamine, Morrison, Mwakalebela na kusuasua kwa mabadiliko ya club ni ushahidi tosha kuwa benchi la ufundi na wachezaji sio sehemu ya tatizo la Yanga kwa sasa. Kuna kila dalili kuwa Tatizo kubwa ni uongozi wa club.

Msolla kuwa na taaluma ya ukocha ni sehemu ya tatizo kubwa kwa makocha na club. Lakini TTF nayo ikaongeza ugumu kwenye shida za yanga.
 
redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,499
2,000
Kiongozi wa Simba ndugu Magori alishawahi kunukuliwa akisema Wao Viongozi wa Simba ndio wanao sajili timu kwakua wachezaji ni Mali ya Klabu na si kocha na Kocha anaweza kutimuliwa wakati wowote. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Yanga wachezaji wanasajiliwa na uongozi.

Nikukumbushe hivi karibuni Simba imesajili Magarasa matatu mfululizo Kama , Junior Lukosa, Chikwende na Peter Muduhwa Sasa utasema tatizo ni uongozi wa Simba na Mbaka Sasa Mabadiliko ya uendeshaji Simba yameshindikana.

MO anaiendesha Simba Kama mpenzi na si mwekezaji na kiuhalisia siku yoyote anaweza akaondoka wakabaki wakina Kaduguda na Hans pop ndio wawekezaji.
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
8,200
2,000
Kiongozi wa Simba ndugu Magori alishawahi kunukuliwa akisema Wao Viongozi wa Simba ndio wanao sajili timu kwakua wachezaji ni Mali ya Klabu na si kocha na Kocha anaweza kutimuliwa wakati wowote...
Yuko sahihi, viongozi ndio wanasajili, kwa ushauri wa kocha, simba ilikuwepo kabla ya mo
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,047
2,000
Kiongozi wa Simba ndugu Magori alishawahi kunukuliwa akisema Wao Viongozi wa Simba ndio wanao sajili timu kwakua wachezaji ni Mali ya Klabu na si kocha na Kocha anaweza kutimuliwa wakati wowote...
Kocha ndiye mwenye mahitaji ya mchezaji ili anapofukuzwa kwa timu kushindwa kutimiza malengo aliyopewa asiwe na la kujitetea. Yeye ndiye anautuma uongozi wamletee mchezaji gani. Na hayo ndiyo madai ya makocha wengi kama Morihno.
 
King_Ngwaba

JF-Expert Member
Jan 11, 2015
1,121
2,000
Kiongozi wa Simba ndugu Magori alishawahi kunukuliwa akisema Wao Viongozi wa Simba ndio wanao sajili timu kwakua wachezaji ni Mali ya Klabu na si kocha na Kocha anaweza kutimuliwa wakati wowote. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Yanga wachezaji wanasajiliwa na uongozi. Nikukumbushe ivi karibuni Simba imesajili Magarasa matatu mfululizo Kama , Junior Lukosa, Chikwende na Peter Muduhwa Sasa utasema tatizo ni uongozi wa Simba na Mbaka Sasa Mabadiliko ya uendeshaji Simba yameshindikana. MO anaiendesha Simba Kama mpenzi na si mwekezaji na kiuhalisia siku yoyote anaweza akaondoka wakabaki wakina Kaduguda na Hans pop ndio wawekezaji.

Mzee Babaa umeletewa Shida za Yanga hasira zako umeshushia kwa Simba.
Toka nilipoona Timu yenu inaamini uwepo wa "WAZEE WA YANGA" kwenye kuendesha Timu na mukawakaribisha Ofisini kufanya Press badae mukawakataa ndiyo nimejua Timu yenu haina kiongozi kila Mtu Kambale Mkubwa Ndevu mdogo Ndevu na kila Mtu Msemaji wamegeuka Kasuku.
 
Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,556
2,000
Kiongozi wa Simba ndugu Magori alishawahi kunukuliwa akisema Wao Viongozi wa Simba ndio wanao sajili timu kwakua wachezaji ni Mali ya Klabu na si kocha na Kocha anaweza kutimuliwa wakati wowote. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Yanga wachezaji wanasajiliwa na uongozi. Nikukumbushe ivi karibuni Simba imesajili Magarasa matatu mfululizo Kama , Junior Lukosa, Chikwende na Peter Muduhwa Sasa utasema tatizo ni uongozi wa Simba na Mbaka Sasa Mabadiliko ya uendeshaji Simba yameshindikana. MO anaiendesha Simba Kama mpenzi na si mwekezaji na kiuhalisia siku yoyote anaweza akaondoka wakabaki wakina Kaduguda na Hans pop ndio wawekezaji.
Ungetoa majibu ya mtoa mada pasipo kulinganisha na Simba ingekuwa ni vyema sana. Mada inahusu Yanga na mleta uzi katoa hoja kuhusu mapungufu ya kiuongozi hivyo ungempinga kwa hoja zinazohusu Yanga au ungemsapoti kwa hoja pia zinazoihusu Yanga.

Kutumia madhaifu ya Simba kuhalalishia yaliyopo Yanga hilo ni tatizo kubwa kwa mashabiki wa Yanga, kupenda kujilinganisha na Simba.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom