Tatizo la Watu kunuka Jasho na Mdomo limekithiri sana

Kuna mkaka nilimkosaga hivi hivi .sasa hivi kaoa, najiuliza kama mimi nilikuwa nakereka kukaa nae tu meza moja mkewe anawezaje kulala nae? Nawaza wanabusiana kweli? Akiongea harufu inayotoka kha!

Yule dada alifata pesa.ila mimi bora nimkose siwezi vumilia ike harufu kisa ndoa kha!
Ungemwambia tuu,isitoshe alikuwa mtu wako wa karibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mshikaji kazini ananuka kama mbuzi aliyekomaa, amesemwa sana na washikaji lakini kama haelewi vile, anaona poa tu. Mimi baada ya kuona kero, nikamnunulia deodorant ya shilling 7,000, akaniuliza ni sabauni gani hii?

Nikamwelekeza namna ya kuitumia huku nikivua shati langu, cha hajabu mpaka leo jamaa hajaitumia ile deodorant kwani ananuka vile vile kama si zaidi. Hivi Mshana Jr mtu kama huyu ni mshirikina au...Yaani hataki kuoga makusudi kwa sababu ya imani zake za kishirikina?
 
Vyakula spicy.

Mtu tangu chai ina spices, mboga, nyama inawekwa spices kibao. Ukitoa jasho linakuwa na harufu.

Dehydration pia. Inabidi unywe maji kwa wingi sana maana hata mdomo mkavu hutoa harufu.

Ila solution kubwa ni maji kwa wingi, nje na ndani.
Kuna watu wanakula ma spice kama watu weupe?wahindi.wazungu etc..ila ni mara chache saana utaskia hao watu wanatoa haruf za ajab...ishu hyo ni usafi tu + kutumia deodorant na mswak....vzur...

wengne sis had tuna lotion za haruf nzur tunapaka mwilin so hata utoke jasho vip..unanukia tuu...unajua pia hata ukipaka deodorant ila ukatoka kasho sehem zingne za mwil.huwa lina haruf so ukipaka lotion nzur..aisee ni unachekelea.sis wengne kunuka jasho ni mwiko....mim nawekeza sana kwenye manukato aisee...kuna madem nangoa sabab ya kunukia tu....
 
Kuna watu wanakula ma spice kama watu weupe?wahindi.wazungu etc..ila ni mara chache saana utaskia hao watu wanatoa haruf za ajab...ishu hyo ni usafi tu + kutumia deodorant na mswak....vzur.
Wahindi jasho lao unalifahamu?

Wazungu hawatumii spices. Wahindi na waafrika hasa wa magharibi majasho yao yana harufu mbaya sana.

From experience.
 
Kuna kademu kamoja Katanga hako kalikuwa kananuka mdomo kama kameza mzoga Mungu wangu.

Ukikapiga kiss hiyo harufu inayopanda hapo khaaaaaaaa nilivumilia mwisho nika run away maana ningekufaaa sio kwa harufu ile

Perhaps inatokea tumboni kbsà

Noted,,kazuri kwa sura na umbo but smells too much trouble
 
Cosmetics na junk foods

Hii point watu hua wanaisahau lakini kwa mfano mtu mzima unalalaje bila kuswaki? Haya shaver zipo kwa nini usinyoe vizuri? Nywele kuanzia kwapani hadi vuzi unakua msafi, haya kwa nini boksa haufui au unapiga wiki nzima na boksa moja hii sio sawa, haya unasafisha kinywa kwa nini ukiweka mswaki mdomoni upige kama unakimbia yaani lazima dawa ifike pembe zote za kinywa,

lazima upitishe brush za mswaki kwenye ulimi tena ukiwa umetoa ulimi kwa nje, lazima ujue kusuuza kinywa kwa maji mara nyingi na mswaki kuepusha harufu ya dawa ya meno, haya mtu mzima anaoga kusafisha vizuri na sabuni tundu za pua hakuna lazima atanuka tu, kusafisha pumbu na katikati ya mapaja hataki, katikati ya vidole vya miguu mtu hasafishi na mbaya zaidi anatwanga soksi au kiatu akiwa hajakausha miguu yake vyema akivua miguu inanuka kama samaki waliooza,

aibu hii, haya kweli hata walau mara mbili kwa wiki kupitisha mouthwash kinywani hasa zile nzuri kama listerin mtu hataki, kunywa maji ya kutosha, kula vitu kama matango harufu ya kinywa kwisha kabisa, mtu usiku tumeshauriwa tule light food ndio mtu anapakia hizo junk food yaani anakula hadi anavimbewa lazima anuke mwili na kinywa.

Usafi watu wanadhani ni kutoka umevaa brands kama LV , Guchi, CK, , Prada au kujipulizia pafyume kopo zima kumbe sio kweli, kwa wale wanaonuka kwapa unashindwaje wakati umelele kukamulia au kupakaa maji ya ndimu au limao yaani utakuta umekaa na mtu unaomba aondoke haraka ili hali ya hewa iwe nzuri, Usafi, Usafi tuudumishe
 
Mnaswaki meno hamswaki ulimi kwanini midomo isitoe harufu?
Mkuu hili ndo tatizo na mimi nilikua hivyo nanuka mdomo lakini mswaki napiga ndipo rafiki yangu wa kweli alinichana live huyu jamaa nampenda mpaka kesho yan ukipiga ulimi mdomo haunukii
 
Mkuu mimi huwa ninatatizo moja ambalo huwa lianinyima amani pindi likitokea(Ni la msimu).

Kunawakati huwa natokwa na harufu kali sana maeneo ya kooni mpaka huwa naihisi kabisa kuwa ni harufu mbaya mnoo.Huwa najikakamua kama vile na kohoa ili kama kuna kitu kitoke lakin huwa inachukua muda..but sometimes huwa vinatoka vijipande vidogovidogo kama mabaki ya chakula vinanuuuuuukaaaaaa balaaa yani sijapata kuona.

Hii hali huwa inanitesa sana kwakweli.Naomba mwenye tiba ya hili tatizo anisaidie jamani.
Periodontal Decease. Nenda kwa daktari wa meno atoe ukoko huo.
 
Madhara ya uchumi wa kati hayo Mkuu.

Dah hili tatizo la Watu kunuka Jasho na Mdomo limekithiri sana kwa Wanaume na wanawake Tatizo litakuwa ni nini Unashindwa kutoa Service kwa mtu kwa jinsi anavyonuka kama beberu hii hali inakera na inaboa sana.
 
Njaa huchangia pia mdomo Kutoa harufu.

Na harufu ya mtu mwenye njaa ni mbaya Sana.

Au ukute mtu "amefunga" halafu aje karibu Yako.. hiii
Pia kukaa muda mrefu bila kuongea, Lotion isiyo moisturizer,kuto kunywa maji ya kutosha hizo ni baadhi ya sababu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom