Tatizo la walimu suluhisho kuanzisha Television ya Elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la walimu suluhisho kuanzisha Television ya Elimu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by RedDevil, May 10, 2010.

 1. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ndugu wajamiiforums, nimekuwa nikifuatilia television moja inayotoa elimu masaa ishirini na nne huku ughaibuni, nikajiuliza hivi kwa nini wizara yetu ya elimu na mafunzo stadi isianzishe television ya elimu itakayo punguza makali ya tatizo la waalimu? Nadiriki kusema hayo kwani huko kijiji nakotoka mimi hali inatisha inatisha wanajamii, watu wanauwezo wa kusoma lakini hawana walimu, nahata hiyo hizo shule za kata nayo ni bahati kuwafikia lakini sasa inshu inabaki walimu, watoto wanaenda shule kucheza na kuongeza miaka tu.

  Natambua mchango mkubwa wa starTV lakini bado nao wanapatikana kwa muda mchache sana kwa ajili ya inshu hiyo hivyo inakuwa vigumu kuwapatia wanafunzi kitu kinachotakiwa. Serikali ingeona umuhimu wa television kama starTV kuipa nguvu(ruzuku) ili iachane na mambo mengine ijikite kwenye elimu inchi nzima. Nadhani itakuwa safi na itawanufaisha watanzania wengi, na kufanya hivyo ndani ya miaka kumi ijayo tutakuwa tunazungumza vitu vikubwa kuliko kuzungumzia namna ya kuondoa ujinga kama saizi kitu amabcho kimekuwa wimbo toka mkoloni.

  Naomba kuwakilisha hoja wanamii.
   
 2. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tupende tusipende hilo ndiyoo suluhisho na nchi hii itabadilika sana. Si hao tu, tuna Watanzania mamilioni kwa mamilioni ambao elimu yao si zaidi ya darasa la saba ambao televisheni za elimu zitawasaidia sana pamoja na wakulima wetu katika kuongeza tija kwa kiwango kikubwa kwa shughuli zao za uzalishaji wanazofanya. Bahati mbaya sana huhitaji zaidi ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka kuweza kufanya na kuleta mapinduzi haya.
   
Loading...