Tatizo la wakulima na wafugaji litakwisha kwa kufanya yafuatayo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,781
2,000
Hata kama huna uhakika kama taifa limekwana mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni moja ya uthibitisho kuwa taifa limekwama na kuonyesha ombwe la uongozi nchini.

Waziri mkuu, mawaziri mwenye dhamana ya kilimo na ufugani, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge, katibu tafara, kata, diwani na viongozi wa vijiji wote hao hawana majibu sahihi ya namna ya kuzuia mapigano ya wakulima na wafugaji, hawamsaidii rais kabisa katika kuiongoza nchi.

Kuna haja ya taifa kufanya utafiti juu ya linacholikumba taifa letu ili kubaini chanzo cha taifa letu kuyumba hata kwa vitu vidogo vinavyostahili kumalizwa kwenye ngazi ya wilaya tu.

Je, tatizo letu liko wapi? liko kwenye katiba yetu, sera za chama tawala, sifa za urais, uteuzi wa wasaidizi wa rais, sheria na kanuni zetu, watendaji wetu au wananchi wenyewe?. Wasomi tupeni majibu ya haya badala ya tafiti zenu za kuonyesha nani anaongoza kura za maoni ya urais 2015 zisizosaidia kutatua kero za wananchi.

Maana utatuzi wa tatizo la wakulima na wafugaji ni rahisi saana kama watu wote kuanzia Rais hadi viongozi wa vijiji wangekuwa wanafanya kazi zao barabara kwa mujibu wa mamlaka yao, usimamizi na sheria imara zinazowaongoza nini kifanyike katika kutatua haraka kero husika za wananchi.

Ufumbuzi: Ili kuepusha migogoro ya wafugaji na wakulima ni kuzuia kabisaaa wakulima wa kutoka vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa mingine wasiende kwenye vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa yenye wafugaji wengi kwenda kutafuta mashamba, na wafugaji kutoka vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa mingine wasiende na mifugo yao kwenye vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa mingine kutafuta malisho ya mifugo yao fulu stopu.

Ni vema matatizo ya wafugaji yatafutiwe ufumbuzi ndani ya vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa yao ya asili kwa kuwa watu wa aina moja wanaelewana kwa tabia na tamaduni zao kuliko watu wa wilaya na mikoa mingine. Na watu wanaotoka wilaya na mikoa mingine wasiende kabisaaa kwenye vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa mingine inayofahamika kuwa na mifugo mingi kwa lengo la kwenda kutafuta mashamba hata kama mikoa hiyo ina mabonde mazuri yanayofaa kwa kilimo, maana "like desolves like" yaani wenye mifugo wahamie kwa wenye mifugo na watafuta mashamba wahamie sehemu wanazoendesha kilimo, halafu inabaki "batter exchange" ya mazao ya kilimo na mazao ya mifugo kwa wanaohitaji kama vile Dar es Salaam wanavyopata nyama na maziwa ya Tanga fresh ingawa hatufugi ng'ombe, Je, kwanini hapa Tanzania vijiji, kata, tarafa, wilaya na mikoa iwe na mvurugano wa wakulima na wafugaji kwa wakati mmoja? Utashangaa hata Dar es Salaam unakuta watu wanafuga ng'ombe, mbuzi, kondoo, punda, kuku, bata, n.k. Huu ni msiba wa mipango na uongozi sawa na misiba mingine kwani viongozi wetu wanashinda Marekani, Ulaya, na Afrika Kusini kila siku kwanini wanashindwa kuiga kutoka huko japo vile vitu vichache vinavyohitaji maamuzi tu?

Kwanini msukuma wa Mwanza aende Pwani na kundi kubwa la ng'ombe? Ni kwa nini mkulima wa Kongwa aende Kibilashi akatafute mashamba ya kulima vitunguu? Ni kweli nchi yetu ni moja na kila mtu ana haki ya kuishi popote ilimradi asivunje sheria, lakini je na mifugo nayo inayo haki hiyo ya kuishi popote kwa mujibu wa katiba na sheria zetu? Kwanini wafugaji wa shinyanga, Mwanza, na Arusha waachwe wasambae na ng'ombe wao nchi nzima? Ni demokrasia gani hiyo inayomlazimisha mpogoro wa Morogoro akubali kwa lazima mifugo ya Mmasai kwenye maeneo yake? utamaduni wake kwa miaka dahari kwa dahari hauruhusu kufuga ng'ombe, na Mmasai naye utamaduni wake hauruhusu kulima kwanini umpelekee mashamba mlangoni kwake ili kazi yake ya kuchunga iwe ngumu sana? huku ukifahamu kuwa maeneo yanayofaa kwa kilimo ni yale maeneo yanayobaki na majani ya malisho na maji wakati wa kiangazi ukifika, mashamba yanapunguza maeneo ya kuchungia na mashamba pia yanaongeza ugumu wa kuchunga ili kuepusha mazao ya watu yasiliwe na mifugo. Hili nalo linahitaji elimu gani kufahamu?

Hili ni ombwe la uongozi nchini lisilofahamika chanzo chake linalopaswa kurekebishwa haraka. Kama chanzo chake ni katiba, chama, rais, mamlaka ya uteuzi, watendaji, sheria, au rushwa hatua za haraka zichukuliwe kurekebisha hali hii badala ya kuendelea kupoteza watu wetu kwa mambo yanayozuilika.

Rais teua mimi uone moto wangu, ha, ha, ha.
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,356
2,000
No body is serious about it, kinashindikana nini kujifunza kutoka kwa mataifa ya wenzetu wanafanyaje, wakati viongozi wa wizara husika kila kukicha wapo ughaibuni wakijinadi kuwa wamekwenda kwenye mafunzo ya namna bora ya kufuga na kulima.

Ukweli ni kuwa hawa viongozi tulio nao wengi wao wananufaika na migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa, hainiingi akilini serikali yenye kila kitendea kazi inashindwa kutatua migogoro ya hayo makundi mawili
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,781
2,000
No body is serious about it, kinashindikana nini kujifunza kutoka kwa mataifa ya wenzetu wanafanyaje, wakati viongozi wa wizara husika kila kukicha wapo ughaibuni wakijinadi kuwa wamekwenda kwenye mafunzo ya namna bora ya kufuga na kulima.

Ukweli ni kuwa hawa viongozi tulio nao wengi wao wananufaika na migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa, hainiingi akilini serikali yenye kila kitendea kazi inashindwa kutatua migogoro ya hayo makundi mawili
Mtu mmoja aliniambia maeneo yaliyobaki yenye afadhali japo kidogo kwa kuwa na malalamiko machache nchi hii ni jeshini (JWTZ), wafanyakazi wa TRA, wabunge, benk kuu, ikulu na wafanyabiashara wakubwa tu basi, kulikobaki koote manzanyange.
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Umekosea
Ufumbuzi wowote wa hili tatizo lazima ulenge kuongeza uzalishaji wa nyama na mazao ya shambani. Kwa wazo lako hili sitashangaa nyama ikaadimika na kuanza kuuzwa 15000 kwa kilo
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,781
2,000
Umekosea
Ufumbuzi wowote wa hili tatizo lazima ulenge kuongeza uzalishaji wa nyama na mazao ya shambani. Kwa wazo lako hili sitashangaa nyama ikaadimika na kuanza kuuzwa 15000 kwa kilo
He he he! wewe unashangaza sana!, hivi wewe unajali nyama iwe bei nafuu badala ya maisha ya watu wanaouana, kuchomeana nyumba na kutiana vilema? Unachojali wewe ni bei ya nyama tu sio watu wanaokufa, this is shame. Katika nchi yenye bahari, maziwa, mito na mabwawa mengi swala la nyama sio issue, ukikosa nyama ya ng'ombe si utakula samaki, kuku na swala? maana sio nchi zote zinafuga ng'ombe lakini nyama zote zipo. Na kwataarifa yako nyama zinazoliwa hapa mjini zinaletwa kutoka Shinyanga, Mwanza (ng'ombe, sato, sangara), Tanga, Dodoma, Singida (kuku), Afrika kusini, n.k. Hatuhitaji nyama ya bei nafuu kwa kubadilishana na maisha ya wakulima na wafugaji wanaouana kila siku.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom