Tatizo la usugu wa magonjwa na jinsi ya kukabiliana nalo

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,162
701

TATIZO LA MAGONJWA SUGU NA JINSI YA KUZUIA USUGU

drug resistance 2.jpg drug resistance 4.jpg

IMEANDIKWA NA:
S&E HEALTH SOLUTIONS
WATAALAM NA WASHAURI WA AFYA, UREMBO NA VIPODOZI

UTANGULIZI
Umewahi kusikia kuhusu Malaria sugu? Maambukizi katika nia ya mkojo (U.T.I.) sugu? Homa ya matumbo (Typhoid) sugu?
Usugu wa ugonjwa ni ile hali ya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa kutokufa vyote kwa dawa au matibabu na hivyo kufanya ugonjwa kutopona kabisa. Matokeo yake ni vijidudu au ugonjwa kuendelea kuwepo mwilini hata kama mtu atatumia dawa vizuri kabisa. Tatizo la usugu linaweza likajitokeza kwa magonjwa mbalimbali yanasosababishwa na bakteria, protozoa, virusi nk kama vile Malaria, Maambukizi katika njia ya mkojo (U.T.I.), Kifua kikuu, Kansa, Ukimwi, Kisonono, Kaswende na mengineyo mengi.
Usugu huo hupelekea dawa za kawaida ambazo ndizo hutumika kuutibu ugonjwa kushindwa kutibu ugonjwa huo na kuhitaji dawa nyingine mpya au ya juu zaidi.
Tatizo la usugu wa magonjwa hupelekea kupungua kwa ufanisi wa dawa na hata dawa kukosa kabisa thamani ambayo ilikuwa nayo zamani.

UKUBWA WA TATIZO LA USUGU WA MAGONJWA
Tatizo la usugu wa magonjwa ni kubwa sana. Ni kubwa kiasi cha kufanya dawa nyingi ambazo zilikuwa zikitumika sana zamani kuanza kuachwa na kuondolewa kabisa katika matumizi. Unazikumbuka dawa za zamani kama vile Chloroquine na Tetracycline? Unaziona sana siku hizi?
Dawa zilizokumbwa zaidi na tatizo hili ni dawa za kutibu magonjwa ya bakteria, malaria, kansa na ukimwi.
Pia tatizo hili linaendelea kukua siku hadi siku. Matokeo yake ni kufeli kwa matibabu, kuongezeka kwa magonjwa, vifo na gharama kubwa za matibabu.
Mbaya zaidi ni kwamba usugu wa magonjwa huweza kuambukizwa kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mtu mwingine, na kumpelekea mtu huyo kuwa ugonjwa sugu. Na pia vijidudu vya magonjwa vinaweza kuwa na usugu kwa dawa nyingi au zote za kundi fulani la dawa.
Endapo ushirikiano na juhudi kubwa kulikabili tatizo hili hazitachukuliwa basi litakuwa kubwa zaidi na kuleta matatizo mengi na makubwa zaidi.
Kushirikiana ili kuzuia na kutokomeza tatizo hili ni jukumu letu sote; Wagonjwa, Watoa huduma za afya wote, Serikali na jamii nzima kwa ujumla.

SABABU ZA MAGONJWA KUWA SUGU
Usugu wa magonjwa hutokea pale vijidudu vya magonjwa vinapojijengea uwezo wa kupambana na dawa na kuweza kuepuka kuuwawa na dawa hiyo. Matokeo yake ni kwamba vijidudu hivyo kuendelea kuishi hata kama mtu atatumia dawa hiyo vizuri, na hivyo ugonjwa huo hautapona moja kwa moja kwa dawa hiyo.

Vitu vinavyosababisha au kusaidia usugu wa magonjwa ni pamoja na
1. Kutofanya vipimo sahihi na kupata uhakika wa vijidudu vilivyosababisha ugonjwa na dawa ambayo itawaua vizuri kabisa
2. Kutotumia dawa sahihi zaidi kwa vijidudu au ugonjwa husika
3. Mgonjwa kutotumia dawa vizuri. Hii ni pamoja na kutomeza dawa kwa wakati, kutomeza dozi zote katika siku na kutomaliza dozi na dawa zote
4. Muingiliano wa dawa na dawa zingine, magonjwa na hata vyakula hivyo kupunguza ufanisi wa dawa na kuviwezesha vijidudu vya magonjwa kutokufa na kuwa sugu
5. Kuambukizwa vijidudu sugu kutoka kwa mgonjwa mwingine

MADHARA YA USUGU WA MAGONJWA
Usugu wa magonjwa na kushindwa kwa dawa kuua vijidudu vya magonjwa na kutibu magonjwa kuna hasara kubwa sana kiuchumi na kiafya. Madhara ya usugu wa magonjwa ni pamoja na
1. Kufeli kwa matibabu na kuendelea kwa magonjwa, maumivu, homa na matatizo mengine ya kiafya
2. Kuenea zaidi kwa magonjwa na kuongezeka kwa mzigo wa magonjwa katika jamii
3. Kuongezeka kwa idadi vifo
4. Wagonjwa kutumia muda mwingi zaidi kutibiwa na/au kulazwa hospitali
5. Kuongezeka kwa gharama za matibabu kutokana na kutakiwa kutumia dawa zenye uwezo wa juu zaidi na hivyo kugharimu gharama kubwa zaidi
6. Hasara katika kampuni na viwanda vya kuzalisha na kuuza dawa kutokana na kushindwa kuendelea kuuza vizuri dawa zao


Madhara ya usugu wa magonjwa yanamuhusu kila mtu katika jamii. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anachukua hatua ili kuzuia na kulitokomeza kabisa tatizo hili.

JINSI YA KUZUIA NA KUTOKOMEZA TATIZO LA USUGU WA MAGONJWA
Mpaka sasa nina imani umelielewa tatizo la usugu wa magonjwa na magonjwa sugu. Pia nina imani utakuwa tayari kukabiliana nalo ili kulizuia na kulitokomeza kabisa.
Tunaweza kulizuia na kulitokomeza kabisa tatizo hili kwa
1. Kufanya vipimo sahihi na kupata uhakika wa vijidudu vilivyosababisha ugonjwa na dawa ambayo itawaua vizuri kabisa
2. Kutumia dawa sahihi zaidi kwa vijidudu au ugonjwa husika. Na hili hujulikana baada ya kufanya vipimo na majaribio ya maabara
3. Kutumia dawa vizuri. Hii ni pamoja na kumeza dawa kwa wakati, kumeza dozi sahihi, kumeza dozi zote katika siku na kumaliza dozi na dawa zote.
Tumia dawa zote kama ulivyoelekezwa na daktari, mfamasia, nesi na kadhalika
4. Wataalam wa dawa kushirikiana na madaktari ili kutoa dawa bila kuwa na muingiliano wa dawa na dawa zingine, magonjwa na hata vyakula.
Pia wakati wa matibabu na kupewa dawa mgonjwa aeleze kama ana magonjwa mengine na kuna dawa zingine anazitumia
5. Kujikinga ili kutoambukizwa vijidudu vya magonjwa kutoka kwa wagonjwa wengine
Hapa ni suala la kuzingatia kanuni zote za afya za kuzuia magonjwa na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
6. Kutoa elimu kwa umma na kushirikiana juu ya tatizo la usugu wa magonjwa na jinsi ya kulitokomeza

Tatizo la usugu wa magonjwa na kufeli kwa dawa ni kubwa lakini linaweza kutokomezwa kabisa. Jamii nzima tushirikiane ili kutokomeza tatizo hili na tuwe na afya bora.
 

Attachments

  • drug resistance 3.jpg
    drug resistance 3.jpg
    9.4 KB · Views: 62
  • drug resistance 5.jpg
    drug resistance 5.jpg
    9.7 KB · Views: 64
  • drug resistance 6.jpg
    drug resistance 6.jpg
    4.6 KB · Views: 60
  • drug resistance 7.jpg
    drug resistance 7.jpg
    5.8 KB · Views: 62
  • DRUG RESISTANCE 8.jpg
    DRUG RESISTANCE 8.jpg
    7 KB · Views: 58
  • DRUG RESISTANCE 9.jpg
    DRUG RESISTANCE 9.jpg
    6.5 KB · Views: 61
  • drug resistance.jpg
    drug resistance.jpg
    8.4 KB · Views: 56
Back
Top Bottom