Tatizo la usafiri stand ya Ubungo lawama nawatupia kamanda Awaz na SUMATRA

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,038
2,000
hali halis ilivyo kwa hivi sasa ubungo ni mateso kwa abiria na haswa watoto wadogo. hii inasababishwa na agizo la sumatra kukataza gari zote zisizo na sticker ya sumatra inayouzwa laki tano zisipakie abiria haswa kwa kipindi hiki cha dharura. huku zoezi hili zima likishikiwa kidedea na kamanda awaz. matokeo yake zilizoingia ndani ni zile chache zenye sticker huku hazikidhi masharti ya safari ndefu kama kuwa na ac tv mikanda. badala yake zimezuka stand bubu za kumwaga huku abiria wakitoa ushirikiano kwa madereva na makondakta wanaopakia kinyemela. naishauri sumatra na kamanda awaz wafikirie mara mbili katazo lao. pia wale wote wanaotaka kwenda moshi arusha nairobi kwa kesho mnione inbox .jana j
usiku nilipokuwa natoka moshi kuja dar nimekutana na maelfu ya gari zilizopakia kinyemela. sumatra ibuni vyanzo vipya vya mapato
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,481
2,000
Hapa tatizo ni poor planning ya mamlaka zetu pamoja na sisi abiria wenyewe (i.e. Watanzania). Kwani kuna asiyejua demand na supply ya hili eneo kwa mwezi December!?
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
173,928
2,000
Kumbe abiria wengi mabasi machache. Si kulikua na habari biashara ya mabasi kipind hiki imedorora sana. Wametokea wap hao abiria wengi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom