Tatizo la unyumba linaweza kusababisha ndoa kuvunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la unyumba linaweza kusababisha ndoa kuvunjika

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msongoru, Sep 23, 2008.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  KUNA sababu nyingi zinazokubalika kisheria kuvunja ndoa ambayo ilifungwa kihalali. Katika mfululizo wa makala hizi siku za nyuma, tuliwahi kujadili kwa kifupi sababu zote na ziada zake zinazokubalika mbele ya jicho la sheria kuruhusu ndoa husika kufikia kikomo.


  Moja ya sababu hizo ilikuwa ni mwanamume kukosa uwezo wa kutenda tendo la ndoa kutokana na kukosa nguvu za kumwezesha kufanya hivyo. Kimsingi ndoa ya mume wa sifa hii mbele ya sheria, hutambulika kama ndoa batilifu, yaani itakuwa batili mpaka hapo mahakama yenye mamlaka itakapotangaza hivyo kufuatia maombi ya kuvunja ndoa ambayo yatakuwa yamewasilishwa na mke husika.


  Ni kwamba, sheria inatoa fursa kwa mwanamke kuwasilisha maombi ya kubatilisha ndoa husika kwa sababu tu mume wake huyo hana uwezo wa kumwingilia kwa ajili ya kutimiliza tendo la ndoa jambo ambalo ni haki ya msingi miongoni mwa wanandoa.

  Ninatahadharisha kuwa somo hili lisieleweke au kunukuliwa vibaya, simaanishi mume kushindwa kumridhisha mkewe, bali mume kushindwa kabisa hata kuwa na hisia za kukutana na mkewe pindi mke anapohitaji.


  Pamoja na kwamba sheria imetoa fursa ya kuomba kuvunja ndoa ya aina hiyo, sheria hiyo hiyo haikuchelea kuweka vigezo ambavyo ni sharti vithibitishwe ili kuruhusu maombi ya aina hiyo yakubaliwe na kufanyiwa kazi na mahakama husika.


  Kwamba, ili kasoro hiyo iweze kukubalika kama sababu ya kuvunja ndoa, ni lazima mume awe ameshambuliwa na uhanithi kabla au wakati wa kufungwa kwa ndoa husika. Hi ni kusema kwamba, ikiwa uhanithi huo ulimpata mume huyo baada ya maisha ya ndoa kuchanganya, hauwezi kuwa sababu ya kukubaliwa kwa ombi la kuvunja ndoa husika.


  Sheria imeweka sharti hili kwa makusudi hasa kwa kuzingatia hali na sura halisi ya maisha ya mwanadamu ambayo yamezungukwa na maradhi mbalimbali ambayo baadhi yake husababisha hali ya mwanamume kutojiweza kijinsia. Mfano mzuri wa magonjwa ya aina hiyo ni kisukari.


  Lakini kwa upande mwingine, sheria inaruhusu mke kuomba talaka kama ikitokea mume kupata uhanithi kwa muda wa mfululizo wa miaka mitano baada ya ndoa kufungwa. Kwa mujibu wa sheria hiyo, haitojali kwamba umempata wakati gani. Lakini sheria hii inaweza kutumika kwa zile ndoa ambazo zilifungwa chini ya misingi na sheria ya kimila pekee.


  Katika kutumia kigezo au sababu hiyo kuvunja ndoa husika, mahakama hulazimika kuhusisha ushahidi na maoni ya kitaalamu kutoka kwa daktari aliyefuzu kuthibitisha kuwa uhanithi huo hauwezi kutibika kwa namna yoyote.


  Hii ina maana ya kwamba, inawezekana kabisa uhanithi huo ukawa unatibika, lakini katika hali ya kushangaza mume akaamua kukataa matibabu kwa sababu anazozijua mwenyewe, mahakama itaruhusu ombi la kuvunja ndoa hiyo hata kama tatizo hilo lillimpata mume wakati ndoa husika imekwishafungwa.


  Kwa upande mwngine, maradhi kama hayo yanaweza pia kumshambulia mke ambaye anaweza kuwa na hali fulani katika viungo vyake vya uke ambayo inaweza kusababisha asiweze kuingiliwa na mumewe. Vivyo hivyo sheria inasema kwamba kutibika au kutokutibika kwa ugonjwa huo wa mke, kunaweza kuwa sababu ya mahakama kuruhusu kusikilizwa kwa ombi la kuvunja ndoa husika hata kama tatizo hilo lilionekana baada ya maisha ya ndoa ya wawili hao kushika kasi.


  Hivyo hata mume anaweza kuwasilisha maombi yake katika mahakama na kufanikiwa kuvunja ndoa hiyo, amri ambayo hutolewa na mahakama ya sheria yenye mamlaka ya kusikiliza kesi husika.
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa ninayemfahamu alioa mke na wakafanikiwa kupata watoto wawili baadae jamaa akapata ajali iliyopelekea kupooza na hatimaye kupoteza kabisa uwezo wa kumuingilia mke wake.
  Je katika mazingira kama haya mwanamke akifungua shauri la kuomba ndoa ivunjwe mahakama itakubali ukizingatia wana watoto tayari wanaohitaji malezi ya baba na mama hata kama mume hawezi kumuingiliamke tena??
   
 3. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2008
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapa kwa kweli ubinadamu nao inabidi uplay part. kwa kweli kwa maoni yangu mke angevumilia tuu waishi wote mpaka mwisho wao. Na hiki ndo kile kipengele kisemacho "ntapenda kwa shida na raha". Kwa kweli kama jamaa anapenda na kumjali hicho ni kitu kidogo ambacho anaweza kukimaliza njia mbadala.
   
 4. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  .

  ..Lorain, nakubaliana na wewe kuwa ubinadamu utumike lakini do you think katika mazingira ya kutegemea ubinadamu tu yaweza kuwa ni njia sahihi ya mwanamke kuendelea kubaki ndani ya ndoa yake na kumuheshimu mume wake kama hapo awali? Njia mbadala za mwanamke kujitosheleza yaweza kuwa ni ubunifu wake mwenyewe lakini je unadhani mume wako atachukuliaje jambo hilo? Suppose anakuuliza swali kuwa " Mke wangu tangu nimepata matatizo ni miaka 2 sasa hivi unamudu vipi kuishi bila kufanya mapenzi?" Unadhani utamwambia ukweli kuwa una njia mbadala unazotumia? au utasema uongo kwa mumeo unaejidai unampenda?

  Nadhani mtoa mada Msongoru naomba ajaribu kulizungumzia hili katika upande wa kisheria zaidi ili kama kutakuwa na mazingira ya mume kukwazika basi ajue kuwa anatakiwa kufanya nini??
   
 5. C

  Chief JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Je, mwanamke kukosa uwezo wa kutenda tendo la ndoa?
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Inauma kwa kweli,...kumbe kuambiana "for better or worse til death do us apart" ni geresha tu eeh?...!
   
 7. Mgirik

  Mgirik JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2014
  Joined: Apr 27, 2013
  Messages: 10,815
  Likes Received: 3,486
  Trophy Points: 280
  Somo zuri sana
   
 8. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2014
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,439
  Likes Received: 14,098
  Trophy Points: 280
  Kuvuja kwa pakacha
   
Loading...