SoC01 Tatizo la unyanyasaji wa wanafunzi katika vyombo vya usafiri

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 29, 2021
81
158
Kama umepata nafasi ya kuzaliwa , kusoma au kuishi katika mkoa wa Dar es Salaam, utakubaliana na Mimi ya kwamba wanafunzi hupata wakati mgumu Sana wakiwa wanaenda mashuleni siku za wiki hasa hasa kwenye magari ambayo yaanaelekea safari za Kariakoo,mnazi mmoja na Muhimbili.

Shule nyingi hapa Dar es Salaam hasa za serikali Kama Shule ya Kisutu, Benjamin Mkapa,Uhuru na nyinginezo zinazopatikana mjini hazina vyombo vya usafiri Kama Mabasi kwajili ya kusafirisha wanafunzi wao. Hii inaathiri Sana wanafunzi wanaosoma kwenye shule hizo, kwasababu inawabidi wagombanie sana ili waweze kupata gari, kinyume na hapo hawataweza kuwahi kufika shule kwa wakati unaotakiwa, kitu ambacho huwasababisha wapewe adhabu au kuchapwa bakora pale wanapofika shule.

Hii inawasumbua na kuwatesa Sana wanafunzi hasa wale wanafunzi wenye umri mdogo sana.
Kutokana na safu iliyochapishwa tarehe 10/06/2016 na gazeti za nipashe kupitia IPP Media limesema kuwa tatizo hili limekuwa tatizo sugu Sana kwasababu lineendelea kwa muda mrefu bila ufumbuzi wowote na pia Cha kusikitisha zaidi Ni kwamba imeonekana Jambo la kawaida kuona madereva na makondakta kuzuia wanafunzi kupanda hizo
Daladala, na hata hatujali tena Kama ilivtokuwa hapo awali. Pia mwandishi huyo anaongeza kwenye safu hi kuwa mfumo wa elinu ndio unachangia tatizo hili.

Kwasababu unakuta mwanafunzi anaishi Tabata lakini anasoma Kibaha . Mfano mtoto anaweza kuchaguliwa kwenda kusoma shule ya secondary ya Kisauke huko madale wakati yeye anaishi Kimara au Kibaha.

Mimi pia nilipata bahati ya kusoma hapa dar es salaam, nilisoma mwaka 2017-2019 katika shule ya Benjamin William Mkapa pale Kariakoo. Mimi pia nilipitia hizi chamgamoto wakati wa kwenda shule. Ilikuwa inanilazimu kuamka saa tisa au saa kumi kujiandaa na kuondoka saa kumi na moja kuelekea shule ili niweze kupata Daladala kwa urahisi na bila ya usumbufu.

Wakati mwingine hata ukitoka saa kumi na moja au kumi na moja na nusu utakuata unasumbuliwa bado hasa nyakati zile za mitihani kwasababu wanafunzi wengi huamka mapema
nyakati hizo ili wasichelewe mitihani. Hivyo unajikuta umewahi kuamka na bado unachelewa kufika shule.


Kinachoumiza Sana Ni kwamba walimu wanakosa uelewa, walimu hufikiri kwamba mwanafunzi akichelewa muda wote Ni Sababu ya uvivu wake, lakini wakati mwingine kunasababu zilizo juu ya uwezo wa mwanafunzi zinazomfanya achelewe.
Unyanyasaji wa aina nyingine ambao niliuona ambao wanafunzi wanapitia katika vyombo vya usafiri, Ni pale wanapolazimishwa siku zote kusimama na kupisha watu wazima kutoka kwenye viti vya kukalia vya kwenye madaladala. Najua watu wengi hawatakuwa pamoja na mimi kwenye hili, lakini kabla hujanipinga naomba nikuelezee ninachomaanisha.

Tamaduni yetu ya kitanzania inatutaka tuwe na heshima kwa wakubwa zetu, na watu wengi wametafsiri hii kuwa pamoja na kusimama na kumpisha mtu mzima ili akae kwenye siti, lakini inaweza isiwe hivyo. Kuna makundi ambayo yanapaswa kupewa heshima hiyo na sio na wanafunzi tu, bali na watu wazima pia.

Makundi hayo ni Wamama wenye ujauzito, watu wenye umri mkubwa sana au wazee sana, walemavu na mtu mgonjwa. Hayo ndio makundi ya muhimu Sana kupewa nafasi kama hiyo na sio watu wote wazima. Nasema hivyo kwasababu wanafunzi wanachoka Sana jamani, wanaamka asubuhi mapema Sana wengine saa kumi, wengine saa kumi na moja na kwenda shule na pia wanachelwa sana kurudi.

Kutokana na hizi purukushani za Daladala wengine hurudi usiku kabisa Kama kwenye saa moja au saa mbili. Utasema watu wazima wanachoka pia Tena Sana wanondoka asubuhi wanafanya kazi mpaka Jioni hivyo wanachoka pia. Sawa ni kweli, lakini ki ukweli wanafunzi wanachoka kuliko sisi kwasababu wao wanatumia Sana akili wakati wa kusoma kuliko watu wazima. Watu wazima wakiamka asubuhi wanaenda kazini au kwenye mihangaiko, na mihangaiko yetu mingi ni ya kutumia nguvu kama vile kubeba zege , kuuza chakula , na kazi nyinginezo nyingi.
Kutokana na haya matatizo watoto wetu wamekuwa wakisumbuka sana wakati wakitafuta elimu.

Na mimi nimeona hili tatizo na nimeona vyema kuweza kutoa mawazo ya jinsi tunavyoweza kuyatatua haya matatizo. Njia ya Kwanza ni kufanya nauli zinazolipwa na wanafunzi zifananane na zile za watu wazima (wakubwa): Makondakta wa madaladala wamekuwa wakikataa kubeba wanafunzi wengi kwasababu ela yao ya nauli Ni ndogo sana na haina masalai ukiilinganisha na nauli ya mtu mzima. Hivyo nauli hizi za wanafunzi zikipandishwa na kuwa sawa na zile za watu wazima itasaidia wanafunzi kupewa haki sawa na watu wazima na kupunguza Kama sio kuondoa kabisa usumbufu kwa wanafunzi wakati wa kwenda shuleni.

Njia nyingine Ni kwamba Serikali iweze kuwekeza pesa na kununua mabasi ambayo yatakuwa yakisafirisha wanafunzi wanaosoma kwenye shule za Serikali kuelekea mashuleni na wakati wa kurudi nyumbani. Serikali inaweza ikawalipisha wanafunzi nauli ndogo ili kusaidia kuchangia huo uwekezaji, au kuisaidia serikali kurudisha pesa yake iliyowekeza kwa kununua au kukodisha hayo mabasi. Haya magari yanaweza pia kufanya biashara za kubeba abiria wengine pale ambapo wanafunzi wanakuwa tayari wameshafika shuleni.

Pale ambapo inapokuwa imeshamaliza kazi ya kuwaleta
wanafunzi mashuleni inaweza ikaingia barabarani kufanya biashara ya kubeba abiria huku ikisubiria wakati wa jioni ili kuwarudisha wanafunzi majumbani kwao. Hi ni njia nzuri ambayo serikali inaweza kuitumia kuingizia kipatao. Hii ni njia nzuri kwasababu inaua ndege wawili kwa jiwe moja, nikimaanisha kuwa mbali na Kusaidia kupunguza tatizo la usumbufu kwa wanafunzi kwenye vyombo vya usafiri, pia itasaidia kutoa ajira kwa watu hususani madereva na Makondakta.

Njia nyingine, serikali itoe ruzuku kwa Daladala zinazoongoza kwa kubeba wanafunzi. Hapa serikali itahitajika mfumo wa dole gumba, ambapo wanafunzi watakuwa wakitambulika kwamba hawa Ni wanafunzi was Shule Fulani pale tu ambapo wataweka dole gumba kwenye mashine. Hizi mashine zitasambazwa na serikali kwenye Daladala zote na wanafunzi watakaopanda watatakiwa kulipa nauli ya shilingi Mia mbili tu kama kawaida na kisha kupata risiti.

Serikali itatoa asilimia Fulani Kama ruzuku kwa Daladala zilizoweza kupandisha wanafunzi na hao wanafunzi wakaweka dole gumba katika hizo mashine. Na kwa kila kichwa , serikali itatoa shilingi 300/= Kama ruzuku ambapo ukijumlisha na nauli ya mwanafunzi anayolipa , shilingi Mia mbili jumla Ni shilingi 500/= na kwa Daladala ambazo zitaongoza kwa kubeba wanafunzi wengi zitaongezewa asilimia au pesa zaidi kama nyongeza au pongezi kwa kuonyesha juhudi na mchango wao katika kutokomeza tatizo hili kuu la unyanyasaji wa wanafunzi katika vyombo vya
usafiri. Hii njia itaondoa hili tatizo na zaidi
itafanya wanafunzi wapewe kipaumbele zaidi kwenye hivi vyombo vya usafiri.

Tunasema kuwa Watoto ni taifa la kesho, na ndio tunawategemea waje wawe viongozi wa kuongoza nchi yetu na kuifikisha nchi yetu ya Tanzania kwenye mafanikio ya kiuchumi na mabadiliko mbalimbali tunayoyahitaji, basi tuweze kuwalea na kuwaheshimu wakiwa bado wako shuleni tuwasaidie ila waweze kwenda shule na kusoma bila usumbufu wowote.
 
Kwanza kitu muhimu ambacho serikali wanaweza kufanya Ni kutangaza kuwa hakuna mwanafunzi anayetakiwa kusoma mbali na eneo analoishi kwa maana hakuna sehemu inayokosa shule mfano mtoto anaishi chanika shule anasoma shule ya msingi kisutu posta je chanika hakuna shule hivyo kukamilisha hili serikali inatakiwa kuwapa uhamisho wanafunzi wote wanaosoma mbali na wanatumia daladala kufika shuleni. Kuwalipia nauli Ni kupoteza hela Bora itumike kujenga madarasa
 
Back
Top Bottom