Tatizo la ummeme: Badra Masoud wa TANESCO -tatizo ni Ukosefu wa fedha...... JK- tatizo ni Ukame!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la ummeme: Badra Masoud wa TANESCO -tatizo ni Ukosefu wa fedha...... JK- tatizo ni Ukame!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by meddie, Jul 21, 2011.

 1. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  Leo asubuhi Badra masoud akihojiwa channel ten amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuwekeza ktk vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme nchini.
  kwa upanda wake Jk akihojiwa bbc amesema tatizo ni ukame na kwamba yeye hanauwezo wa kumuomba mungu alete mvua, hasa wakati huu baada ya kuondokewa na msaada wake sheik yakhaya!
  Kwa tofauti hii ya maelezo na mtazamo kuhusiana na chanzo cha tatizo la umeme na kwa jk kuamua kutembea nje kipindi taifa lipo gizani, inaashilia hasivyojali na hasivyo kuwa na jibu kamili wala mkakati wa kumaliza tatizo la ukosefu wa umeme nchinii. hii nikusema hatakama serikali itapewa mwaka mzima acha week tatu, hakutakuwa na majibu ya utatuzi wa jambo hili


  lkn jambo jingine lakushangaza ni kuona ktk kipindi hiki ambapo taifa limogizani, hali ya maisha ikipanda, raisi wetu akichanja mbuga kama hana akili mzuri. Majeshi yetu yapo kimywa wakiendelea kuponda hela za walipakodi!
  Kama kweli jeshi bado ni la wananchi watz nategemea wasikae kimya ktk hali kama hii. Natumai wote tunakumbuka kauli iliyotolewa wakati wa uchaguzi na mkuu wa majeshi kupitia mnadhimu wake mkuu Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo ya kuvitaka vyama vya siasa kukubali matokeo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba na kuonya kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote atakayejaribu kuyakataa matokeo.

  Kama kauli hii ilitokana na uzalendo na upendo kwa TZ na siyo unafiki na kumkingia kifua JK na kuwatisha wananchi na vyama vilivyokuwa vikishiriki uchaguzi. basi wakikae kimywa wakati huu, bali watoe tamko pia!!

  vinginevyo shiit kwao!!

   
 2. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Haya yote ni mchakato wa laana kutenda kazi!!!!!!!!!!!!!! Taifa lenye viongozi wake kutegemea majini; sasa mwenye majini amekufa, sijui kama hayo majini bado yanatii yule aliyerithi mkoba???????????????? Eeeeeeeeeeeeee Tanzania nakulilia kwa kuuzwa kwa majini na makafara!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama tatizo ni fedha ile TSh 1bn/- ya kuhonga wabunge ilitoka wapi?
   
 4. k

  kakolo Senior Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  WATANZANIA TUMELAANIWA. Viongozi wetu waliapa kwa kutumia vitabu vitakatifu kuwa watatekeleza haya na yale, then wanakiuka waliyo yaahidi, guess what waki-resign tena watu wanazimia wakiwaomba wabadili nia wabaki kutuongoza. Chenge alivyotolewa uwaziri alienda jimboni kwake wapiga kura wake waliandamana na kumlaki kwa msululu wa magari kumfarji yaliyomkuta. Kikombe cha babu kina hitajika kulikomboa taifa.
  Mawazo yangu.
   
 5. B

  Bateko Senior Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli sijaelewa if mkuu alijibu swali aliloulizwa alijuua maana yake, coz swali lilikuwa jepesi sn but kwa alivyojjieleza seems waTz kutoka gizani ni ndoto za alinacha
   
 6. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 7. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wakati matokeo ya uchaguzi znz yanakaribia kutangazwa pale Bwawani hotel Zanzibar, watu walikuwa wamekusanyika mpaka saa tatu usiku, askali walipewa amuri ya kuwaondoa raia, lakini walikuwa wanawambia raia msiende mbali mkae karibu mpaka matokeo yatangazwea bega. Hii ilizihilisha jinsi askali wanavyofahamu udanganyifu wa ccm na hivyo walikuwa begakwa bega na raia.
  hapa kwetu askali ni majuha, hawana msaada wowote hata raia wanapopigania mambo yenyemaslahi kwao pia!!
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Sioni usichokielewa ni nini hapo? Hakuna asiejuwa kuwa kina cha maji Mtera kimepungua na umeme unaozalishwa kule kwa sasa ni asilimia kumi tu ya kiwango chake na hilo limesababishwa na ukame. Na ili kuondokana na utegemezi wa vyanzo vya umeme unaotokana na maji inabidi uwe na fedha za kununulia mitambo itayoendeshwa na aidha Gas au Mafuta au Upepo au Makaa. Kwa hiyo yote yana ukweli na hayapingani unless uwe ufaham finyu.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mtera kabla ya hili sekeseke ilikuwa inazalisha MW ngapi vile?
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  530 kama sikosei. Unaweza kupitia tovuti ya Tanesco kupata uhakika zaidi.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Umeme wa maji ni very cheap na ndio mtanzania wa kawaida anaweza kuafford, umeme wa mafuta is very expensive na athari zake tunaziona kwa kupanda kwa gharama ya bei ya umeme nchini.

  Faiza foxy acha kumislead watu besti kwani mtera ilijengwa kama dam ya kusaidia Kidatu na haikujengwa kama dam inayojitegemea na hivyo basi mipango mibovu ndio ilichangia kupungua kwa kina cha maji Mtera na Kidatu. Vilevile maji kama yamepungua mbona mto Ruaha na Rufiji maji yamefurika???? Wanashindwa nini kwenda kujenga Stiegler gorge kule????

  Umeme wa upepo, jua hautakuwa mwingi zaidi ya MW100 wakati mahitaji ya umeme nchini yanakuwa zaidi ya 100 MW kila mwaka kwanini wasiende kujenga Stiegler gorge inayoweza kuzalisha umeme wa 2100 MW au River Malagarasi inayokisiwa kuzalisha umeme usiopungua 500 MW au Mto Ruvuma. Mnaleta umeme wa transformer wa MW 10, 20 wakati vyanzo vya maji sehemu nyengine vipo?? Mmeishiwa mawazo na ufisadi ndio umetufikisha hapa tulipo na sio mvua facts za hali ya hewa zinawakatalia na ndio maana Tanesco wanasita kukubaliana nanyi.
   
 12. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mkakati wa muda mfupi ni kutuma wajumbe Thailand, ili watuletee wale wataalamu wa kutengeneza mvua kwa ajili ya Mtera!
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huyu Badra haoni anamuumbua bosi wake ivi ivi!
  Wachukue ela za stimulus package wakanunue mafuta maana ata hatujui zimeenda wapi izo 1.7trillion
   
 14. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sikutaka ku-comment lakini kwa hizi pumba unazoongea hapa inabidi nikuambie. Wewe unawaambia wenzako wana "ufaham finyu". Mimi naona wewe ndiyo hasa mwenye "ufaham finyu" kwa sababu wakati wenzako wanahoji nchi hii kuwa katika hali hii ya giza baada ya miaka takriban 50 ya uhuru, kwamba watawala wameshindwa kubuni njia mbadala ya kupata umeme kuliko kungojea kudra ya mvua kutoka kwa mwenyezi Mungu, rasilimali za nchi kuchukuliwa na wageni wakati wenye nchi wakitaabika, watawala kuacha kutumia fedha kununulia mitambo ya kuzalisha umeme badala yake wanahongana wewe mwenzetu umeshikilia ugamba wako na kuongelea mtera, mtera, fedha za kununulia mitambo, gas??!!! hivi wewe kama hela hakuna hizo wanazohongana sio hela?? Umeambiwa gas lenyewe mgogoro visima wameshavichakachua, juzi wanaingiza mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gas. Huoni kwamba wewe na hao magamba wenzao ndiyo mataahira kabisa ninyi??????????????Shame on you magamba
   
 15. W

  Wisson Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli huu ukosefu wa umeme ni tatizo kubwa sana na linamuathiri kila Mtanzania kasoro labda viongozi wa serikali hii. Last week nilikuwa naanzisha project ya kujenga kanyumba changu nikaenda kununua matofali nikaambiwa ni za kuorder na kusubiria sabababu mitambo ya kutengeneza matofali inatumia umeme na umeme hamna na hivyo hata bei ya tofali imepanda sababu yako machache. Hakuna wa kulaumiwa zaidi ya viongozi wa serikali sababu toka walipoanza kutuingiza kwenye mikataba mibovu wakianza na ITPL mpaka Richmond tatizo halijaisha.

  Huwezi kusema tatizo ni ukame wakati toka mwaka 1992 serikali ilipoingia mkataba na IPTL tatizo hilo lilikuwa linajulikana. Na swala hapa sio ukame sababu tuna mito kibao na kwa hasara tunayoendelea kuipata kutoka IPTL na mikataba mingine ya kifisadi tungeweza kuanzisha chanzo kingine cha umeme wa maji kwenye vyanzo vingine vya uhakika zaidi kama huko Stiglers gorge, Malagarasi nk. Wakati fulani Daniel Yona akiwa waziri wa nishati na madini alisema eti mkataba wa IPTL ni sawa na wewe uwe na harusi, ualike kampuni ya kukupikia uwaambie waandae chakula cha watu 200 alafu wakaja watu 20, kwahiyo hauna ujanja zaidi ya kulipa gharama ya watu 200 ata kama wamekula watu 20. Nikasema kwa hali ya kawaida kwenye harusi zetu watu huzidi labda kama Yona alimaanisha harusi za ulaya au za mafisadi wanaoishi kama wako ulaya kwenye hili giza la umeme. unaweza kuona ni jinsi gani hatuko makini katika kushughulikia umeme mpaka tunaingia mikataba ambayo tunakuwa tunapata hasara kila kukicha.

  Mkurugenzi wa TANESCO aliyepita Dr. Idrissa alisema nchi itaingia gizani kama mitambo ya kuzalisha umeme haitapatikana haraka hiyo ilikuwa mwaka 2008 kama sijakosea. Wanasiasa akiwemo raisi Kikwete wakasema watahakikisha hali hiyo haitatokea, leo imetokea. Ingekuwa nchi zingine kama Japan asinge subiri kuambiwa ajiuzulu, yeye angekuwa ashajiuzulu. Nawashangaa sana wanaomtaka Ngeleja ajiuzulu wakati tatizo kama alivyosema mwenyewe baada ya bajeti yake kugonga ukuta kwamba hili ni swala la serikali nzima. Kikwete anatoa 1.7 trillion kwa ajili ya 'wafanyabiashara' wachache eti wasiathirike na anguko la uchumi!! Tunaoathirika na ukosefu wa umeme anatuambia tatizo ni ukame!! Kwanini tusiamini kwamba hizo 1.7 trillion zimeliwa na Mafisadi anaowakumbatia??? Anahitaji mbinu gani za kitaalamu zaidi ya Mkurugenzi wa TANESCO aliyekuwa anawakilisha wataalamu wa fani husika??!!!

  Napendekeza
  tuanze kuanzisha Hydro-elecric power plant zingine sababu kwa kweli ndo umeme raisi tutakaoweza kuumudu. Huu ndo uwe mpango wa mda mrefu ukijumuishwa na makaa ya mawe. Sisi (TANESCO) tusiingie mkataba na kampuni yoyote ili kuzalisha umeme sababu tatizo litaendelea kuongezeka. taratibu tuanze kuifuta iliyopo. Kwa sasa kanuni za manunuzi zivunjwe ili TANESCO wakiwezeshwa na serikali wanunue mitambo hata kama ni ya mtumba (mbona tunavaa mitumba na tunang'aa) haraka ili izalishe umeme kututoa gizani na kunusuru maisha yetu kiuchumi na kijamii. Umeme iwe huduma muhimu ya serikali kwa watu wake na maendeleo yao na sio suala la watu kufanya biashara sababu hatuna wafanyabiashara wa ngazi ya kuzalisha umeme ambao hawatakuwa mafisadi au mawakala wa mafisadi na watatuongezea tu matatizo juu ya tatizo tulilonalo.

  Kwa kweli hili ni tatizo kubwa sana. Tunahitaji umeme sio mipango na kutaja tumeongeza megawati kadhaa. Acheni Ujuha nyie wenye madaraka ya kuongoza nchi hii.

  Naomba kuwasilisha haswa haswa kwa Raisi Kikwete na wenzake waliopo Seriakalini. MUNGU atulinde na atuongoze tutatue tatizo hili, Amen.
   
Loading...