Tatizo la Umeme: Ujerumani yaisaidia Tanzania Sh bilioni 357 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la Umeme: Ujerumani yaisaidia Tanzania Sh bilioni 357

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Oct 5, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  Na Elizabeth Mjatta | Mtanzania | Ijumaa, Octoba 05, 2012

  SERIKALI ya Ujerumani imetoa msaada wa Sh bilioni 357 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutatua tatizo la umeme nchini.

  Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam jana kati ya Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na Balozi wa Ujerumani nchini, Klaus-Peter Brandes.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo Brandes alisema serikali yake imekuwa ikiisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali yakiwamo ya maji, afya na elimu.

  “Tanzania ni moja ya nchi zinazonufaika na misaada kutoka kwetu lakini kwa mwaka huu kwa mara ya kwanza tunaingia katika kuunga mkono sekta ya umeme na lengo letu likiwa ni kumaliza tatizo lililopo.

  “Tumetoa kiasi cha Euro milioni 26 ambazo zitasaidia kuongeza nguvu katika suala la umeme hususan katika umeme wa gesi ili kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania,” alisema.

  Alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Serikali yake imeisaidia Tanzania Euro milioni 147 ambapo mwaka huu msaada umeongezeka na kufikia Euro 176 ambazo ni sawa na Sh bilioni 352.

  Akitoa nchanganuo alisema Euro milioni 18 zitakwenda kusaidia bajeti, maji Euro milioni 45, afya Euro milioni 42.5, umeme Euro milioni 26 na mazingira Euro milioni 31.5.

  Alisema Euro 6.5 milioni ambazo zimeelekezwa katika kusaidia serikali za mitaa na euro milioni 1 itasaidia katika masuala ya mafunzo.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa alisema msaada huo unazidi kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili na kusema kuwa watahakikisha msaada huo unasimamiwa ipasavyo.

  “Ndugu zetu hawa wamekuwa wakitusaidia kwa awamu, wametusaidia katika miaka mitatu iliyopita na sasa leo tumesaini makubalino ya kutusaidia katika miaka mitatu mingine,” alisema Dk. Mgimwa.
   
 2. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wamkabidhi Prof. Muhongo hayo mabilioni achape kazi. Tuna imani naye katika utendaji wake na tunaamini tatizo la umeme litakuwa historia kama hawatamuwekea mizengwe.
   
 3. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,251
  Trophy Points: 280
  imeshaliwa yote hiyo hela. Kuna watu wameshaipangia mahitaji yao.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kiasi gani wataingiza kwenye 'utafiti, posho, warsha na kongamano' hawa wenzetu wanamagamba huko wizarani badala ya ku-invest fedha zote moja kwa moja kwenye kukamilisha miradi mipya ya kupatikana kwa umeme mwingi zaidi??????

  Hakika tukiwezakuingiza kwenye gridi ya taifa umeme mwingi zaidi kwa mtaji wa msaada tulioupata, ninayo imani ya kwamba ongezeko hilo umeme utakaochangia sana tu bei ya gharama ya kununuliwa kwa kila unit kushuka, gharama ya uzalishaji nayo kushuka katika sekta za uzalishaji nchini kisha uwekezaji kupanuka zaidi na ajira kuwa za kumwaga kwa vijana na taifa kuwa salama zaidi kwa udokozi kushuka mitaani na mwisho jeshi la polisi kuhamishia nguvu zao maeneo mengine mmbadala kuleta tija zaidi kwa kila kodi inayotumika kuwalipa.

  Mkuu Masale, fedha hizi basi kwa mara ya kwanza ziende kwenye malengo ya msingi bila kupigwa konzi na walafi njiani na mwisho wa siku watu tukaanza kuonana wabaya hapa. This is a serious and necessary financial intervention by German friendly donor (s) that MUST JUST go the right way and its MULTIPLIER EFFECTS GET TO TRICKLE DOWN immediately to lowering costs of living in our country, if used properly, since a lowered cost of production would certainly translate into more affordable goods and services being released into the markets.

  Hakika kwa haya ma-bilioni ya Ujerumani, kuja kusikia bla bla bla nyingi za hapa na pale iwe ni mwiko.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa Prof Muhongo na Masele mnayaona maneno haya hapa chini na jinsi gani maoni yetu sisi wananchi mnaopaswa kutuhudumia yalivyopindishwa na utendaji wa MAZOEA NA BLA BLA BLA NYINGI HUKO SERIKALINI (UVIVU MBELE KAZI MWIKO LAKINI UFISADI KAMA ROSARI KWA KWENDA MBELE) tunaoshuhudia toka huko kila kukicha?????

   
 6. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,626
  Trophy Points: 280
  wakawalipe dowans sasa. mia
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Duh! Nikilinganisha Tanzabia na Nchi za jirani..Kenya kwa mfano, tuna hivi/haya

  1. Maziwa, mabwawa,maporomoko.
  2. Vyura wa Kihansi.
  3. Makaa ya mawe.
  4. Nguvu/nishati za asili Jua,Upepo.
  5. Gesi

  Na mengine mengi, lakini bado asilimia 14 (14%) ya wananchi ndio wenye umeme!! Na huu umeme walionao bado si wa uhakika(Wenye kuwa na mgawo takribani kila mwaka)! Bado hata kama tukipewa pesa kiasi gani, bado tatizo litaendelea kubaki pale pale.

  Tujiulize katika nchi za Afrika Mashariki, mbona nchi nyingine hawana mgawo kiasi hiki, wenye kuwa na vyanzo vichache vya uzalishaji wa umeme wao, na nchi nyingine zikigawa umeme kwa nchi nyingine(mfano Kenya ifanyavyo kwa Uganda)...wao wanatumia nini? Mbona ni Hydropower(umeme wa nguvu ya maji) hiyo hiyo na wakiwa na vyanzo vichache?!!
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KWA MTAJI WA FEDHA HIZI JAPO SI KITU SANA, LAITI NINGALIKUA NI WAZIRI WA NISHATI NA MADINI NCHINI ...

  Kwa kweli kwa fedha hizi, japo bado hazitoshi kitu, laiti ningalikua waziri katika wizara ya nishati na madini ningalifanyia kazi fedha hizi kwa ubunifu na uadilifu wa hali ya juu kwa kutekeleza walau yafuatayo:

  1. Kuita technical bench ya wizara yangu na wizara nyinginezo muhimu ili kupanga mkakati murua kufikia lengo la kuongeza umeme mwingi zaidi kwenye gridi ya taifa bila kuleta siasa, uvivu na majungu kazini lakini bila kulipana posho kitu hapa,

  2. Nitaunda vikosi kazi (kwa gharama ile ile ya mishahara wao serikali) na kuyapa malengo na majukumu ya kutekeleza, katika hatua mbali mbali za kuelekea upatikanaji wa lile lengo kuu hapo juu, ndani ya vipindi maalum bila kuingiza Kiswahili kingi na kufuatilia mwenyewe utendaji wao bila kusubiri mi-ripoti kwenye viyoyozi ma-ofisini;

  3. Nitamtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani kunipa nguvu kazi ya wafungwa kibao kote nchini kwenda kuchangia taifa lao kwa kufanya kazi zote zisizohitaji utaalam maalum katika kupatikana ongezeko zaidi ya umeme kwenye gridi ya taifa lakini kwa gharama sifuri kwa upande wa nguvu kazi hiyo;

  4. Nitamsihi Waziri wa Ulinzi na JKT kunipa vijana kibao wenye taaluma mbali mbali huko jeshini kama vile Engineers, Technicians, Surveyors, Managers, Accountants na wengine kibao kujiunga na timu yangu ya wizarani KWENDA ADUI HUYU UMASIKI unaotowesha ajira kwa vijana nchini, kwa kutumia taaluma zao hizo na zile nidhamu za kijeshi KUHAKIKISHA YA KWAMBA ubora wa kazi viwango vya juu sana unapatikana lakini kwa gharama nafuu zaidi, muda sahihi zaidi na UFISADI NA UFUJAJI sifuri mwisho wa siku;

  5. Nitahakikisha kwamba kazi hii nitaifanya kwa uchungu na umakini mkubwa sawa tu na jinsi ambavyo ningalikua nikipenda nifanye kwa kazi au biashara binafsi BILA KUPITISHA LAAWAMA KWA WENGINE na kunyosheana vidole ki-majungu vile.

  Hakika nitafanya kazi hiyo mara kumi zaidi ya Mhe Lowassa enzi zake zile au zaidi ya Dr Maghufuli lakini bila kujigeuza KUKU WA MAYAI ANAYETAGA MAYAI MENGI SANA NA KUGEUKA KUYANYWA kwa zaidi ya asilimia 80 hata kabla ya kukabidhi kazi kwa wananchi walipakodi wa nchi hii.

  Profesa Muhongo na Dr Masele, hebu tuonyesheni ya kwamba nyinyi hapo ni wa tofauti na walau mkapata kumuumbua yule SHETANI WA UVIVU, MAJUNGU na UFISADI KAMA ROSARI kwenye hii serikali ya Magamba ambapo procristination ni jambo la kawaida, ripoti za kubuniwa chini ya mwembe kama kazi, na vikonzi kwenye fedha za misaada na kodi kwenda kwenye fuko la 'SAIDI CCM ISHINDE UCHAGUZI' iko mbeeeeele kama tai kwao.
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  zitaishia mfukoni mwa wenye meno tu hizo
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Siku tutakapokoma hii tabia ya 'MKULIMA KULA MBEGU YOTE NA KUAMUA KUUZA JEMBE KISHA KUAMUA KUHAMIA JUMLA KWENYE MISAADA KILA UCHAO' ndipo tutakapoanza nini maana ya maendeleo kwa faida ya wananchi na hatimae ulipaji kodi nayo kutanuka zaidi na zaidi nchini.

   
 11. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [​IMG] Watanzania wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaa! (Generali Ulimwengu 2011).
  [​IMG]
   
 12. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [​IMG] Watanzania wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaa! (Generali Ulimwengu 2011). [​IMG]
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  tunaendelea kusaidiwa tu,,,,,,,dah
  wajeruman wanataka tuwe na umeme wa uhakika ili wale rasilimali zetu uzuri
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  namba 1,2 na 4 zipo maalum kwa kuuwezesha mchakato uwe wa KULA PESA,,,,UZITEGEMEE JIPYA
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Code:
  
  
  Akitoa nchanganuo alisema Euro milioni 18 zitakwenda kusaidia bajeti, maji Euro milioni 45, afya Euro milioni 42.5, umeme Euro milioni 26 na mazingira Euro milioni 31.5.
  Code:
  
  
  Unaweza badili heading yako ni maji umeme na mazingira etc
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tusubiri tuone maana mvinyo ulele kasha jipya! sitegemei mabadriko yoyote aidi ya kuishia kwenye warsha, semina, mpango mkakati na vitu kama hivyo
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mungu wangu weeeeeeeeeeeeeee masikini wenzetu hawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

   
Loading...