Tatizo la umeme tanzania na mtindo wa kukodisha mitambo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la umeme tanzania na mtindo wa kukodisha mitambo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HISIA KALI, Feb 21, 2011.

 1. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la umeme Tanzania limekuwa ni donda ndugu tangu wanatanzania wajue kuwa kuna kitu kinaitwa umeme. Viongozi wengi wamekuja na kupita lakini tatizo la umeme bado lipo na linazidi kuongozeka kila siku. Tanzania sasa ina watu wanaofikiriwa kufikia zaidi ya milioni 45 lakini uwezo wa Taifa kuzalisha umeme umekuwa haukuwi kuendana na idadi ya watu na shughuli za kiuchumi na kijamii ambazo zinahitaji nishati ya umeme. Katika dunia ya leo nishati ya umeme ni kitu muhimu kwani shughuli nyingi zinategemea nishati hiyo. Taifa lisilo kuwa na uhakika wa nishati ya kutosha haliwezi kuendelea hata kidogo. Hakuna mtu mwenye akili zake atakaye kuja kuwekeza katika nchi ambao nishati sio ya uhakika, na kama atatokea basi gharama za uendeshaji zitakuwa ni kubwa sana hivyo kushindwa kushindana na wazalishaji wengine waliowekeza kwenye nchi zenye umeme wa uhakika. Tukumbuke hata kama umeme utakuwa unauzwa kwa bei ya juu kidogo lakini kama unapatika muda wote hakutakuwa na tatizo kubwa kwa wazalishaji wa bidhaa. Kwani watazalisha zaidi hivyo kufidia gharama zao kwa njia ya kufanya biashara kubwa zaidi. Faida za umeme wa uhakika ni nyingi sana, kwa hiyo si kitu kipya kujadili hapa.

  Kwa ufupi kujua kwamba kuna tatizo la umeme Tanzania sio kitu kipya na hivyo kujadili tatizo lipo kwa kiwango gani ni kupoteza muda bure. Kitu cha kujadili kwa sasa ni ufumbuzi wa tatizo lenyewe.

  Hivi karibuni Tanesco imetangaza mgawo wa umeme. Wanasiasa mbali mbali wamejitokeza na hoja mbalimbali, kwa mfano wengine walitaka kupeleka hoja binafsi bungeni ili kupata maelezo kutoka kwa serikali, wengine wameandika barua kutaka maelezo hayo hayo. Kamati ya bunge inayoshughulia umeme pamoja na mambo mengine ilikwenda kutembea bwawa la Mtera, ingawa sijui walikwenda kuona nini kimpya kule. Waziri anayehusika na umeme ametoa hotuba bungeni yenye kuonyesha mipango ya sekta ya umeme nchini. Hotuba ile ilijaa miradi mingi tu ya kusambaza umeme sehemu mbalimbali za nchi. Lakini sikuelewa ni umeme upi utasambazwa nchini wakati hakuna umeme wa kutosha, kwani hata kule ambako miundo mbinu ya umeme imefika nishati ya umeme inapatikana kwa shida ua hakuna kabisa. Kimsingi umeme wa Tanesco umekuwa sio kitu cha kutegemewa na watumiaji wake kwani leo upo lakini kesho haupo. Katika hali kama hiyo hakuna mtu atakaye weza kufanya mipango ya maana ya kichumi inayohitaji umeme.

  Katika miaka ya mwanzo Serikali ya Tanzania na shirika la Tanesco zilijitahidi kuanzisha vituo mbalimbali vya kuzalisha umeme. Kituo cha mwisho kikubwa kujengwa kama sijakosea ni bwawa la Kihansi. Baadaya ya hapo tumekuwa tukisikia zaidi miradi kwenye hotuba za kisiasa bila kuona utendaji wa kuridhisha.

  Katika miaka ya hivi karibu tumeshuhudia Serikali na Tanesco zimekuwa zikija tu na mikakati ya umeme pale tu mabwawa ya kuzalisha umeme yanaposhindwa kufanya hivyo kutokana na ukame. Labda wanayo mipango kwenye makaratasi muda wote. Mabwawa ya umeme yamekuwa ni chanzo kikubwa cha umeme nchi kwa muda mrefu sasa. Lakini swali la kujiuliza hapa ni je kwa wakati wa sasa ni busara kutegemea mabwawa ambao hayawezi kuzalisha umeme wakati wote wa mwaka? Mvua ikikosekana tu tatizo linaanza. Tunajua kabisa hali ya mazingira imebadilika kwa hiyo kutegemea mvua kwa miaka hii ya sasa si kitu cha busara kwani mvua zi nyingi kama miaka ya zamani, na hili halina ubishi.

  Kuna haja sasa kubuni njia mbadala za kuzalisha umeme tena kwa bei nafuu. Hili nalo sio wazo jipya kwani naamini kuna mipango mingi tu ya kufanya hivyo. Tatizo hapa naamini ni utekelezaji wake.

  Kichwa cha maada kina neno kukodisha mitambo. Hiki ndicho kitu kimenifanya kuandika leo. Kuna maswali hapa ya kujiuliza; Hivi ni kwa nini serikali inaona njia ya kutatoa tatizo la umeme ni kukodisha mitambo? Hivi kwa nini serikali ikodishe na sio kumiliki mitambo?

  Mimi kwa ufahamu wangu ninajua kwamba katika biashara kuna vitu viwili. Kumiliki au kukodisha. Ili kuchagua kimojawapo lazima kuwe na sababu. Sababu kubwa hapa ni tofauti ya gharama kati ya kumiliki na kukodisha. Sababu ya pili ni muda wa hitajio la hiyo mitambo, yaaani ni muda gani hiyo mitambo itahitajika.
  Kwa sababu hizi mbili tu ninashawishika kwamba serikali inatakiwa kumiliki mitambo na wali si kukodisha. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo.
  1) Serikali ina uwezo kwa kununua hiyo mitambo. Pesa zipo serikalini, mipango ifanyike mitambo inunuliwe. Kama serikali haina pesa taslimu inaweze kabisa kukopa katika taasisi za fedha na kununua hiyo mitambo tusije kuogopa riba. Kwanza serikali inakopesheka kirahisi kuliko mtu binafsi kwani kuna uhakika wa kulipa deni zaidi. Serikali inapaswa kujua hata kama itakodisha mitambo lazima italipa tu riba ya benki. Hii ina maana kuwa hata hiyo kampuni ambayo itakodishia serikali mitambo haina hela taslimu, inakwenda kukopa benki. Na ikikopa inaweka hiyo gharama ya riba kwenye malipo ambao serikali itafanya baada ya kukodisha hiyo mitambo. Na si riba tu bali pia gharama ya mitambo pamoja na faida yake zote zinalipwa na mkodeshaji ambaye atakuwa ni serikali. Kwa ufupi kwa kukodisha mitambo serikali inalipa hela nyingi zaidi. Hizi ni gharama za mitambo, gharama za kuendesha mitambo, gharama za ofisi ya kampuni ya mitambo, riba ya benki, na faida ya kumpani yenye mitambo. Kwa maelezo haya mafupi ni dhahiri kuwa kumiliki ni nafuu zaidi ya kukodisha. Hili ni jambo la kawaida katika biashara. Naomba ufanyike uchambuzi yakinifu hapa ili kuangalia unafuu wa gharama uko wapi kati ya kumiliki na kukodisha.

  2) Je tatizo la umeme ni la muda gani? Tatizo la umeme Tanzania sio la muda mfupi ni la muda mrefu. Suala la ama kumiliki au kukodisha mitambo naona linatikiwa pia kutazamwa kwa kuangalia Serikali inatafuta suluhisho la muda mfupi au mrefu. Mimi nadhani suluhisho linatakiwa liwe la muda mrefu. Nasema hivyo kwa sababu tatizo la mgawo limekuwepo miaka mingi, mara kwa mara kila kunapokuwa na ukame tu kunakuwa na mgawo wa umeme hapa Tanzania. Vile hata kama vyanzo vyote vilivyopo sasa vitazalisha umeme, nishati itakuwa haitoshelezi mahitaji kwani havina uwezo huo. Kuna haja ya kuwa na vyanzo vingine vingi zaidi ili kuongeza nishati hiyo, hata kama tukizalisha zaidi ya mahitaji si vibaya kwani tuweza pia kuunza umeme kwa nchi za jirani na kupata fedha za kigeni. Serikali ikinunua mitambo yake yenyewe itaweza kutumia kwa muda mrefu zaidi na bila kuingia gharama za zaida kama ambavy ingekuwa inakodisha. Pia serikali ikumbuke kwa bei za mitambo zinapanda kila siku, bei ya mitambo iliyonunuliwa miaka miwili iliyopita huwezi kuipata leo kwani tayari bei imeshapanda. Hizi gharama zote zitalipwa kama serikali itakodisha mitambo mara kwa mara.

  Kwa leo naona niishie hapa, kwa kushauri serikali iangalie upya suala la ama kumiliki au kukodisha mitambo. Mimi nashauri kununua na kumiliki mitambo ili kupunguza gharama za muda mrefu hata matatizo mengine kama kesi ya Richmond na Dowans.

  Ombi la rasmi.
  Kwa kuwa umeme ni kitu muhimu sana kwenye uchumi wa nchi. Kwa nini serikali yetu isichukuwe hatua za makusudi na kufanya maamuzi magumu ya kuwekeza kwenye hii sekta ili nchi iweze kuzalisha umeme kwa wingi zaidi? Na imani tukiamua hivyo tunaweza. Kuna hela nyingi tu nchi hii zinapotea bure kwenye matumizi ambao hayana maana.
  Nadhani sote tunaona uwanja mpya wa Taifa ulijengwa na serikali ya mzee Mkapa. Hivi kwa nini tusijifunze hapa. Mzee Mkapa alisema potelea mbali lazima nijenge uwanja wa kisasa hapa nchini. Alifanya maamuzi na kutekeleza ndio maana sasa tuna uwanja mzuri wa mpira ambao hata akina Kaka kutoka Brazil walikuja kucheza mpira.

  Viongozi wa serikali ya sasa jamani chukueni maamuzi ya kuwekeza kwenye vyanzo ya umeme. Semeni tu potelea mbali tunataka ifikapo mwaka fulani tatizo la umeme nchini liwe historia. Na fanyeni hivyo kwa kujenga vyanzo vipya ya umeme kwa vitendo. Tumieni hata uranium kuzalisha umeme. Nakuambieni hamtajutia maamuzi hayo hata siku moja na vizazi vijavyo vitawasifu kwa hilo.

  Tunaweza, ila tunatakiwa tu tuwe nia na udhubutu kwa kutenda.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hayo yote uliyoandika tunayajua siku nyingi.........

  Tukimaliza tatizo la umeme hela za ufisadi tutapata wapi? chaguzi ni kila baada ya 5 yrs. tunahitaji hela mkuu za chapchap kwa kupitia shida zenu.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukipatikana ufumbuzi wa kudumu wakubwa watakula wapi! uoni ya kuwa hii ni njia mulua ya kuamka masikini ukalala tajiri; kwani katika masuala ya umeme mtu anaweza akaleta mitambo yake hata kama ni mibovu, akaendelea kuvuna mamilioni ya fedha kila siku. Si kuna capacity charge bwana, mtu analipwa awe amewasha mitambo yake au la.
   
Loading...