Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka
Nchi hio mashughuli huitwa Tanzania.


Tumesikia mara kibao bwawa limekauka maji nakwahio haliwezi kuzalisha umeme unaotosha.

Kuna baadhi ya mito mikubwa Tanzania.

Kama serikali haiwezi kutengeneza mabwawa mengine kutokana na uhaba wa pesa, [Ooops nimesahau pesa za EPA.]

Kwanini serikali isitoe mwito kwa kila mtanzania kwenda kujenga dam kwa mikono?

Watu 33 Mn kwa sensa ya 2002 tushindwe kujenga dam kwa mikono yetu linaloweza kuzalisha umeme wakututosha na pengine wakuuza kwa nchi za jirani?

Mzee hapa una-bore. Haya masuala ya kutazama Ramani yalitumika miaka hile ya zamani wakati tunatafuta identity ya utaifa.

Miaka ya sasa ni lazima tuachane na fantasy na kuangalia reality. Ujenzi wa dam una negative impacts kwa ecosystem.
 
.........................Pili Mo wewe ukiwa kama mbunge wa Singida, na kwa kuwa serikali kwa hivi sasa wamejikita zaidi katika kuwekeza kwenye Miradi midogo midogo ya MW 100 nk
je umefanya nini kushauri wadau binafsi kama wewe, au halmashauri ya Mji wa kauza Shares ilikupata mtaji wa kufungua katanesco kadogo hapo Singida, na mkiona Mtaji unao hitajika ni mkubwa, basi mnaweza omba mitaji toka nje ya Singida, na kutoka kwenye institution zingine kama world bank, na watu wa moja moja hapa Bongo na Nje?
Ili mradi shares ziwe zinauzwa pale DSE

Mkoa wa Tanga kupitia kampuni iitwayo Katani Limited wameweza kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya mmea wa katani. Inachukua mabaki yote ya mmea wa katani, mabaki ya kiwandani etc ili kuzalisha umeme na end product yake inatoa mbolea murua kabisa. Umeme huo, according to one Mr. Shamte unaweza kuzalisha umeme wa kutosha kuelectrify Tanga nzima and Kilimanjaro regions - the problem is wanaambiwa wauingize kwenye grid ya taifa!

Kuna mtu hapo juu kasema maybe microplant ndogondogo ni jawabu lakini problem itakuwa na monopoly ya TANESCO kwani lazima kumuuzi yeye.

BTW, Mo, Shamte told me wana mpango wa kwenda Singida kwani kule kuna masalio ya mashamba ya katani ambayo yamekuwa neglected miaka mingi kwa hiyo lengo ni kwenda kung'oa yale makatani (na kupanda mingine) na kuyatumia kuzalisha umeme. Maybe get in touch with him on that.
 
Mzee hapa una-bore. Haya masuala ya kutazama Ramani yalitumika miaka hile ya zamani wakati tunatafuta identity ya utaifa.

Miaka ya sasa ni lazima tuachane na fantasy na kuangalia reality. Ujenzi wa dam una negative impacts kwa ecosystem.
Mkuu, haiwezekani hii kuwa ni lugha ya biashara maanake hawa wanasayansi wetu wa siku hizi biashara ndio hujenga Uchumi wa nchi zao. China, Canada, Norway, Brazil, Venezuela, ndizo zinaongoza kwa matumizi ya Hydro lakini sijasikia matatizo hayo na wanaendelea ujenzi wa Hydro ktk nchi zao..Na wanatisha kiuchumi na maendeleo..

Kweli nakubali inawezekana sana ujenzi wa Hydro kubwa sana kuelta madhara lakini kwetu sisi na hizi za chini ya MW1000 kweli zinaweza kuwa na madhara hayo! labda nipeni mfano maanake Hydro nyingi zimejengwa miaka zaidfi ya 50 iliyopita, tungesikia...
 
hii article yako yote umeitoa NY times halafu umeitafsiri, sio kitu kibaya lakini unge wa acknoledge. usiposema source watu tunaona ni plagiarism.
link hii hapa
Hatujawekeza ipasavyo kwa miaka 15 hadi 20 katika kitengo cha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hayo maneno yalitamkwa na Lawrence Musaba, Meneja wa Southern African Power pool, muungano na mtandao wa nchi kumi na mbili kusini mwa Sahara.
Ukiitoa nchi ya Afrika Kusini kwenye mambo hayo, nchi zote zilizobaki za kusini mwa jangwa la Sahara lenye watu milioni 700, linapata umeme sawa na wananchi wa Poland ambao ni milioni 38 tu.


http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html
hii ndio article ya kiingereza ambayo umetafsiri kwa kiswahili. maneno haya yafananishe na hapo juu

"We've had no significant capital injection into generation and transmission, from either the private or public sectors, for 15, maybe 20 years," said Lawrence Musaba, the manager of the Southern African Power Pool, a 12-nation consortium of electricity utilities at the continent's tip.

The gravity of this year's shortage is all the more apparent considering how little electricity sub-Saharan Africa has to begin with. Excluding South Africa, whose economy and power consumption dwarf other nations', the region's remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland.


http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html
hii article inanikumbusha uk 2007 nikiwa nimekaa na watu kutoka kenya, uganda, nigeria, ghana, ivory cost na cameroon tukawa tunajidili jinsi waandishi wa habari jinsi wanavyoiandika vibaya africa na effect zake kwenye tourism na kuzuia investment flows. niliposoma hii ya kwako kwa kiswahili nikajua tu utakuwa umeitafsiri, nikatumia kama nusu saa kuitafuta mpaka nikaipata.

mo ukisoma hizi habari au research paper yeyote lazima uingalie kwa makini
na uitafakari. "the region's remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland".
huu ni uongo wa hali ya juu ambao unaandikwa na waandishi wa habari wa nje juu ya africa, kina chosikitisha na wewe ume copy na ku paste na kuja kutulisha hapa JF. huyu mwandishi ni watu ambao wanakuja mara moja tu africa na kuondoka na hawajui hali ya africa na kazi yao ni kuandika negative about africa.

ukiangalia TZ peke yake tukasema dar na mwaza kuna umeme, kwa ajili sio kila mtu ana umeme katika mikoa hii miwili kwa hiyo tuseme mikoa mingine yote ya tz haina umeme (arusha, mbeya, kilimanjaro, tanga na kwingineko kote hamna umeme). watu wa dar + mwanza ni 8mil, kwa hiyo ni watu mil 8 out of 40m wana access to electricity which is 20% of all tanzanians.
nimetembea kenya sehemu mbali mbali, na kenya watu wengi wana umeme zaidi ya tanzania.
jamaa zangu wa nigeria, ghana, ivory cost, cameroon na uganda walinitolea mifano hiyo hiyo na wakanihakikishia kuwa more than 20% of their pop has access to electriicty. ukijumlisha 20% ya inchi zote utaona inapita 38mil by miles.
hata UN estimate ni 12% which is 84mil.

tuachane na data turudi kwenye mada

tatizo kubwa ambalo linaikabili sekta ya umeme africa ni uongozi/corruption. nchi za africa zina viongozi ambao wanafikiria matumbo yao tu na si kutatua matatizo ya watu waliowapigia kura.
mfano ethiopia wanajenga bwawa kubwa sana la umeme (huu ni mpango wa long term) lakini shutuma ndio zile zile kwamba ni hela nyingi imeliwa na hela pia haitoshi.
http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/7937480.stm
tukienda nigeria obasanjo na wenzake wametafuna karibuni $2bn ambazo zilikuwa zitumike kwenye umeme.

tukirudi dar rashid ametuambia tusiponunua mitambo ya rafiki yako dowans tutakaa kwenye giza, hii ni dhairi kabisa watu hawataki kufanya mipango ambayo haifaidishi matumbo yao.

karibu JF
 
Generally,kuna wanasiasa wanaoguswa kwa dhati na matatizo yanayoikabili nchi yetu lakini kinachowakwaza ni unity yao na CCM.Nadhani tunahitaji sana wazalendo wanaoweza kujitoa mhanga kwa manufaa ya nchi,na hiyo ni pamoja na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kuendeleza itikadi za siasa.If you try that,Mheshimiwa Dewji,I'll be the first to shout aloud "MOHAMMED DEWJI FOR PRESIDENT OF TANZANIA


Wacha kumponza mwenzako.

Na akigombea u-president hata kama ni kwa kutumia CCM ataangushwa vibaya.

Mheshimiwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo lake kwani juhudi zake tunaziona. Na najua kwa vyovyote vile atachaguliwa tena kwenye jimbo lake kwa juhudi zake.

Labda ategemee nafasi ya kuteuliwa kuwa waziri fulani kupitia CCM lakini Urais utamponza.

Hii ni kwamba:
Japokuwa Mo ni mtanzania mwenye asili ya Asia na moyo wake ni wa kiafrika lakini mambo kama ya EPA ndiyo yatakayomponza.

Wako wanasiasa ambao wataitumia hio nafasi ya kumshambulia kutokana na watanzania wenzake wenye asili ya Asia walivyofanya Radar, EPA etc
 
Mkuu, haiwezekani hii kuwa ni lugha ya biashara maanake hawa wanasayansi wetu wa siku hizi biashara ndio hujenga Uchumi wa nchi zao. China, Canada, Norway, Brazil, Venezuela, ndizo zinaongoza kwa matumizi ya Hydro lakini sijasikia matatizo hayo na wanaendelea ujenzi wa Hydro ktk nchi zao..Na wanatisha kiuchumi na maendeleo..

Kweli nakubali inawezekana sana ujenzi wa Hydro kubwa sana kuelta madhara lakini kwetu sisi na hizi za chini ya MW1000 kweli zinaweza kuwa na madhara hayo! labda nipeni mfano maanake Hydro nyingi zimejengwa miaka zaidfi ya 50 iliyopita, tungesikia...

Mkuu Mkandara,

Tuambie ni mara ipi mipya ya Hydro inajengwa katika nchi hizo? Three gorges wa China ni disaster. Aswan ni disaster. Sidhani kama Venezuela na Brazil wana miradi mikubwa mipya ya Hydro. Canada sijui. Norway nao sidhani kama wanampango. Lakini hata hivyo ukiangalia mazingira ya Norway ni tofauti na sisi, wao wanamajabali na fjords ambazo waliweza kutumia bila madhara makubwa. Hawana kitu kujaa tope, kwa mfano. Hivi karibuni nadhani ni India ndiyo walikuwa na mradi mkubwa ambao na wenyewe umekumbwa na matatizo.

Amandla......
 
Last edited by a moderator:
Naona nishukuru Makutano Show kwa kufanya hii Link kuweza kuiona... Hii topic iko valid bado to date. Maswala kama haya Mkuu Invisible nashauri kama ingewezekana mngeweka utaratibu wa kumfuatilia mhusika kama mna contact hasa kama ni verified kama mh. Dewji. A great (very valid) discussion but bado inaelea...
 
Mkuu Mkandara,

Tuambie ni mara ipi mipya ya Hydro inajengwa katika nchi hizo? Three gorges wa China ni disaster. Aswan ni disaster. Sidhani kama Venezuela na Brazil wana miradi mikubwa mipya ya Hydro. Canada sijui. Norway nao sidhani kama wanampango. Lakini hata hivyo ukiangalia mazingira ya Norway ni tofauti na sisi, wao wanamajabali na fjords ambazo waliweza kutumia bila madhara makubwa. Hawana kitu kujaa tope, kwa mfano. Hivi karibuni nadhani ni India ndiyo walikuwa na mradi mkubwa ambao na wenyewe umekumbwa na matatizo.

Amandla......
Wee fanya ku- google utaziona kibao...
Wakati mwingine tufikirie sana hizi hypes za West wanapopiga vita kitu hutokana na kwamba wao hawauzi kitu. Matumizi ya mafuta yanatumaliza walati wao wenyewe wanatumia Nuclear, tukitengeneza sisi wanasema tunataka kutengeneza vichwa vya mabomu na hatari. Kuna kitu hatari kama global warming mbona wote wanatetea kwamba hakuna kitu hicho..
 
Back
Top Bottom