Tatizo la umeme nchini linahitaji ufumbuzi wa muda mrefu na sio muda mfupi

Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka
Nchi hio mashughuli huitwa Tanzania.


Tumesikia mara kibao bwawa limekauka maji nakwahio haliwezi kuzalisha umeme unaotosha.

Kuna baadhi ya mito mikubwa Tanzania.

Kama serikali haiwezi kutengeneza mabwawa mengine kutokana na uhaba wa pesa, [Ooops nimesahau pesa za EPA.]

Kwanini serikali isitoe mwito kwa kila mtanzania kwenda kujenga dam kwa mikono?

Watu 33 Mn kwa sensa ya 2002 tushindwe kujenga dam kwa mikono yetu linaloweza kuzalisha umeme wakututosha na pengine wakuuza kwa nchi za jirani?
 
Kama kwa FM unamaanisha Fundi Mchundo umekosea. Mimi sio engineer bali ni technician (Fundi Mchundo).

Majibu kuhusu hii miradi ( ongezea na Aswan Dam la Misri) utayapata kwenye bandiko la August. Big dams are a disaster in the making. Inaelekea utafurahi kusikia hakuna hata tone la maji ya Rufiji linafika Bahari ya Hindi! Are you for real?

Amandla......

Kama Aswan/Three Gorges are a disaster, si lazima kila big dam iwe a disaster. Of course nitafurahi sana kama tutaweza kutumia maji yote mashambani, uvuvi, viwandani, majumbani, nk kuliko tunapoyaacha yaishie baharini na kulialia njaa na umaskini.
 
Kwanza sina budi kukupongeza Mheshimiwa Dewji kwa kujumuika nasi hapa jamvini.Laiti tungekuwa na viongozi wa CCM japo watano tu wenye mtizamo kama wako basi tungeweza kupiga hatua kidogo.Kuna usemi wa busara kwenye stadi za siasa unaosema kwamba wanasiasa mahiri hupendelea mijadala kwenye hadhira yenye potential ya kutoafikiana nao.You truly have shown the way to your fellow wana-CCM but sitrajii kuone the like of Rostam,Lowassa,Sofia Simba,etc kujumuika nasi hapa unless "ramli" ziwajulishe kuwa kuna votes which their money can't buy.

Pamoja na kuafikiana na mtazamo wako lakini nadhani umekwepa kuangalia kikwazo halisi cha kufanikiwa kwa mipango yetu mingi ikiwa pamoja na katika sera ya nishati iliyogeuzwa "shamba la bibi",kila mwenye mbinu ya kuiba anataka kuweka mkono wake hapo.My point is,hakuna mpango wowote wa maendeleo utakaofanikiwa pasipo kudhibiti ufisadi.Tutakuwa wendawazimu kutaraji upatikanaji wa umeme wa uhakika ilahi asilimia kubwa ya waliotukwaza huko nyuma wanaendelea kubaki sehemu muhimu katika uandaaji na utekelezaji wa mipango hiyo.

Hivi Mshehimiwa Dewji,unadhani wakijitokeza wafadhili wa kutoa fedha za kuboresha sekta ya umeme,wezi wa Richmond hawatapenyeza watu wao kuhakikisha wanapiga panga sehemu ya fedha hizo?Kumbuka kwamba Mwenyeketi wako,ambaye ni Rais wetu,Jakaya Kikwete,aliwahi kutuahidi kuwa tatizo la umeme lingekuwa historia.Wapo waliomwamini kwa vile alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambapo sekta ya umeme inaangukia humo.Matokeo yake tukaletewa majambazi wa Richmond.

Mipango ya muda mrefu haiwezi kufanikiwa iwapo watawala wetu wanataka kuishi kama wewe mfanyabishara uliyejijenga kwa muda mrefu.Naomba nieleweke kwamba hapa sikutupii dongo wewe bali namaanisha kuwa maisha ya watawala wetu hayaendani kabisa na hali halisi ya nchi yetu.Ninyi wafanyabiashara mna kila sababu ya kuendesha magari ya thamani kubwa,majumba ya kifahari,samani za bei mbaya,nk kwa vile ni matokeo ya jitihada zenu binafsi (exclunding ndoa ya mafisadi na watawala).Nchi ni kama familia,iwapo baba atataka kuvaa suti za bei mbaya ilhali uwezo wake ni duni basi ni dhahiri masuala kama ada za shule za wanawe au hata mlo hapo nyumbani itakuwa ni tatizo.

Halafu kingine ambacho naweza kukiita kama ushauri kwako ni kwamba mwenzetu uko katika nafasi ya ku-initiate change (of course,kwa kushirikiana na wazalendo wengine).Je hufikirii kwamba mawazo haya mazuri uliyonayo yanaweza kuwa even more productive iwapo utajaribu kuyasambaza kwa baadhi ya wanasiasa wenzio tunaowafahamu kama wanaopenda nchi kwa dhati (or at least that's how they portray themselves)?

I strongly believe kuwa unaguswa kwa dhati na matatizo yanayoikabili nchi yetu japo nafasi uliyonayo kama mbunge wa CCM inakwaza your full potentials.Kadhalika natambua kwamba mazinigra ya baishara katika nchi zenye nunu-demokrasia yanakuwa magumu iwapo mfanyabiashara hataonyesha kuafikiana na kila mtazamo wa chama tawala.Sasa kwa vile CCM imeshajitambulisha kuwa ngome muhimu ya ufisadi,napata shida kuona namna mawazo yako mazuri yatakavyoweza kuzaa matunda yanayokusudiwa.

Generally,kuna wanasiasa wanaoguswa kwa dhati na matatizo yanayoikabili nchi yetu lakini kinachowakwaza ni unity yao na CCM.Nadhani tunahitaji sana wazalendo wanaoweza kujitoa mhanga kwa manufaa ya nchi,na hiyo ni pamoja na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kuendeleza itikadi za siasa.If you try that,Mheshimiwa Dewji,I'll be the first to shout aloud "MOHAMMED DEWJI FOR PRESIDENT OF TANZANIA"
 
Kwanza sina budi kukupongeza Mheshimiwa Dewji kwa kujumuika nasi hapa jamvini.Laiti tungekuwa na viongozi wa CCM japo watano tu wenye mtizamo kama wako basi tungeweza kupiga hatua kidogo.Kuna usemi wa busara kwenye stadi za siasa unaosema kwamba wanasiasa mahiri hupendelea mijadala kwenye hadhira yenye potential ya kutoafikiana nao.You truly have shown the way to your fellow wana-CCM but sitrajii kuone the like of Rostam,Lowassa,Sofia Simba,etc kujumuika nasi hapa unless "ramli" ziwajulishe kuwa kuna votes which their money can't buy.

Angalia tabia ya watanzania kuwalamba miguu wakubwa badala ya kuchangia mada unatoa majipoint yasiyokuwa na msingi Dewji amezungumzia nini kifanyike kuhusu umeme wewe unaanza kampeni tutafika kweli hali hii!!!
 
Angalia tabia ya watanzania kuwalamba miguu wakubwa badala ya kuchangia mada unatoa majipoint yasiyokuwa na msingi Dewji amezungumzia nini kifanyike kuhusu umeme wewe unaanza kampeni tutafika kweli hali hii!!!

Nakubaliana na uchambuzi wako.Unaonaje kama ungenitendea haki kwa wewe kuwa mfano wa kujadili hoja za msingi?

Kabla ya kukurupuka kunikosoa ungesoma posts nzima.Kama umesoma lakini hukunielewa basi kwa kifupi namfahamisha Dewji kuwa mipango ya muda mrefu haiwezi kufanikiwa in midst of ufisadi.What's wrong with that

Kabla ya kunihukumu ungenitendea haki kwa kuangalia posts zangu tangu nilipojiunga na mtandao huu Agosti 2006,au unaweza kumuuliza Invisible who certainly is aware of my political stance.

By the way,katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa haki kwangu kama Mtanzania kutoa uhuru wa mawazo yangu alimradi siutumii uhuru huo kumdhalilisha,kumtukana au kumkwaza mtu mwingine.

Kosa kumsifia Dewji?Kama ni mbunge wa kwanza wa CCM kuja hapa jamvini asipongezwe?Nimemtendea haki kwa kumpongeza kisha nikaweka wazi mtazamo wangu kuwa kikwazo ni ufisadi na lifestyle ya watawala wetu.Hilo la pili hukuliona?

Basi ungefanya la maana zaidi kwa kunikosoa (kwa lugha yoyote unayoona inakufaa) kisha ukachangia mada kwa mtizamo wako.Kufika tutafika lakini mnaotukwaza ni ninyi mnaosubiri flani aseme kisha mrukie kuongeza idadi ya posts kwa lunatic criticisms.
 
Nakubaliana na uchambuzi wako.Unaonaje kama ungenitendea haki kwa wewe kuwa mfano wa kujadili hoja za msingi?

Kabla ya kukurupuka kunikosoa ungesoma posts nzima.Kama umesoma lakini hukunielewa basi kwa kifupi namfahamisha Dewji kuwa mipango ya muda mrefu haiwezi kufanikiwa in midst of ufisadi.What's wrong with that

Kabla ya kunihukumu ungenitendea haki kwa kuangalia posts zangu tangu nilipojiunga na mtandao huu.

By the way,katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa haki kwangu kama Mtanzania kutoa uhuru wa mawazo yangu alimradi siutumii uhuru huo kumdhalilisha,kumtukana au kumkwaza mtu mwingine.

Nisamehe mkuu ikiwa sijakutendea haki but sidhani mantiki kumwambia muheshimwa Mbunge wetu Dewji kuwa utampigia kura for presidency maana uongozi ni wito.

Na kama ungelipendelea awe rais ungelianzisha thread nyengine ndugu yangu ama kuhusu points zengine naweza kukubaliana na wewe somehow ila hili la urais no!!! unless muswada wa kutenganisha biashara na uongozi itakapopitishwa ndio nitakuwa pamoja na wewe
 
Pili tutafute njiambadala wa umeme. Sishauri Dam project kwani nadhani waliopita wameshalitolea tahadhari but nadhani ni ushauri mzuri kama nuclear ni expensive kwanini basi tusiombe mkopo World Bank?? kwavile tanzania tuna reserve kubwa za uranium tutumie hio opportunity kuzalisha umeme wa nguvu za atomic tukawa tunauza nchi nyenginezo given kuna shortage ya umeme barani afrika.

Nakubaliana na wewe kuhusiana na suala la nuclear.Lakini tatizo kubwa katika nchi zetu za Afrika ni kuwa tuna walamba sana miguu hawa ma giant petroleum lobbyist.

Nchi za jumuia ya Afrika Mashariki wana uwezo kwa pamoja kujenga nuclear plant. Lakini ni Kagame tu ambaye anaonekana mwenye mwanga haya mengine sijui.
 
Nisamehe mkuu ikiwa sijakutendea haki but sidhani mantiki kumwambia muheshimwa Mbunge wetu Dewji kuwa utampigia kura for presidency maana uongozi ni wito.

Na kama ungelipendelea awe rais ungelianzisha thread nyengine ndugu yangu ama kuhusu points zengine naweza kukubaliana na wewe somehow ila hili la urais no!!! unless muswada wa kutenganisha biashara na uongozi itakapopitishwa ndio nitakuwa pamoja na wewe

Haina neno Mkuu,

Kuhusu Dewji na urais,naelewa wazo hilo linaweza kuonekana la kipuuzi kupita mfano lakini let's be honest.Jinsi huyu jamaa anavyolitumikia jimbo lake kwa mafanikio si mara 20 bora kuliko huyu world traveller JK anavyobomoa nchi?I understand kwamba ubunge sio SI UNit ya urais lakini I'm kinda impressed by Dewji,and that from mie ambaye kwa muda mrefu nimekuwa siridhishwi na mwenendo wa watanzania wenye asili ya kiasia.Labda siko sahihi lakini something useful is better than nothing.

Hilo la kutenganisha biashara na uongozi halitekelezeki kwa vile haihitaji ujuzi mkubwa wa sheria kutambua kuwa linapingika mahakamani.By the way,tatizo si biashara bali ufisadi.Still,kutenganisha biashara na siasa kwa mtindo wa sheria hakutakuwa tofauti na kupiga marufuku takrima ambapo tunaendelea kushuhudia hata chaguzi za madiwani zikitawaliwa na takrima (a polite word for rushwa).Siku zote tatizo halijakuwa kwenye sheria kwani zipo tangu tupate uhuru.Kikwazo ni ukweli kwamba tuliwakabidhi jukumu la kusimamia sheria hizo ndio vinara wa uvunjaji sheria.Na si wasimamizi wa sheria pekee waliobobea kwenye uvunjaji wa sheria bali hata watunga sheria wenyewe wamo kwenye mtindo huo (refer sakata la posho mbilimbili za wabunge).
 
Mdondoaji et-all
Sishauri miradi midogo midogo ya umeme vijijini pekee ndiyo jawabu la hasha. Kwa kifupi mapendekezo yangu ni haya:

1) Tuwekeze kwenye micro hydro projects kwa ajili ya vijiji na miji midogo.

2)Tuangalie uwezekano wa kutoa umeme karibu na watumiapo kwa kuangalia resources ziliopo. K.m. miji kama Singida inaweza kuwekeza kwenye kuvuna umeme kutoka upepo na jua; miji ya Kigoma kutoka jua, maporomoko madogo, taka taka; Arusha kutokana na taka taka, chem chemi za moto n.k.

3)Tuboroshe efficiency ya distribution na kuhakikisha tuna-minimize upotevu wa umeme kutoka unapozalishwa hadi unapotumika.

4) Wenye viwanda vikubwa wawe encouraged (kwa unafuu wa kodi etc.) kuzalisha umeme hapo walipo kutokana na process yao ya uzalishaji. Kwa mfano, baggase ambayo inatokana na uzalishaji wa sukari ni source nzuri sana ya umeme. Viwanda vingi vina uwezo wa kutumia joto linalotokana na uzalishaji wao kutoa umeme.

5) Tu-encourage matumizi ya vyombo vinavyotumia umeme kidogo. Hivi karibuni California wametangaza kuwa watapiga marufuku luninga zinazotumia umeme kwa wingi. Na sisi hiyo hivyo. Tupunguze kwa mfano gharama ya balbu bora na tupige marufuku incandescent bulbs, n.k.

6) Tuwape motisha watu wazalishe umeme katika majumba, maofisi na sehemu wanazofanyia biashara. Jua, upepo na biogas vinatosha kabisa kutoa nishati kwa ajili ya matumizi yetu ya kawaida. K.m. mashule, mahakama yote yawekewe solar panel kuzalisha umeme kwa matumizi yake ya kila siku. Sehemu hizi mara nyingi zinatumika mchana na mahitaji yao ni kwa ajili ya kuwasha taa, kuendesha kompyuta, maabara n.k.

7) Tuanze kutoa viwango na kutoa nishani kwa majengo yanayotumia umeme kidogo. Marekani wana kitu kinaitwa LEED. Ni upuuzi kulazimika kuwasha taa mchana au kutumia kiyoyozi katika maeneo mengi ya nchi yetu. Ubunifu kidogo utaondoa ulazima huu.
Tufanye mipango kabambe ya kuzalisha umeme kutokana na gesi kibao tuliyo nayo. Hii source ni efficient na safi.

Mengine mtaweza kuongezea nyie wasomi.

Ninachosema ni kuwa badala ya kukimbilia miradi mikubwa tuangalie uwezekano wa kutumia resources tulizo nazo vyema zaidi. Miradi kama hiyo ya big dam na nyuklia itatusumbua kuanzia kuitekeleza hadi kuiendesha. Itatupa bragging rights za muda mfupi na kutuumiza vichwa baadae.

Amandla......
 
Fundi Mchundo,

Mkuu ushauri mzuri sana lakini swali langu lipo pale pale..Ikiwa tumeshindwa kutunza tulivyokuwa navyo ambayo sii ghali kuvifanyia ukatabati itawezekana kujenga vyanzo vipya wakati tumeshindwa kurekebisha Mapungufu yetu?.

Nitakukumbusha tena. Mashirika ya Umma na viwanda yalibinafsishwa wakati mapungufu yalikuwa ktk Uongozi.. Sasa ikiwa tumeona mashirka yakibinafsishwa (yasiyokuwa na mapungufu) na kuwaacha Viongozi wenye mapungufu wakiendelea kuongoza wizara, mashirka, taasisi na kadhalika hata baada ya wao ku fail kiutendaji walipokuwa viongozi wa mashirika yaliyotaifishwa. Kweli tunaweza kuanzisha miradi mipya chini ya mfumo ule ule wa viongozi wabovu?..
 
Last edited by a moderator:
Fundi Mchundo,
Mkuu ushauri mzuri sana lakini swali langu lipo pale pale..Ikiwa tumeshindwa kutunza tulivyokuwa navyo ambayo sii ghali kuvifanyia ukatabati itawezekana kujenga vyanzo vipya wakati tumeshindwa kurekebisha Mapungufu yetu?.

Nitakukumbusha tena. Mashirika ya Umma na viwanda yalibinafsishwa wakati mapungufu yalikuwa ktk Uongozi.. Sasa ikiwa tumeona mashirka yakibinafsishwa (yasiyokuwa na mapungufu) na kuwaacha Viongozi wenye mapungufu wakiendelea kuongoza wizara, mashirka, taasisi na kadhalika hata baada ya wao ku fail kiutendaji walipokuwa viongozi wa mashirika yaliyotaifishwa. Kweli tunaweza kuanzisha miradi mipya chini ya mfumo ule ule wa viongozi wabovu?..

Nakubaliana nawe. Sehemu kubwa ya matatizo yetu ya umeme yanatokana na hali mbaya ya vyanzo vyetu. Mabwawa kujaa tope, turbines kuharibika, n.k. Ndiyo maana miradi mikubwa kama ya Stiegler Gorge naipinga. Tuwekeze kwenye miradi ambayo tuna uwezo nayo. Na kwa kuwa na vyanzo vingi vya umeme vitatupunguzia adha ya kukosa umeme chanzo kimoja kikiwa na matatizo. Ili kufanikisha hili, Tanesco itakiwe kunua umeme wa ziada kutoka kwa kila mzalishaji pale inapowezekana. Katika baadhi ya nchi za ulaya mtu binafsi unaweza kuuza umeme wa ziada kwa kampuni yenye mamlaka ya kusambaza umeme sehemu unayoishi. Viwanda kama vya MPM viruhusiwe kuuzia umeme miji ya karibu na vile kwa viwanda vya sukari, simenti n.k.

Yote haya yafanyike pamoja na kuhakikisha kuwa viongozi wanaopewa dhamana ya nishati wanastahili dhamana hiyo. Na kwa vile wazalishaji watakuwa wengi, athari ya uongozi mbovu sehemu moja itapungua kwa kiasi kikubwa.

Amandla.....
 
kwa nini afrika tu? They are still with us. Kumbuka wale jamaa waliotaka kuhujumu mitambo ya msumbiji akiwemo mjerumani nadhani ili wapate dili la biashara za majenereta. Wafanyabiashara nanyi mmo kwa kutengeneza matatizo!! Hata tatizo letu ni artficial, kuna watu wanafanya biashara zao, na ndivyo zilivyo nchi nyingine za afrika.

tunajitafuna wenyewe
 
Kuwa na nishati ya umeme endelevu lazima ianzie kwenye SERA makini ya Nishati.

Mo na Wabunge wenzako acheni ushabiki, upambe, kutukuelewaa mambo kwa mapana na kwa kiasi fulani upeo finyu wa mambo, mshawishi kuwepo kwa sera bora ya upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.

Hatuwezi kusongoa katika upatikanaji wa nishati nchini kwa muundo wa sasa wa Tanesco. Serikali ikihamasishwa na bunge iletee sera ya kufumbua tatizoo hiliii..
 
Na ndio maana na mimi nasisitizia wadau wakila sehemu. iwe wabunge, wafanya baishara, halmashauri etc etc wajikite katika kuhamasishana katika kutatua tatizo la umeme sehemu zao, kwa hii ndio itaongeza vipato na kuchochea maendeleo sehemu zao. na pia kuongeza ushindani wa kibiashara na hata kukuza soko letu la mitaji.

Nakubaliana na wewe!
Tunakimbilia miradi mikubwa mikubwa ya umeme wakati hatuwezi hata kutengeneza vyanzo vidogo vidogo vinavyotuzunguka. Inashangaza kwamba halmashauri nyingi za wilaya hazina umeme ilhali zimezungukwa na mito kibao. Kuna mushkeli katika sera zetu za maendeleo.

Kama Aswan/Three Gorges are a disaster, si lazima kila big dam iwe a disaster. Of course nitafurahi sana kama tutaweza kutumia maji yote mashambani, uvuvi, viwandani, majumbani, nk kuliko tunapoyaacha yaishie baharini na kulialia njaa na umaskini.

Kabisa.
Wamisri wanatucheka kila leo kwamba tunayaacha maji yatiririke hadi baharini bila kuyatumia huku tukilia njaa na ukosefu wa umeme, ni uendawazimu fulani hivi. Something needs to change in our heads.
Kwa faida ya wasomaji wwa thread hii, kuna jedwali la mpango wa umeme wa taifa kwa miaka kadhaa ijayo. Sasa tuangalie na tujadili ni namna gani utekelezaji wake tuufanikishe kwa rasilimali (ikiwemo watu) tulizonazo.

Tanzania power plan generation Mix (Source: TANESCO, 2005)

Project Name
Possible Commencing Year
Cost (Million US$)
Conversion of Tegeta Diesel Units (no new capacity)
2006
12.3
60 MW Combustion Turbine at a “Green-field”
2007
30.006
60 MW Combined Cycle at a “Green-field”
2009
79.848
Zambia Interconnector 200 MW
2010
168.10
Ruhudji Hydropower Development 358MW
2012
400.63
Mchuchuma Coal fired Plant (200 MW)
2018
201.72
Mchuchuma Coal fired Plant (200 MW)
2023
176.505
Rumakali Hydropower Development (222 MW)
2024
338.161
60 MW Combustion Turbine at a “Green-field”
2027
34.53
60 MW Combustion Turbine at a “Green-field”
2028
30.00

Tuendelee na mjadala

Idimi

 
Hawezi kuepuka responsibility hata umtetee vipi. It was under his watch hali ya sasa ndiyo imetokea. Obama analaumiwa kuhusu kukesekana kwa kazi marekani ingawa wote wanajua matatizo yalianza na George W. Yeye ndiye yuko kwenye madaraka na hawezi kukwepa responsibilty. Ndivyo ilivyo kwa Idriss. Hawezi kuepuka kwa kuwasingizia waliomtangulia au wanasiasa. Yeye angeona yote haya kama ni obstacle basi angeachia ngazi.

Hapana, Mkuu. Dr. Rashidi hafai kuendelea na uongozi wa Tanesco. Awapishe wengine wajaribu. Sababu nyingine ziko hapa http://allafrica.com/stories/200907280404.html



Amandla.....

Red. Ndio maana waTz tunashindwa katika mengi sababu ya kupenda kueka watu wanaojaribu jaribu.

Tukubali kuwa wawekwe watu wenye ujuzi wa kufanya na sio kujaribu.
 
Red. Ndio maana waTz tunashindwa katika mengi sababu ya kupenda kueka watu wanaojaribu jaribu.

Tukubali kuwa wawekwe watu wenye ujuzi wa kufanya na sio kujaribu.

Katika hao unaowasema wanawekwa kujaribu jaribu Dr. Idriss yumo?

Amandla.....
 
Hivi Mo, ukitaka kuendelea unajilinganisha na aliyeshindwa kama Nigeria au au unamwangalia yule aliye fanikiwa kama kichocheo cha maendeleo?

Maana nakumbuka tulipokuwa tunasoma na kuwa na marafiki, wazazi watakutaka uwe na marafiki ambao mtaongozana vizuri, iwe kitabia na kimasomo nk, sasa hapa naona wewe unatushauri tumwangalie Nigeria au Afrika kusini kuhalalisha kushindwa kwetu.

Je, hii ni Sawa?
 
jmushi1:

Yes, tunahitaji viongozi. Lakini mengi ya matatizo hayo ni attitudes zetu kama jamii.

Vijana wengi wa Tanzania wanapotumia technologies au viongozi wao wanapoagiza technologies wanafikiria kuwa umeshuka from outerspace. Lakini wagefikiri kuwa kuna watu wame-invest mawazo yao hili vitu vitokee, basi tungetumia jitihada kubwa kwenye investment ya elimu na mambo yanayomfanya mtu kufikiria zaidi kuliko kutafuta short cuts.
 
Last edited by a moderator:
Idimi itabidi tuwasiliane. Maana nahitaji umeme kwa shughuli zangu tu binafsi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom