kenethedmund
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 347
- 89
Ni wakati sasa umefika kwa Watanzania tuandamane nchi nzima kupinga uhuni unaofanywa na Serikali iliyoko madarakani haiwezekani tatizo la umeme liwe linatutesa kiasi hiki karibia kila mwezi ukiangalia umeme unakatika mara ngapi utakuta karibia siku 10 za mwezi mzima hakukuwa na umeme na hata zaidi. Na hapo bado mgao wa umeme haujatangazwa lakini kimya kimya. Tutawezaje kuzalisha katika taifa ambalo gharama za umeme ni kubwa lakini bado tunashindwa kupata huduma bora ya umeme na ya uhakika kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana.
Na viongozi wanaendelea kupita bila kujali kuwa uzalishaji tunaofanya katika mazingira magumu ndio unaofanya tuweze kulipa kodi na wao kupata posho za safari zao pamoja na mishahara minono ila wanashindwa kumthamini Mtanzania wa hali ya chini na hata wa juu ambaye anachangia katika uzalishaji wa kila siku. Wanatujia na majibu mepesi kwenye maswali magumu na kujitahidi kutuaminisha kuwa wanafanya kazi na kwamba wanasambaza umeme vijijini ikiwa asilimia 18% ya Watanzania ndio tunaotumia umeme na bado tunapata umeme wa kubahatisha na wamashaka kiasi cha kupelekea uchumi kuzidi kudorora.
Naomba tujadili kuna haja gani yakubaki na Serikali hii madarakani ikiwa inaweza kufanya usanii na maisha ya Watanzania kiasi hiki. Mpaka leo bado Umeme ni tatizo kwenye Taifa hili na pia kuna haja gani ya kuendelea kulipa kodi ikiwa huduma tunayopewa hailingani na kodi tunazotozwa.
Nawasilisha