Tatizo la umeme limefikia mahala kwa watanzania kuandamana nchi nzima

kenethedmund

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
348
195
Ni wakati sasa umefika kwa Watanzania tuandamane nchi nzima kupinga uhuni unaofanywa na Serikali iliyoko madarakani haiwezekani tatizo la umeme liwe linatutesa kiasi hiki karibia kila mwezi ukiangalia umeme unakatika mara ngapi utakuta karibia siku 10 za mwezi mzima hakukuwa na umeme na hata zaidi. Na hapo bado mgao wa umeme haujatangazwa lakini kimya kimya. Tutawezaje kuzalisha katika taifa ambalo gharama za umeme ni kubwa lakini bado tunashindwa kupata huduma bora ya umeme na ya uhakika kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana.

Na viongozi wanaendelea kupita bila kujali kuwa uzalishaji tunaofanya katika mazingira magumu ndio unaofanya tuweze kulipa kodi na wao kupata posho za safari zao pamoja na mishahara minono ila wanashindwa kumthamini Mtanzania wa hali ya chini na hata wa juu ambaye anachangia katika uzalishaji wa kila siku. Wanatujia na majibu mepesi kwenye maswali magumu na kujitahidi kutuaminisha kuwa wanafanya kazi na kwamba wanasambaza umeme vijijini ikiwa asilimia 18% ya Watanzania ndio tunaotumia umeme na bado tunapata umeme wa kubahatisha na wamashaka kiasi cha kupelekea uchumi kuzidi kudorora.

Naomba tujadili kuna haja gani yakubaki na Serikali hii madarakani ikiwa inaweza kufanya usanii na maisha ya Watanzania kiasi hiki. Mpaka leo bado Umeme ni tatizo kwenye Taifa hili na pia kuna haja gani ya kuendelea kulipa kodi ikiwa huduma tunayopewa hailingani na kodi tunazotozwa.

Nawasilisha
 

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
^^
Mambo ya kitaifa yanapogeuka miradi ya wachache, wanaumia wengi waliogawika kwa misingi ya udini,ukabila na vyama.
Neno ALUTA CONTINUA litabaki vinywani na si ktk utendaji
^^
 

markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
195
Hatauwezi kuwa na maendeleo kama umeme utakuwa sio imara. Ili kukuza uchumi wa nchi nishati ni moja ya vitu muhimu sana. Kuanzia majumbani, makazini viwandani etc. Hawa Tanesco wanapandisha bei kila siku, lakini hawaboreshi huduma mi nafikiri pia hii wizara imekuwa sugu na imeongozwa na mawaziri wengi lkn tatizo liko pale pale. Turuhusu kampuni binafsi kuingia katika sector hii kuondoa huu ukiritimba wa Tanesco. Kama ilivyo kwenye cm hakuna mwenye haja na TCCL tena
 

juve2012

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
3,339
2,000
Watanzania tumeicheza ngoma ya mafisadi vya kutosha tena bila ya kupenda.Nadhani ifike wakati na wao waanze kuicheza ngoma yetu iwe wanataka au hawataki.Lakini niitazamapo nchi hii mitaani,barabarani,kwenye daladala na magari binafsi,maofisini,kwenye biashara,mijini na vijijini,naona sura za watz waliokata tamaa na kuchoshwa na taabu za maisha haya,lakini sioni sura za watu walio tayari kudai haki zao.Naona wanyonge waoga.Wanasema kuna utumwa wa akili.Mimi nasema na utumwa wa moyo upo pia.Hofu ni utumwa wa moyo.Na moyo ulio katika kifungo cha hofu hauna maisha marefu.Amkeni Watanzania.Muokoe nafsi zenu na giza nene mbele yenu.Watazidi kuwanyonya hadi mjitambue na kusimama kutetea haki zenu.
 

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,053
2,000
Watanzania tumeicheza ngoma ya mafisadi vya kutosha tena bila ya kupenda.Nadhani ifike wakati na wao waanze kuicheza ngoma yetu iwe wanataka au hawataki.Lakini niitazamapo nchi hii mitaani,barabarani,kwenye daladala na magari binafsi,maofisini,kwenye biashara,mijini na vijijini,naona sura za watz waliokata tamaa na kuchoshwa na taabu za maisha haya,lakini sioni sura za watu walio tayari kudai haki zao.Naona wanyonge waoga.Wanasema kuna utumwa wa akili.Mimi nasema na utumwa wa moyo upo pia.Hofu ni utumwa wa moyo.Na moyo ulio katika kifungo cha hofu hauna maisha marefu.Amkeni Watanzania.Muokoe nafsi zenu na giza nene mbele yenu.Watazidi kuwanyonya hadi mjitambue na kusimama kutetea haki zenu.

Mkuu umesema yote niliyotaka kuyasema.
Ukweli utabaki kuwa ukweli. Wakati wa kuongea majukwaani na kwenye mitandao umekwisha.
Hakuna atakayekuja kuwasaidia watanzania, iisipokuwa watanzania wenyewe.
Huu 'uhuru' ambao kila mwaka watanganyika husherehekea ifikapo Desemba 9 haujamkomboa mtanganyika.
Ni wakati sasa wa kila mtanganyika aliyechoka aamue kuikomboa nchi yetu kutokana na mkoloni huyu fisadi anayeendelea kutuangamiza huku akijinadi ya kuwa ni yeye tu anayeweza kututoa kwenye hali hii.
Shida ya umeme ni moja tu ya changamoto zinazomkabili mtanganyika, ambaye hana matumaini ya kuondokana na shida na karaha bila kuuondoa mfumo mzima uliopo.
Muda wa maneno ya majukwaani umekwisha, watanzania tudai haki yetu ya kupatiwa huduma muhimu kama umeme wa uhakika na zinginezo. Tukisubiri vibali vya kugoma na kuandamana, basi tujue tunaangamia wote!!!
 

Kaka1

Member
Aug 7, 2013
87
95
Sioni ccm atayekuja na mawazo ya kuwakomboa watanzania, Wanaojifanya wema leo ni kutaka uongozi kisha kwa faida ya familia zao,wakati mjini na vijijini kuna shida na karaha mfano umeme na maji,UKIWAZA KWA UMAKINI JUU YA MALI ZA NCHI ZINAVYOTUMIKA UTAPUNGUZA SIKU ZA KUISHI.
 

Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
20,925
2,000
Kwakweli hili tatizo la umeme limekua kero sugu,ni kero ni kero yani hadi hasira,wanakata umeme hovyo bila taarifa na siku hizi wameongeza masaa ya giza,jana wamekata kwa masaa 22. Sasa kwa style hii hayo maendeleo yatachkua mda sana.
 

SUYA

Senior Member
Jun 24, 2009
128
195
Hii nchi bila sku kuingia barabarani haiwezekani tena kuishi kwa ahadi na matamko yenye mikakati hewa.
Nchi haiendeshwi kwa kaulimbiu by Mch Msingwa
 

BARRY

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
418
250
Mgomo wa kitaifa wa umeme.....unafahamu ni Asilimia ngapi Ya wa tz Wanapata Huduma ya umeme? Only 14 percent...86 percent wanakaa kwenye giza! Shame on you..goma Wewe na TANESCO yako.
TANESCO inatakiwa wawekeze kwenye miundombinu ili kukuza Namba ya Wateja
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom