Tatizo la umeme limeanza lini? Kweli tumekosa suluhisho?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la umeme limeanza lini? Kweli tumekosa suluhisho??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyani Ngabu, Oct 15, 2009.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi hili tatizo la umeme liemeanza lini Tanzania? Mwaka huu 2009? 2008? 2000? 1995? 1990? 1985? 1980? 1975? 1970? 1965? 1960? 1955?

  Nauliza kwa sababu huu mjadala unavyojadiliwa unanipa impression ya kwamba hili ni tatizo jipya (lililoanza miaka hii ya karibuni). Mnaojua saidieni.....
   
 2. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi naona tatizo hili limeanza toka umeme ulipokuwepo. Hata nyumba za nyumba za ibada (Makanisa, misikiti) miaka ya nyuma kabisa walijenga makanisa madogo na wakati huo yalitosheleza tena na kubaki. Lakini baadaye waumini walipozidi kuongezeka hatimaye wakawawekea mgao yaani wengine wasali ibada ya kwanza halafu baadaye wengine watasali ibada ya pili, hatimaye ya tatu na kuendelea na mwishowe wakaamua kujenga makanisa makubwa zaidi.


  Vivyo hivyo hata upande wa umeme kadri siku zinavyokwenda ndipo na matumizi ya umeme yanapoongeza. Kwa hiyo serikali kwa kushirikiana na Tanesco inatakiwa kuangalia namna ya kuongeza uzalishaji wa umeme kadri siku zinavyokwenda.
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Tatizo la umeme bongo mimi kipindi nazaliwa nililikuta.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo la Umeme haswa limeanza mwaka 1990. ndipo tulipoanza kusikia hizi hadithi za bwawa limeziba na umeme wa mgao na kadhalika, lakini kama unataka kujua mahitaji yetu ya umeme kulingana na uzalishaji uliopo nadhani hili limeanza zamani isipokuwa uwezo pia wa wananchi ulikuwa mdogo sana.
  Nakumbuka miaka ya 70 na 80 kuweka umeme ilikuwa deal yaani mwenye fedha yeyote yule aliweza kuvuta umeme nyumbani kwake au kiwandani. Hata maji safi ilikuwa kwa mwenye uwezo zaidi ya kukosekana kwa maji au kukatika kwa maji. Hatukuwahi kusikia hili neno Umeme wa Mgao ila tulikuwa na mgao wa chakula!
  Hivyo hiyo asilimia 12 ambayo inawapa umeme leo ilikuwa ni ndio asilimia 60 hadi 80 ya wakati ule kama watu wangekuwa na uwezo wa kuvuta umeme.. yaani umeme ulikuwa bwelele lakini wananchi wenye uwezo mdogo - Athari za Ujamaa.
  Tatizo la leo ni kwamba hata kama unayo fedha, umeme hautoshi na bado tuinakatiwa mgao na kuwa tatizo jingine juu ya matatizo asilia.
   
 5. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Tatizo la umeme hapa tz mbona linakuwa sugu?
  Tanzania ina mito na maziwa mengi pamoja na wataalamu.
  Kwanini tunazidi kukosa umeme kulika hata nchi ndogo kama Rwanda na Burundi?
  Chanzo cha mto Nile ni Ziwa Victoria lakini mto huu unaifaidisha Uganda na mataifa ya kaskazini mwa Afrika.
  Kwani lipi ni suluhisha la upungufu huu wa umeme?
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  rais kasema tatizo la umeme tz ni mitihani ya mungu so sie tunamuachia mungu atatupa nafuu
   
 7. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Tatizo hili la upungufu wa umeme hapa tz halina suluhisho?
  Kwanini rasilimali tulizo nazo hazitusaidii?
   
 8. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mitihani ya Mungu au ya Shetani?
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Subiri RICHRUKW a.k.a richmond ndiyo itamaliza tatizo.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mgao ulianza kipindi hicho, 1990. Lakini Tanesco hawajawahi kusema kuwa tatizo hilo limetokana na watumiaji wengi wa umeme kulingana na umeme unaozalishwa. Toka awali tatizo la umeme limekuwa likihusishwa na kukauka kwa mabwawa ya nyumba ya mungu, mtera kidatu etc.Tukumbuke kuwa kwa muda mrefu sana umeme wetu ulikuwa thermo hivyo ununuzi wa mafuta ya kuendesha ulitegemea fedha na sio hali ya hewa. Hydro ilikuwa source ndogo ya umeme mpaka ilikpokuja national grid tukaona mahydro ya nini, tukatangaza tenda na kuuuza mitambo ikabaki labda wilayani na baadhi ya mikoa.Kwa ufupi, baada ya mikoa mingi kuunganishwa grid ya taifa tulisahau kuwa huenda kungekuwa na shortage ya maji hivyo hatukuweka fallback position matokeo ndio haya. Kuanzia hapo hakuna mkakati wa muda mrefu wa kumaliza tatizo hili, mipango yote ni zimamoto, ndio tunapata IPTL, Richmond, dowans nakadhalika
   
Loading...