Tatizo la umeme: Kwa miaka 60 sasa, kiakili bado tupo utumwani kwa wakoloni weusi (kiutawala) wananchi sisi ndio mzigo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,986
144,313
February 2018, Kampuni za umeme, Australia zilitakiwa kulipa fidia kwa wakazi wa Victoria, nchini Australia waliothirika kwa kukosa umeme, malipo ya $180 kutegemeana na muda ambao 'nyumba ilikosa umeme'. Zilitengwa $5M. Umeme ulikatika kati ya saa 3—20.

Huku kwetu Mabwepande, umeme unakatwa bila taarifa, hakuna anaejali, ni wewe Mwananchi kujitetea tena ukibembeleza waurudishe. Vinyozi, wachomelea vyuma, mafundi aluminum, wachapaji, banks etc hasara ni zao sio vinginevyo, nani wa kuwatetea? Nani wa kuwalipa fidia kwa hasara yao?

Serikali iruhusu uwekezaji wa kampuni binafsi za kutoa huduma za umeme, TANESCO ni kama wameshindwa hii kazi kabisa. Nchi inakwenda 'blackouts' tangu asubuhi hadi usiku? Mnajichekesha tu.. Nchi yetu tumekabidhi kwa watu wasiokuwa na sera, mikakati na blueprint za kuendesha nchi.

Tufanye kama Singapore. Sekta ya umeme ipo chini ya Singapore Power. Wanatoa huduma za umeme na gesi, wanasambaza huduma, kwa wateja wake. It is one of the largest corporations in Singapore. Sasa hawa SP wako na 'Major subsidiaries' ambao wanawasaidia kufanya huduma zao.

Mfano; PowerGas, AusNet Services, SP PowerGrid, SP powerAssets, SP Telecom, SP service, Nje ya hapo kuna SP wapo na Major joint ventures, mfano; Power Automation hawa wanahusika to offer engineering services in protection systems.

Substation control & energy management and information systems across the country. Pia wapo Singapore District Cooling. Involving the centralised production of chilled water for distribution to commercial buildings. Serikali ikajifunze vitu hivi kutoka Singapore na Malaysia?

Kufikia November 2011, Singapore waliunganisha zaidi ya 80% ya huduma ya gesi to power-generation companies which go to turn the gas into electricity and feed it into the national grid. 20% inayobaki inatoka kwenye fuel oil and other sources such as waste and renewable energy.

Ok! Mtasema Singapore ni wakongwe, basi tutumie mfano wa Malaysia. Nchi ambayo tunalingana nayo umri. Kwa mujibu wa 'energy commission' kuna more than 18 utilities and major power producers. Though, Energy suppliers in Malaysia are regulated by the state.

The Department of Gas and Electricity Supply Act maintains price regulation. Fedha ya mteja ndio inaendesha shirika la umeme Tanzania na nyingine inatumika kwenye REA na TRA huko. Tena mteja anatoa fedha ya malipo kabla ya matumizi. Kwanini mteja adhulumiwe haki yake?

Umeme unakatika siku nzima wakati mteja amelipia huduma kwa ajili ya matumizi yake? Ofisi za serikali na hata Ikulu ni wateja wa TANESCO wa Post-paid, hawana shuruba hizi wanazokutana nazo wateja wa kawaida wa TANESCO wa Pre-paid. Umeme kwao haukatiki kwa sababu ya LUKU.

Miaka 60, (nusu karne na miaka 10) bado kuna zaidi ya 37 million Households hazina umeme. 32% ya watanzania ndio pekee yenye kutumia umeme wa TANESCO. Vijijini 17% na mjini 65%. Zingatia, vijijini ndio kuna wakazi wengi kuliko mjini. Rural population 68%. Urban population ni 32.3%

Mfumo wa manunuzi ya umeme hauna backup? TANESCO wanapokea kodi kutoka kila transaction ya kununua umeme, waboreshe sasa mfumo huo. Hizi hasara nani atafidia kwa wananchi? Mtumiaji analipa VAT, EWURA, REA katika fedha anayonunua umeme. Sio hisani. Ni huduma za malipo. Tunataka huduma bora.

Mfano, ukinunua umeme kwa njia ya mitandao ya simu, umeme wa Tsh 1,000/- Cost (gharama) 819.68, VAT (kodi ya ongezeko la thamani) 18%—147.53, EWURA (Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji) 1%—8.20, REA (wakala wa umeme vijijini) 3%—24.59, TOTAL 1,000.00

Kwa miaka 60 sasa, tumetoka UTUMWANI kimwili na kiakili bado tupo UTUMWANI kwa wakoloni WEUSI (kiutawal) Wananchi sisi ndio MZIGO. Tunawekwa gizani, tunakosa umeme kwa uzembe wa serikali lakini tunashindwa kuiwajibisha serikali kwa uzembe wake. Leo watu walipaswa kuwajibishwa kwa kuwekwa gizani hovyo!

Umeme ukirudi, tunashangilia “huoooooooo” kama tumepata uhuru, tunakwenda kulewa, kunyoosha nguo, kucheza PS, kuchaji simu na power bank, kutengeneza nywele, kuangalia Ertugrul na Ndanga na kufanya ngono halafu tunalala, kesho tena wanakata. Tunaanza upya. Sisi ni VILAZA!

#MMM, Martin Maranja Masese
 
"...ukirudi tunashangilia huooooo"
Miaka 60 sasa tuko hapo. Na wanasema bado mingine 940 ifike 1000 wanayosema watatawala.

Miaka 60 hakuna contingency plans yakitokea majanga ya aina yoyote. Mwaka huu mvua zilizidi, baadhi wakamlalamikia Mungu. Jua/joto limekithiri lawama kw wafugaji, wamwagiliaji...nk

Kuna maeneo yenye mito ya misimu ambapo kuna uwezekano wa kutegesha maji mengi kuzalisha mabwawa na mengine hata kuzalisha kiasi flani cha umeme lkn waapi!
Miaka yoote tumekuwa na ng'ombe, umwagiliaji lkn sasa imekuwa balaa. Na huenda sasa wenye mifugo mingi watakiona, wenye mashamba ya umwagiliaji, wataipata, isipokua sijasikia wachimbaji madini wenyekutumia maji mengi... au kuna wahusika huko? Wala kwa kuwa tuna mbuga za utalii na tembo, faru, nyati wanakunywa maji mengi, sasa baas!

Au pengine tuna laana ya kupata watawala mabomu! Kila mwaka unaokuja ni mbaya kuliko ulopita! Ikiwa ni hivi, tutafikia hiyo 1000 wanayoiota?! Haitafika mahala watu wakasema "enough is enough", liwalo na liwe? Na ikiwa hawataki katiba mpya wanafaidika na hii yenye viraka, watamlaumu nani!?

WaTz wafike mahala wakubali kuwa miaka 60 ya maafa ya katiba mbovu yatosha na kwamba imefika mahala, nguo imejaa viraka, haifai kuongeza kiraka kingine tena, tuweze ondoa maviongozi bomu bila kumwaga damu, ebo!
 
Kama watanzania tumeshindwa kuwaondoa hao wavivu wa kufikiri basi tuendelee kuvumilia tu
 
Tunajua sana kuchambua matatizo yetu,tuanze sasa kuandika namna ya kuyatatua.
Tatizo sio watu kuandika namna ya kutatua changamoto zetu,maana kama ni kuandika watu wameshaandika na kushauri sana ila hayo mawazo yote yanabaki kwenye makabrasha kabatini.Tatizo lipo kwenye aina ya viongozi tulionao.ndo maana kwa miaka 60 bado hakuna hata jambo moja ambalo tunaweza kujivunia kua tumelifanya kwa ufanisi wa angalau asilimia 90,afya shida,elimu shida,miundombinu tabu,uchumi hoi.ongeza mengine.
 
Magufuli alitaka kuongeza kwenye Gridi ya Taifa zaidi ya MW 2000, wakampinga wakafunga safari kwenda Misri na kucancel mradi, sasa tuna MW 1500 tu kwenye nchi yenye watu zaidi ya milioni 45.

Kama ma slow thinking wasingefuta Stiegler ndani ya mwaka tungefikisha MW karibia 5 000, …
 
Tatizo sio watu kuandika namna ya kutatua changamoto zetu,maana kama ni kuandika watu wameshaandika na kushauri sana ila hayo mawazo yote yanabaki kwenye makabrasha kabatini.Tatizo lipo kwenye aina ya viongozi tulionao.ndo maana kwa miaka 60 bado hakuna hata jambo moja ambalo tunaweza kujivunia kua tumelifanya kwa ufanisi wa angalau asilimia 90,afya shida,elimu shida,miundombinu tabu,uchumi hoi.ongeza mengine.
Tumeshajua siku nyingi tatizo ni viongozi so what next?! sasa naona tatizo ni mimi na wewe, ni sisi, tumelala mno tunasubiri miujiza.
 
Ni aibu kubwa.
Ili taifa liendelee kiuchumi na kuwa na viwanda na kazi kwa wingi, UMEME NA MAJI ni kipaumbele kikubwa.
Tanzania ni siasa tu na ubambikiaji kesi wanaotaka kuonyesha yale tunayotaka.
 
Tatizo sio watu kuandika namna ya kutatua changamoto zetu,maana kama ni kuandika watu wameshaandika na kushauri sana ila hayo mawazo yote yanabaki kwenye makabrasha kabatini.Tatizo lipo kwenye aina ya viongozi tulionao.ndo maana kwa miaka 60 bado hakuna hata jambo moja ambalo tunaweza kujivunia kua tumelifanya kwa ufanisi wa angalau asilimia 90,afya shida,elimu shida,miundombinu tabu,uchumi hoi.ongeza mengine.
Kubadilisha mfumo ni mchakato unaoweza kuchukua hata karne na karne.Lakini sisi kama watu mmoja mmoja tunaweza anza kutafuta suluhisho.Kwa mfano kijiji/mtaa unaweza kuanzisha miradi ya visima vya maji,pia wanaweza kujadili namna ya kuanza kuzalisha umeme.
 
Back
Top Bottom