Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu limefika kileleni. Serikali ichukue hatuna kuepusha matatizo ya kisiasa na kijamii

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,907
2,769
Hili ni kwa serikali na watunga Sera wa Taifa hili. Kuna tafiti moja nilikuwa nasoma imefanywa na Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, nimeshangaa kuona hili tatizo lilipofikia. Sio kwamba nilikuwa sijui bali tatizo ni kubwa na vijana waliohitimu vyuo vya elimu ya juu kwa maelfu hawana kazi wala matumaini.

Kwa wale wanaokuja na kauli kwamba hawa vijana wangejiajiri labda wajiulize hili, upatikanaji wa mikopo ukoje kwenye taasisi za kifedha? As far as I know financial institutions nyingi zinakopesha operating businesses, sio startups, wanakopesha a working business, ambayo financial flow yake inaeleweka, it is financially predictable.

Suala la vijana kudai ajira ni haki yao kwa taifa lao, ndio maana Rais Trump always brags via Twitter kwa jinsi gani amepunguza unemployment mpaka asilimia 3%, kwa maana nyingine asilimia 97 ya Wamarekani wana kazi.

Suala la ukosefu wa ajira is a serious political business, na lisipochukuliwa hatua na serikali kwa kujenga mazingira either ya vijana kujiajiri au kuajiriwa, let's call a spade a spade, lazima majanga ya kisiasa yanatungoja, vijana wamekata tamaa, wamekuwa mizigo kwenye familia. I do understand its not their choices to be jobless and hopeless, mbinu zimeisha, kama hauna kazi na hauna mtaji what can you do?

Hebu tusaidie hawa vijana, hali yao ya kimaisha ni mbaya, kelele kwenye mitandao ya kijamii haitaisha. We have to find a solution.

Serikali itafuta namna ya ku-empower hawa vijana before they become a political threat kwenye jamii yetu. They deserve a better future. Mtu anawezaje kumaliza Cambridge na Masters yake nzuri na anahangaika mtaani? Inasikitisha sana.

Let's find a workable solutions, kwani serikali haiwenzi anzisha programs kubwa za kilimo na zikawapa graduates maeneo ya kulima strategic food products hata for export and industrial raw materials? Mchina anataka muhogo wa kutosha, kuna Chia seeds, kuna kokoa, mazao kibao, kwanini serikali isianzishe mashamba makubwa hawa vijana wape kazi kama viwanda mambo yanaenda taratibu?

Ni ombi tu. Tusijifikirie sisi tulio maofisini. Hawa vijana wasiposaidia leo, kesho watakuwa watumwa kwenye nchi yao wenyewe.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hatuna pesa za kuajiri,tuna pesa za kujenga miundo mbinu....
Serikali inatanua fursa in jukumu LA walengwa kuisaidia serikali,tena kwa kulipa kodi stahiki na kufanya marejesho ya mikopo walio itumia vyuoni...
 
Hii Serikali yetu inawaza Kujenga Madaraja, Kununua ndege Ila suala la ajira Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila kutengeneza miundombinu wezeshi hizo ajira zitatoka wapi? Tanzania ilikuwa imekaa kama kisiwa! Kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine unatumia 12 up to 24 hours njiani na ukifika lazima ulale hiyo shughuri utaifanya kesho yake! Kujenga SGR, ununuzi wa ndege, madaraja mafupi na marefu, Barabara za mwendo kasi, umeme wa uhakika bonde la nyerere, mtandao mzuri wa barabara za lami, miundombinu ya uduma za afya, n.k. Haya yoote anayoyafanya JPM yangetakiwa yafanywe na watangulizi wake! Shame on his predecessors! Miundombinu na mazingira wezeshi ya kiuchumi yakiwa sawa ajira na kujiajiri inawezekana. SGR itamwezesha mtanzania kusafirisha ndizi za bukoba kutoka mwanza mpaka Dar ndani ya masaa 12. Vijana wetu wakiwa Dar au Mwanza wakipata mchongo wa hela ndani ya masaa 8 tayari mtu kaishasafiri toka Dar to Mwanza. Jamani msimtwishe JPM mizigo iliyotakiwa kubebwa na awamu zilizopita!
 
Mleta mada anasema:
"......Mtu anawezaje kumaliza Cambridge na Masters yake nzuri na anahangaika mtaani? Inasikitisha sana."

Wengi wa hao ni kutishia watu mitaani kuwa nimesoma. Kama wana qualifications hizo hiweje waangaike na kupiga domo la kukosa ajira? Hawa ndo white color job seekers na kutishia watu na makaratasi ya vyeti ambavyo haviwasaidii wao vitawezaje kusaidia jamii. Kama umegraduate Cambridge inamaana wewe unahela ya mtaji wa biashara basi jiajiri? Kama ulishindwa kusave few millions zikusaidie kujiajiri unataka serikali ikusaidieje? Kaza buti JPM watu wacome-up to their senses!
 
Hili swala ni gumu sana,siyo tu kisiasa ila kijamii na kiuchumi.
Ni kweli serikali haiwezi kuwaajiri wote. Lakini tunahitaji kujiuliza kidogo.
Kwa nini waliongeza shule na vyuo vikuu ?(sifa)
Je waliandaa mazingira kwa wahitimu?(siasa)
Na wahitimu je,waliambiwa ukweli kuhusu yaliyombele yao?(jamii)
Wakati namaliza diploma yangu,mkuu wa chuo alitumia saa sita kuhitimisha (alishafundisha sana) tujue tunarudi kwa jamii,tutapata kazi na tutaishije mazingira tofauti tofauti. Ukipelekwa kijijini kafanane na wanakijiji huku ukiendelea kuwa na taaluma yako.
Maisha siyo shule,hakuna suspension Wala kufukuzana!jichanganye bila kupotea.
Asee masela walilia walipoambiwa huko unaweza hata kulala njaa,na zile penalty za kijamii Kama kujikuta juu ya bati asubuhi.
 
Mkuu hapa nilikuwa nakusanya takwimu niandike suala kama hilo. Uzuri umeniwahi basi naomba nikupe pongezi kwa andiko hili.

Tunafahamu vijana wahitimu wa diploma na degree wapo wa fani mbalimbali. Lakini hizi fani zote zipo zinazoingiliana katika mnyonyoro wa thamani ambapo ukiinua wale wa kilimo, ufugaji (kuku, samaki nk), uvuvi nk basi utatoa ajira kwa mainjinia, masoko, nk.

Wenzetu wa PASS (https://pass.or.tz) wameanzisha program ya vijana na wanawake ambayo kundi la kwanza limetoka baada ya mafunzo ya mwaka mmoja. Sasa wameanza kuwapa mikopo vijana hao ili waanzishe mashamba yao ya kilimo kwa kutumia green house na wale wengine ni wafugaji wa mbuzi. Huu ni mwanzo, lakini vijana hawa wanaosimamiwa na PASS ni wachache ukilinganisha na kundi lililopo mtaani.

Matarajio yangu Serikali ingechukua mfano huu na kuundeleza kwa vijana wengine kwa uhakika. Nimelifuatilia na nasikia Benki ya Kilimo nayo imeingia mkataba na PASS lakini bado haitoshi.

Tuna bahari ambayo vijana tu waliomaliza elimu ya ufugaji samaki kwa mfano wakapewa mafunzo maalum ya kuzalisha samaki na kufuga katika vizimba kwa kutumia mfano wa program ya PASS tutatengeneza ajira nyingi. Vile vile kwa Ziwani. Katika kilimo kama ulivyosema nako ni hivyo. Hapa nchini kuna wataalam wa sekta nyingine wakitumiwa wanaweza wakaja na mawazo ya wale waliohitimu fani nyinginezo kama habari, mawasiliano, uchakataji wa vitu / bidhaa mbalimbali nk wanaweza wakatengeneza ajira kwa namna ipi.

Huu ni mfumo, hivyo wataalam husika wa mipango mikakati na uwekezaji wanaweza kuleta jawabu mfumo huu kwa ukubwa wake utekelezwe vipi.

Ombi: Mh. Rais tunakuomba tumia hata 1.5 Trillion (figure tu ya kuhamasisha) kuwekeza katika hili. Utawezesha kuongeza ajira kwa vijana hapa nchini. Tuna sehemu ya kuanzia ya kujifunza kupitia PASS (wanaweza kuwa na mapungufu lakini kwakuwa wameanza tunaweza kuboresha).
 
Dunia ya leo vyanzo vya ajira ni vingi sana kama vikiruhusiwa vijana wajipambanue kusaka fursa za kidunia ambazo ni pana zaidi kuliko tu fursa twa restricted area (yani Tanzania pekee) hapo ndo unakutana na msaada wa kiteknolojia sasa ambao vijana uzuri wake wana uelewa nao mzuri sana mfano instgram kuigeuza kuwa vipato, blogs, youtube, affiliate marketing, forex or commodities trading, etc hizi dunia za wenzetu zina watu wamewekeza na wanapiga hela maisha yanaenda ......njoo kwetu sasa kijana hata ki channel cha youtube na blog anaombwa akatie leseni kwa laki kadhaa 😂😂 nadhani utajua kiwango chetu cha kufikiri kilivyo haba.
1.png

Note: Vijana wa kitanzania watadumu kuwa maskini tu kwa aina ya sera na miongozo inayo fanywa na walioshiba salary slip.
 
Mkuu hapa nilikuwa nakusanya takwimu niandike suala kama hilo. Uzuri umeniwahi basi naomba nikupe pongezi kwa andiko hili.

Tunafahamu vijana wahitimu wa diploma na degree wapo wa fani mbalimbali. Lakini hizi fani zote zipo zinazoingiliana katika mnyonyoro wa thamani ambapo ukiinua wale wa kilimo, ufugaji (kuku, samaki nk), uvuvi nk basi utatoa ajira kwa mainjinia, masoko, nk.

Wenzetu wa PASS (https://pass.or.tz) wameanzisha program ya vijana na wanawake ambayo kundi la kwanza limetoka baada ya mafunzo ya mwaka mmoja. Sasa wameanza kuwapa mikopo vijana hao ili waanzishe mashamba yao ya kilimo kwa kutumia green house na wale wengine ni wafugaji wa mbuzi. Huu ni mwanzo, lakini vijana hawa wanaosimamiwa na PASS ni wachache ukilinganisha na kundi lililopo mtaani.

Matarajio yangu Serikali ingechukua mfano huu na kuundeleza kwa vijana wengine kwa uhakika. Nimelifuatilia na nasikia Benki ya Kilimo nayo imeingia mkataba na PASS lakini bado haitoshi.

Tuna bahari ambayo vijana tu waliomaliza elimu ya ufugaji samaki kwa mfano wakapewa mafunzo maalum ya kuzalisha samaki na kufuga katika vizimba kwa kutumia mfano wa program ya PASS tutatengeneza ajira nyingi. Vile vile kwa Ziwani. Katika kilimo kama ulivyosema nako ni hivyo. Hapa nchini kuna wataalam wa sekta nyingine wakitumiwa wanaweza wakaja na mawazo ya wale waliohitimu fani nyinginezo kama habari, mawasiliano, uchakataji wa vitu / bidhaa mbalimbali nk wanaweza wakatengeneza ajira kwa namna ipi.

Huu ni mfumo, hivyo wataalam husika wa mipango mikakati na uwekezaji wanaweza kuleta jawabu mfumo huu kwa ukubwa wake utekelezwe vipi.

Ombi: Mh. Rais tunakuomba tumia hata 1.5 Trillion (figure tu ya kuhamasisha) kuwekeza katika hili. Utawezesha kuongeza ajira kwa vijana hapa nchini. Tuna sehemu ya kuanzia ya kujifunza kupitia PASS (wanaweza kuwa na mapungufu lakini kwakuwa wameanza tunaweza kuboresha).

unaangalia wapi course structure zao??wangapi wamemaliza hio course na kupewa mikopo??,nimeingia lakini sijaona..msaada please...
 
Dunia ya leo vyanzo vya ajira ni vingi sana kama vikiruhusiwa vijana wajipambanue kusaka fursa za kidunia ambazo ni pana zaidi kuliko tu fursa twa restricted area (yani Tanzania pekee) hapo ndo unakutana na msaada wa kiteknolojia sasa ambao vijana uzuri wake wana uelewa nao mzuri sana mfano instgram kuigeuza kuwa vipato, blogs, youtube, affiliate marketing, forex or commodities trading, etc hizi dunia za wenzetu zina watu wamewekeza na wanapiga hela maisha yanaenda ......njoo kwetu sasa kijana hata ki channel cha youtube na blog anaombwa akatie leseni kwa laki kadhaa 😂😂 nadhani utajua kiwango chetu cha kufikiri kilivyo haba.View attachment 1311176
Note: Vijana wa kitanzania watadumu kuwa maskini tu kwa aina ya sera na miongozo inayo fanywa na walioshiba salary slip.

ki youtube mpk ulipie hela!! wenyewe ndio wanaona wamebuni chanzo cha mapato...😅😅😅
 
Tatizo Afrika mtu akiwa hana shida basi hawezi kufikiria wenzie but what goes around comes around, kama sio wajukuu zao basi vitukuu vyao vitakuja kupata shida kama wapatazo watoto wa maskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dua la kuku halimupati mwewe, wangeacha zile technical colleges, na professional colleges, lakini zote zimekuwa converted into degree college vijana wengi wanamaliza degree hata kujieleza ni zero kabisa, na hawa unasema wanasubiri ajira, wanasubiri sana mpaka karatasi zao za degree zitafanana na wao walivyo na ukungu kichwani. Vyuo vya kilimo, Ufundi na biashara zingesaidia sana kupunguza tatizo ndo maana China wanaconvert degree college kuwa technical college vijana wasome hali halisi ya maisha ya dunia lakini sisi tunaconvert technical na professional college kuwa degree college. Kukalili kupata A a B na GPA kubwa lakini technically ni zero kwenye uhalisia wa maisha ya sasa.
 
Mleta mada anasema:
"......Mtu anawezaje kumaliza Cambridge na Masters yake nzuri na anahangaika mtaani? Inasikitisha sana."

Wengi wa hao ni kutishia watu mitaani kuwa nimesoma. Kama wana qualifications hizo hiweje waangaike na kupiga domo la kukosa ajira? Hawa ndo white color job seekers na kutishia watu na makaratasi ya vyeti ambavyo haviwasaidii wao vitawezaje kusaidia jamii. Kama umegraduate Cambridge inamaana wewe unahela ya mtaji wa biashara basi jiajiri? Kama ulishindwa kusave few millions zikusaidie kujiajiri unataka serikali ikusaidieje? Kaza buti JPM watu wacome-up to their senses!
Tatizo unaongea without some senses, kwanza huyo amesoma Kwa scholarship cz he was smart enough, wamemaliza amerudi kazi hakuna. Pia unafikili watu wangapi wana qualifications nzuri na kazi hamna? Hivi kwann usiwe na akili na kujua suala LA ajira sio Siasa ni uchumi? Unataifa vijana maelfu hawana kazi na unaleta domo? Mkapa mwenyewe ameliongelea hili suala LA ajira, you think you're smarter than him?
 
unaangalia wapi course structure zao??wangapi wamemaliza hio course na kupewa mikopo??,nimeingia lakini sijaona..msaada please...
Nimeweka website ili kuwapa mwangaza wa PASS. Ila nenda kwenye news utaona tangazo kituo atamizi. Nimefuatilia tangia wamechukua vijana awamu ya kwanza na sasa najua wapo waliokopeshwa wachache, wengine wapo katika hatua maana walikuwa hawana mashamba yao binafsi. Na sasa wapo na batch ya pili katika mafunzo. Taarifa zaidi wapigie wwenyewe PASS.Mimi nimefurahishwa na ndio maana nawafuatilia nione mwisho wake. Asante
 
Back
Top Bottom