Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu limefika kileleni. Serikali ichukue hatuna kuepusha matatizo ya kisiasa na kijamii

Bila kutengeneza miundombinu wezeshi hizo ajira zitatoka wapi? Tanzania ilikuwa imekaa kama kisiwa! Kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine unatumia 12 up to 24 hours njiani na ukifika lazima ulale hiyo shughuri utaifanya kesho yake! Kujenga SGR, ununuzi wa ndege, madaraja mafupi na marefu, Barabara za mwendo kasi, umeme wa uhakika bonde la nyerere, mtandao mzuri wa barabara za lami, miundombinu ya uduma za afya, n.k. Haya yoote anayoyafanya JPM yangetakiwa yafanywe na watangulizi wake! Shame on his predecessors! Miundombinu na mazingira wezeshi ya kiuchumi yakiwa sawa ajira na kujiajiri inawezekana. SGR itamwezesha mtanzania kusafirisha ndizi za bukoba kutoka mwanza mpaka Dar ndani ya masaa 12. Vijana wetu wakiwa Dar au Mwanza wakipata mchongo wa hela ndani ya masaa 8 tayari mtu kaishasafiri toka Dar to Mwanza. Jamani msimtwishe JPM mizigo iliyotakiwa kubebwa na awamu zilizopita!
ok embu tueleze SGR yakutoka bongo kwenda Morogoro inasolve hili tatizo kwa asilimia ngapi? Nauli za ndege zimepanda two times, na moshi imepelekwa treni badala yakusafiri nusu siku unasafiri siku nzima, gari zimefungwa fleet management system safari iliokua ya siku moja tunatumia two days! Kama hizi ndio njia zakuongeza ajira kwa kuimprove mobility Kwakweli yajayo yanafurahisha
 
Mkuu hapa nilikuwa nakusanya takwimu niandike suala kama hilo. Uzuri umeniwahi basi naomba nikupe pongezi kwa andiko hili.

Tunafahamu vijana wahitimu wa diploma na degree wapo wa fani mbalimbali. Lakini hizi fani zote zipo zinazoingiliana katika mnyonyoro wa thamani ambapo ukiinua wale wa kilimo, ufugaji (kuku, samaki nk), uvuvi nk basi utatoa ajira kwa mainjinia, masoko, nk.

Wenzetu wa PASS (https://pass.or.tz) wameanzisha program ya vijana na wanawake ambayo kundi la kwanza limetoka baada ya mafunzo ya mwaka mmoja. Sasa wameanza kuwapa mikopo vijana hao ili waanzishe mashamba yao ya kilimo kwa kutumia green house na wale wengine ni wafugaji wa mbuzi. Huu ni mwanzo, lakini vijana hawa wanaosimamiwa na PASS ni wachache ukilinganisha na kundi lililopo mtaani.

Matarajio yangu Serikali ingechukua mfano huu na kuundeleza kwa vijana wengine kwa uhakika. Nimelifuatilia na nasikia Benki ya Kilimo nayo imeingia mkataba na PASS lakini bado haitoshi.

Tuna bahari ambayo vijana tu waliomaliza elimu ya ufugaji samaki kwa mfano wakapewa mafunzo maalum ya kuzalisha samaki na kufuga katika vizimba kwa kutumia mfano wa program ya PASS tutatengeneza ajira nyingi. Vile vile kwa Ziwani. Katika kilimo kama ulivyosema nako ni hivyo. Hapa nchini kuna wataalam wa sekta nyingine wakitumiwa wanaweza wakaja na mawazo ya wale waliohitimu fani nyinginezo kama habari, mawasiliano, uchakataji wa vitu / bidhaa mbalimbali nk wanaweza wakatengeneza ajira kwa namna ipi.

Huu ni mfumo, hivyo wataalam husika wa mipango mikakati na uwekezaji wanaweza kuleta jawabu mfumo huu kwa ukubwa wake utekelezwe vipi.

Ombi: Mh. Rais tunakuomba tumia hata 1.5 Trillion (figure tu ya kuhamasisha) kuwekeza katika hili. Utawezesha kuongeza ajira kwa vijana hapa nchini. Tuna sehemu ya kuanzia ya kujifunza kupitia PASS (wanaweza kuwa na mapungufu lakini kwakuwa wameanza tunaweza kuboresha).
Mawazo mazuri sana
 
My two cents:
1. Idadi ya watu: Tusipodhibiti ongezeko la idadi ya watu Tanzania, hili bomu litakuwa kubwa zaidi. Ikiwa juzi tu UNICEF wameproject zaidi ya watoto 5,000 wamezaliwa siku ya mwaka mpya, hebu fikiria idadi hiyo ndani ya mwaka, halafu zaidi ya asilimia hamsini wataingia kwenye soko la ajira by 2040..

2. Makuzi (malezi), Elimu na Ujuzi: nafasi ya kila mmoja kama mwananchi hujengwa na aina ya makuzi anayoyapitia. Je tunalelewa kukabili vipi changamoto za ukubwani na kuwa wananchi wa aina gani? Lishe bora hasa kwa watoto chini ya miaka mitano ni jambo muhimu sana sana sana. Halafu, e elimu yetu inatutayarisha kutumia talanta zetu ipaswavyo? Tunapata ujuzi wa kutosha kutumia na kutengeneza fursa?

3. Sekta binafsi ni mwajiri na mtengeneza fursa maalum katika nchi yoyote. Serikali ni msimamizi, mwezeshaji na mkusanya kodi. Tukiimarisha mazingira ya sekta binafsi kushamiri na kukua, vilevile tutaongeza wigo wa ajira na fursa za kujiajiri.
 
Umezungumza point muhimu sana. Naamini itatendewa kazi
Hili ni kwa serikali na watunga Sera wa Taifa hili. Kuna tafiti moja nilikuwa nasoma imefanywa na Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, nimeshangaa kuona hili tatizo lilipofikia. Sio kwamba nilikuwa sijui bali tatizo ni kubwa na vijana waliohitimu vyuo vya elimu ya juu kwa maelfu hawana kazi wala matumaini.

Kwa wale wanaokuja na kauli kwamba hawa vijana wangejiajiri labda wajiulize hili, upatikanaji wa mikopo ukoje kwenye taasisi za kifedha? As far as I know financial institutions nyingi zinakopesha operating businesses, sio startups, wanakopesha a working business, ambayo financial flow yake inaeleweka, it is financially predictable.

Suala la vijana kudai ajira ni haki yao kwa taifa lao, ndio maana Rais Trump always brags via Twitter kwa jinsi gani amepunguza unemployment mpaka asilimia 3%, kwa maana nyingine asilimia 97 ya Wamarekani wana kazi.

Suala la ukosefu wa ajira is a serious political business, na lisipochukuliwa hatua na serikali kwa kujenga mazingira either ya vijana kujiajiri au kuajiriwa, let's call a spade a spade, lazima majanga ya kisiasa yanatungoja, vijana wamekata tamaa, wamekuwa mizigo kwenye familia. I do understand its not their choices to be jobless and hopeless, mbinu zimeisha, kama hauna kazi na hauna mtaji what can you do?

Hebu tusaidie hawa vijana, hali yao ya kimaisha ni mbaya, kelele kwenye mitandao ya kijamii haitaisha. We have to find a solution.

Serikali itafuta namna ya ku-empower hawa vijana before they become a political threat kwenye jamii yetu. They deserve a better future. Mtu anawezaje kumaliza Cambridge na Masters yake nzuri na anahangaika mtaani? Inasikitisha sana.

Let's find a workable solutions, kwani serikali haiwenzi anzisha programs kubwa za kilimo na zikawapa graduates maeneo ya kulima strategic food products hata for export and industrial raw materials? Mchina anataka muhogo wa kutosha, kuna Chia seeds, kuna kokoa, mazao kibao, kwanini serikali isianzishe mashamba makubwa hawa vijana wape kazi kama viwanda mambo yanaenda taratibu?

Ni ombi tu. Tusijifikirie sisi tulio maofisini. Hawa vijana wasiposaidia leo, kesho watakuwa watumwa kwenye nchi yao wenyewe.

Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila kutengeneza miundombinu wezeshi hizo ajira zitatoka wapi? Tanzania ilikuwa imekaa kama kisiwa! Kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine unatumia 12 up to 24 hours njiani na ukifika lazima ulale hiyo shughuri utaifanya kesho yake! Kujenga SGR, ununuzi wa ndege, madaraja mafupi na marefu, Barabara za mwendo kasi, umeme wa uhakika bonde la nyerere, mtandao mzuri wa barabara za lami, miundombinu ya uduma za afya, n.k. Haya yoote anayoyafanya JPM yangetakiwa yafanywe na watangulizi wake! Shame on his predecessors! Miundombinu na mazingira wezeshi ya kiuchumi yakiwa sawa ajira na kujiajiri inawezekana. SGR itamwezesha mtanzania kusafirisha ndizi za bukoba kutoka mwanza mpaka Dar ndani ya masaa 12. Vijana wetu wakiwa Dar au Mwanza wakipata mchongo wa hela ndani ya masaa 8 tayari mtu kaishasafiri toka Dar to Mwanza. Jamani msimtwishe JPM mizigo iliyotakiwa kubebwa na awamu zilizopita!
Miundo mbinu zjengwe lakn mkuu jiulize zile hospital idadi kubwa zilizojengwa na serikal nan anefanya kaz au mmeajir wachawi?
 
Mleta mada anasema:
"......Mtu anawezaje kumaliza Cambridge na Masters yake nzuri na anahangaika mtaani? Inasikitisha sana."

Wengi wa hao ni kutishia watu mitaani kuwa nimesoma. Kama wana qualifications hizo hiweje waangaike na kupiga domo la kukosa ajira? Hawa ndo white color job seekers na kutishia watu na makaratasi ya vyeti ambavyo haviwasaidii wao vitawezaje kusaidia jamii. Kama umegraduate Cambridge inamaana wewe unahela ya mtaji wa biashara basi jiajiri? Kama ulishindwa kusave few millions zikusaidie kujiajiri unataka serikali ikusaidieje? Kaza buti JPM watu wacome-up to their senses!
Broo hayajakukuta amin kwamba kuna watu yan ukoo wote amna aliajirw licha ya kua wamesma baadh ambao wangepat ajira wangepeana company mitaji wote wanatoka, kujiajir bila mtaj n kugum sana maana hata bank haimkopesh asie na kitu
 
Watu wanaona kwamba mtu haitakiwi aajiriwe eti tujiajiri. Ukienda kuchukua mkopo benki ili uwazishe biashara watakuuliza unakiwanja. Una duka. Una nyumba .ya kuwekeza. Kuajiriwa muhimu. Unamwambia fresh graduate ajiajiri. Unataka awekeze benki kitumbua au tigo ili apate mtaji. Tuache kujitoa ufahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa la kwanza ni kufikiria kua serikali inatoa ajira, yaani kua na mentality hiyo tu ni kufeli hata kabla ya kuanza mapambano.
Kitu cha pili, hivi vijana wenzangu hua tunatafutaga wapi "mitaji" na tunakosa?? Isije ikawa taarifa tu za upatikanaji wa mikopo hauna na hata elimu juu ya namna ya kutafuta mtaji hauna halafu unalalamika kua "mitaji hakuna" mana zipo njia nyingi tu za kupata mitaji sio lazima ukope sasa kabla hujaanza kuonyesha kibanzi kwenye jicho la mwenzio (kulaumu) hebu kwanza toa boriti kwenye jicho lako, hebu hakikisha kwanza tunayafahamu haya? Tunayajua nje ndani?
Halafu sio lazima kung'ang'ania mitaji toka hapa ndani tu, let's get out from our comfort zone, huko nje kuna watu wana mitaji yao ya kutosha tu wanatafuna SERIOUS startups za kuwekeza why not taking a risk and going for it?
Kwanini nasema kuilaumu serikali na kuitegemea on this it's a wrong idea? Kwa sababu tunasahau kua entrepreneurship and entrepreneurs are the ones that drives the economy of any successful nation let me give you an example.
Facebook sio kampuni ya serikali, Google sio kampuni ya serikali, Microsoft sio kampuni ya serikali, Coca-Cola sio kampuni ya serikali and the thing is... Tunachelewa kuamini kua haya makampuni yalianzishwa na wajasiriamali kama hawa hawa tuliinao hapa kwetu na haya makampuni makubwa yanachangia mapato makubwa sana katika nchi zao plus nafasi za ajira.
Hivyo kama tunataka kusukuma uchumi wa wananchi wetu mmoja mmoja na kiujumla lazima wahitimu wetu wa vyuo wabadili mindset zao kua za kiujasirilia mali. And watakuja hapa na lawama kua serikali ibadili mfumo wa elimu yes, Serikalini inawajibu wake on this but wakati serikali ipo kwenye "michakato" kwa hiyo tunafanyeje sasa hapa kati kati? Tuisubirie serikali? (na kama unavyojua ilivyo slow?)
Mimi nategemea sasa wahitimu wetu watumie nafasi tuliyonayo kwa sasa ya kuwepo kwa knowledge kwenye mtandao kuji update na kuja na ideas za kibunifu badala ya kuilaumu serikali na mtaala wake wa elimu.
I'm sorry to say this but kwa msomi kulilia kukosekana kwa ajira ni aibu!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni kwa serikali na watunga Sera wa Taifa hili. Kuna tafiti moja nilikuwa nasoma imefanywa na Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, nimeshangaa kuona hili tatizo lilipofikia. Sio kwamba nilikuwa sijui bali tatizo ni kubwa na vijana waliohitimu vyuo vya elimu ya juu kwa maelfu hawana kazi wala matumaini.

Kwa wale wanaokuja na kauli kwamba hawa vijana wangejiajiri labda wajiulize hili, upatikanaji wa mikopo ukoje kwenye taasisi za kifedha? As far as I know financial institutions nyingi zinakopesha operating businesses, sio startups, wanakopesha a working business, ambayo financial flow yake inaeleweka, it is financially predictable.

Suala la vijana kudai ajira ni haki yao kwa taifa lao, ndio maana Rais Trump always brags via Twitter kwa jinsi gani amepunguza unemployment mpaka asilimia 3%, kwa maana nyingine asilimia 97 ya Wamarekani wana kazi.

Suala la ukosefu wa ajira is a serious political business, na lisipochukuliwa hatua na serikali kwa kujenga mazingira either ya vijana kujiajiri au kuajiriwa, let's call a spade a spade, lazima majanga ya kisiasa yanatungoja, vijana wamekata tamaa, wamekuwa mizigo kwenye familia. I do understand its not their choices to be jobless and hopeless, mbinu zimeisha, kama hauna kazi na hauna mtaji what can you do?

Hebu tusaidie hawa vijana, hali yao ya kimaisha ni mbaya, kelele kwenye mitandao ya kijamii haitaisha. We have to find a solution.

Serikali itafuta namna ya ku-empower hawa vijana before they become a political threat kwenye jamii yetu. They deserve a better future. Mtu anawezaje kumaliza Cambridge na Masters yake nzuri na anahangaika mtaani? Inasikitisha sana.

Let's find a workable solutions, kwani serikali haiwenzi anzisha programs kubwa za kilimo na zikawapa graduates maeneo ya kulima strategic food products hata for export and industrial raw materials? Mchina anataka muhogo wa kutosha, kuna Chia seeds, kuna kokoa, mazao kibao, kwanini serikali isianzishe mashamba makubwa hawa vijana wape kazi kama viwanda mambo yanaenda taratibu?

Ni ombi tu. Tusijifikirie sisi tulio maofisini. Hawa vijana wasiposaidia leo, kesho watakuwa watumwa kwenye nchi yao wenyewe.

Mungu ibariki Tanzania.
Ajira n betting n forex

Lazma vjana tuchkue maamuz stahik 2020 inafikia wakat contents juu ya koz uliyo soma inapotea kichwan. Refer to the Use and Dis use theory by Lamarckism'
 
Sio siri kuna ukweli na hili ni tatizo

maoni yangu
in the short run
Vijana shika ufanye kazi yoyote iliyoko mbele yako walau upate chochote kwa kuanzia.,
Hata kama hujaisomea hio mana hali ya soko si nzuri

kubuni na kujishughulisha na kile unachopenda nje ya kazi za kuajiriwa maadam kinaweza kukuingizia pesa...mfano kufundisha tuitionkuonyesha hata mpira,grocery,duka,ufundi, kutoa huduma flani hapo ulipo na ukaichaji pesa, upishi,house keeping,kilimo nk

Ni mtu kukaa na kuwaza kwa mazingira haya niliyopo jamii inayonizunguka inahitaji nini ambacho nikiwapa wanaweza nilipa nikawa nasogeza siku

for the long run...issue kubwa sio siri ni malezi na maandalizi...tuwaandae watoto/vijana kujitegemea na kujishughulisha mapema

Stadi za maisha kuanzia nyumbani na technical schools zishike kasi mapema mashuleni ili mtu aweze kujiajiri kuanzia ufundi,kilimo mpaka housekeeping

wazazi tuchukue hatua mapema tuanzishe shughuli za kiuchumi na tuwafundishe watoto ingali mapema..si vyema kukomaa nao soma soma tuuu utapata kazi nzuri tuwaze nje ya box

serikali ije na namna ya kuwasogeza vijana
Mfano project za Kilimo cha umwagiliaji,ufadhili wa kiasi flani ili kuanza biashara flani..mtu/kikundi wanakuja na wazo mnampima mnampa mtaji japo kidogo ili kuchochea mzunguko flani na vijana wapate matumaini
 
kubuni na kujishughulisha na kile unachopenda nje ya kazi mfano kufundisha tuitionkuonyesha hata mpira,grocery,duka,ufundi, kutoa huduma flani hapo ulipo na ukaichaji pesa, upishi,house keeping,kilimo nk

Hizo biashara Mtaji anautoa wapi, vijana sio hawaoni fursa MTAJI wanautoa wapi mtu mfukoni hana hata Shs 10.

Portfolio | 2020
 
Mfano kufundisha tuition ni akili yako mwenyewe andaa mazingira watoto wakae wafundishe

Kazi za ndani ni nguvu zako pia...u may babysit ukacharge pesa,unaweza fanya gardening,upishi usafi, ufundi nk..kikubwa anza tu
Kazi za kujitolea ni nguvu na juhudi zako pia
Lengo ni kuanza/kupata shughuli unaoga asubuhi unatoka au unajishughulisha japo uanze tu mbele kwa mbele utajiongeza utakutana na watu na fursa zitajitokeza

nakumbuka nilishafundisha watoto shule miezi kadhaa na sijasomea ualimu na nishawahi fanya kazi ya kujitolea ndo badae mambo yakaenda sawa

u js need to start
Asikuambie mtu hamna kitu kizuri kama kutoka asbh uende duniani kuchangamana na watu...unafungua akili
 
Tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa sana hapa Tanzania. Ni tatizo kubwa kuliko inavyofikiriwa na kwa bahati mbaya linawagusa watu wengi sana kuliko hata hao graduates wenyewe.
Immediate solution should be introduced to mitigate the problem, otherwise the future is not exciting at all.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfano kufundisha tuition ni akili yako mwenyewe andaa mazingira watoto wakae wafundishe

Kazi za ndani ni nguvu zako pia...u may babysit ukacharge pesa,unaweza fanya gardening,upishi usafi, ufundi nk..kikubwa anza tu
Kazi za kujitolea ni nguvu na juhudi zako pia
Lengo ni kuanza/kupata shughuli unaoga asubuhi unatoka au unajishughulisha japo uanze tu mbele kwa mbele utajiongeza utakutana na watu na fursa zitajitokeza

nakumbuka nilishafundisha watoto shule miezi kadhaa na sijasomea ualimu na nishawahi fanya kazi ya kujitolea ndo badae mambo yakaenda sawa

u js need to start
Asikuambie mtu hamna kitu kizuri kama kutoka asbh uende duniani kuchangamana na watu...unafungua akili
hivi hizi akili za kuandika haya bila kufikiria huwa mnazitoa wapi?
 
Back
Top Bottom