Uke kutoa harufu kali(Vaginal Odor): Chanzo, dalili na tiba zake

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
1642396453025.png

Nimeona hii article sehemu nikaona niwashirikishe wenzangu ili kama mna jamaa zenu wenye matatizo haya ili kuyakabili. Kutoka harufu ukeni kunaumiza sana.

Kama kuna njia nyingine watu mnajua basi wasaidie ambao wanahitaji msaada wenu.
===

Tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni
Kutunza uke na kulinda afya ya uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke. Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni kiashiria kwamba unaumwa na hauko sawa. Hali hii inaweza kuathiri heshima ya mwanamke na pia mahusiano na mwenza wake.

Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida. Japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.

Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo la samaki basi ujue kuna tatizo kubwa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaji.

Sababu Za Uke Kutoa Harufu Mbaya:
Zipo sababu nyingi zinazopelekea mwanamke kutokwa na harufu mbaya ukeni, baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;


A) Magonjwa Ya Zinaa (Sexually Transmitted Diseases).

Mfano wa magonjwa ya zinaa ni pamoja na kisonono, kaswende, Trichomoniasis n.k. Magonjwa haya yasipotibiwa kwa wakati hupelekea mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni.


B) Matumizi Mabaya Ya Dawa Za “Antibiotics”.

Hutumiaji kiholela wa dawa hizi bila ushauri au maelekezo ya wataaalamu wa afya (daktari) ni mojawapo ya sababu ya mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni. Hivyo ni vyema mwanamke akafuata ushauri na maelekezo ya wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa za Antibiotics.

C) Kutozingatia Usafi Na Kutokwa Sana Na Jasho.

Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya.Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (Apocrine sweat glands) hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo ya mwili.

D) Maambukizi Katika Via Vya Uzazi (Pelvic Inflammatory Disease).

Pelvic Inflammatory Disease (PID) hili ni tatizo linalotokana na magonjwa sugu ya zinaa kama vile gonorrhea, chlamydia. Hivyo magonjwa ya zinaa ambayo hayakugundulika mapema, tiba hafifu, au uzembe wa kutumia dawa ni chanzo kimojawapo cha mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni.

E) Bacterial Vaginosis.
Kwa kawaida mwili wa binadamu una bakteria wa aina mbili, bakteria rafiki (normal flora) na bakteria adui (pathogens) ambapo ukeni kuna bakteria rafiki kwa kiwango kinachohitajika, bakteria hawa wanapoongezeka na kuvuka mahitaji huwa sio rafiki tena, huanza kushambulia sehemu ya uke na kuruhusu maambukizi ambayo hutoa majimaji yenye harufu mbaya ukeni.


F) Mabadiliko Ya Homoni.
Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi (menopause) wapo kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana na hivo kusababisha tishu za kuwa na tindikali kidogo.

DALILI.
Kama tatizo hili litatokana na kisonono tatizo dalili zake zitakua zile za kisonono ambazo ni;
  • Maumivu wakati wa haja ndogo
  • Mkojo kutanguliwa na usaha n.k

Kama chanzo ni kaswende basi hali hiyo itaambatana na miwasho mikali na kidonda katika mlango wa uke, kidonda hiki huwa hakina maumivu pindi unapokigusu.

Kama itatokana na fangasi watokanao na maambukizi katika via vya uzazi vilevile muathirika anaweza kupata miwasho.

ANGALIZO
Wakati mwingine sio lazima mtu atokewe na dalili hizi isipokua maji meupe kama maziwa yaliyo via, weupe unaoelekea kwenye unjano.

Mambo Ambayo Mwanamke Hatakiwi Kufanya Wakati Wa Kusafisha Uke Wake
1) Vaginal Douching.

Hii ni ile tabia ya kuosha sehemu nza ndani ya uke kwa kutumia viosheo maalumu vinavyopatikana madukani au super markets mbalimbali. Pia vaginal douching ni kule kutumia sabuni za maji au maji maalumu ambayo yanakuwa yamechanganywa na iodine, vinegar, magadi na kuyaingiza ndani ya uke, hii ni hatari kwa afya ya uke wako.

Ikumbukwe vaginal douching ni tofauti kabisa na ule unawaji wa kawaida au uoshaji wa kawaida wa uke wakati wa kuoga kwani haijakatazwa kuosha uke kwa maji ya uvuguvugu kwani ni salama na hakuna matatizo kiafya.

Njia bora ya kusafisha uke ni kutumia maji ya vuguvugu pale unapooga kwa kusafisha sehemu za nje na sio ndani ya uke kwani sehemu ya ndani uke hujisafisha wenyewe (vagina is self cleansing).

b) Vaginal steaming​

Hiki ni kitendo cha kujifukiza uke kwa kutumia marashi yaitwayo YONI STEAM ambapo mwanamke hukaa juu ya kiti ambacho chini yake kuna bakuli yenye maji ya moto na mvuke huo huenda moja kwa moja kwenye sehemu za uke. Kitendo hiki hufanywa kwa nia ya kusafisha uke lakini kimepigwa vita na madaktari wengi ambao wanaeleza kuwa kitendo hiki huwaondoa bakteria wanaotakiwa katika kurekebisha mfumo wa homoni na hivyo kusababisha madhara.

Hatua 6 za Kujikinga dhidi ya Harufu Mbaya Ukeni

1. Vaa nguo za ndani za pamba, zisizobana sana

Nguo zilizoabana zinazuia kupita kwahewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.

2. Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi
Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.

3. Punguza uzito kama inawezekana
Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na kama tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu inaleta fangasi na bacteria wabaya. Chagua kula lishe nzuri na kufanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako. Unaweza kutuma kifurushi chetu cha weight loss package ili upunguze uzito wako vizuri pasipo kujinyima kula.

Epuka Kuflash Uke Kila Mara (Douching)
Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bacteria wazuri. Bakteria hwa ni walinzi, na hivo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bacteria wabaya pamoja na fangasi wa candida.

Epuka Kutumia Spray na Marashi Ukeni
Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray kuingia kwenye damu. Usiingie kwenye mtego huu, kumbuka miili yetu imeumbwa kujisafisha yenyewe, Pale unapoongeza kitu cha ziada basi unaharibu normal flora na kuharibu kinga ya mwili.

Epuka Baadhi ya Vyakula Ambavyo ni Adui wa afya yako
Kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vianweza kukuathiri wewe kama mwanamke kwenye swala la uzazi. Vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bacteria wazuri na kubadili PH. Vyakula vyenye sukari, Pombe, ngano na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa fangasi wa Candida.
 
Naombeni msaada wa majina ya dawa, mpenzi wangu ana tatizo la kunuka kwenye uke (vagina) pindi tukimaliza kufanya sex, inatokea harufu mbaya sana.

Kama kuna mtu anajua jina la dawa aniambie pliz
 
mwambie awe msafi na awe anaosha manta vizuri . ikishindikana achape mwendo hospt.
 
Dah! Nazikumbuka hizo harufu. Tena huwa zinafanana na harufu za pumba za chakula cha mifugo. Awe anakunywa maji mengi
 
Thank you for this usefu thread. Unajua dada wa kazi amekuwa na hili tatizo kwa muda mrefu nafikiri leo ndiyo limeisha. Nimeprint nampeleke a leo nimsomee vizuri na kumfundisha.

Asante kwa website hiyo, itasaidia wengi.
 
naombeeni msaada wa majina ya dawa,mpenzi wangu ana tatizo la kunuka kwenye uke(vagina) pindi tukimaliza kufanya sex,inatokea harufu mbaya sana.kama kuna mtu anajua jina la dawa aniambie pliz
Kabla ya kukimbilia madawa ajaribu kwanza kuosha K vizuri, baadhi ya dada zetu hawajui kuosha, anapiga maji juu basi amemaliza-mwambie awe anaingiza vidole kunako anasafisha na maji mengi.

Kukitakata vidole inakuwa shida kuingia tofauti na wakati kuchafu. Kama bado harufu inatoka then hilo ni tatizo anaweza kutafuta madawa
 
poa kaka amejaribu kusafisha lakini bado harufu ni ile ile hafanyeje?
 
Kabla ya kukimbilia madawa ajaribu kwanza kuosha K vizuri, baadhi ya dada zetu hawajui kuosha, anapiga maji juu basi amemaliza-mwambie awe anaingiza vidole kunako anasafisha na maji mengi. Kukitakata vidole inakuwa shida kuingia tofauti na wakati kuchafu. Kama bado harufu inatoka then hilo ni tatizo anaweza kutafuta madawa

Kuntaaaa....
 
naombeeni msaada wa majina ya dawa,mpenzi wangu ana tatizo la kunuka kwenye uke(vagina) pindi tukimaliza kufanya sex,inatokea harufu mbaya sana.kama kuna mtu anajua jina la dawa aniambie pliz

Hata akipewa dawa gani kama haoshi nanihii baada ya kunanihii tatizo linakuwa vile vile mwambie ajifundishe kusafisha sehemu zake za siri. mbegu zisipomea na zikaoza zinatengeneza harufu mbaya..
 
Kuntaaaa....

Hata mimi nimeshangaa kama wewe...Sina hakika kama amesoma post yangu kuhusu huo ushauri wake na madhara ya douching.

Anyway, naona ni mwendo wa kipofu kumwongoza kipofu mwenzake...tatizo ni kuwa wanacheze maeneo nyeti sana!
 
kwa msaada zaidi pia mwambie asafishe kwa kutumia maji ya uvuguvugu atie chunvi kidogo na ndimu au delto aingize vidole hadi ndani ikiwezekana alale chali umsafishe mwenyewe ila atanue miguu ili uweze kusafisha kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom