Kalamu Huru
Member
- Dec 2, 2017
- 11
- 8
Wasalaam,
Kalamu huru imevutika kuandika kidogo kuhusu mjadala wa muda mrefu wa Lowasa kuhamia CHADEMA.
Ikumbukwe kuwa, ni haki ya kikatiba kila mwananchi kujiunga au kuachana na chama chochote cha siasa. Hivyo, kuhama chama kwa kwenyewe, sio tatizo.
Kikubwa, tunaamini anajiunga kwa kuwa anakubaliana na misingi, falsafa na itikadi ya chama ajiungacho. Sote twajua hizi sio sababu zilizompeleka Lowasa CHADEMA. Ila sitajikita kwenye hilo leo.
Pamoja na yote hayo, ilipaswa mwenye kuja chamani abadilike kulingana na misingi, falsafa na itikadi ya chama.
Tatizo la ujio wa Lowasa CHADEMA ni chama kubadilika kufiti ujio wa Lowasa badala ya Lowasa kubadilika kufiti misingi, falsafa na itikadi ya chama. Hilo tu.
Ni muhimu sasa kwa chama kutengeneza (nurture and mould) vijana ambao wataweza si tu kuwa wagombea, bali viongozi wa nchi. Hii pokea pokea makapi ya CCM na kuyaamini na kuyapa nafasi nyeti bila hata kuwachunguza kwa kina dhimira zao hakukisaidii chama katika kipindi cha muda mrefu (in the long run). Matokeo yake ndio haya ya watu kuacha nafasi za uwakilishi na kumuunga mkono Rais.
Ni muhimu chama kuukubali ukweli, kuupokea na kufanya jitihada kurekebisha ili tuwe na upinzani wenye afya.
The Quill.