Tatizo la udumavu wa Upinzani wa Nchi hii ni kwa sababu ya viongozi madikteta wanang'ang'ania madaraka

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Katika hali ya kawaida tu huwezi kuzuia jambo fulani lisifanywe na wale eti ni baya ilhali wewe ndiwe mshirika mkuu kwalo.

Mbowe na Zitto ni vinara wa mahubiri demokrasia na kwalo ni wazungumzaji taralia mithili ya tarumbeta japokuwa na kwa mshangao wao ki uhalisia si wanademokrasia.

Unaitaje wengine dikteta wakati nawe ndiye.

Mbowe ni dikteta mkuu ndani ya Nchi hii anayeongoza taasisi huru ki dikteta.

Miaka zaidi ya 20 umeongoza taasisi kwa mbinu zilezile na hata kama ulibadiri na zilifeli hakika haipo sababu ya yeye kubaki hapo.

Kuminywa na kukimbilia ng'ambo ni sababu tosha ya kuwaelewa madikteta ya maslahi-vyama kwamba hawapo na wafuasi wao.

KIONGOZI SHUPAVU WA UPINZANI NI YULE AWAYE TAYARI KWA GHARAMA YEYOTE KUPINZANA NA WAFUASI WAKE KWENYE ENEO LA UPINZANI NA SI UPINZANI WA KWENYE TWITTER.

Dikteta Mbowe apishe damu mpya kwa sababu hana tena kipya.
 
Wewe ni mwana chadema? Kama wenyewe hawalalamiki wewe unalallamika kama nani? Magufuli analalamikiwa kwa sababu alikuwa kiongozi wa nchi siyo wa chama!

Ulishawahi kusikia watu wanamlalamikia Mangula?

Kwani alianza jana kuwa kiongozi wa chama cha CCM?

Udikteta wa kiongozi haupimwi kwa mtu kukaa madarakani muda mrefu ndugu. Hata kambarage alikaa muda mrefu lakini ulishawahi sikia akiitwa dictator popote?

Jifunze zaidi kwa kusoma historia na sifa za madictator duniani Afu ulinganishe na lile dubwasha Lenu mlilofukia Kule CHATO
 
Kuna wakati huwa nawashaa baadhi wa Watanzania kama wewe na kujiuliza huwa umefikiria kabla ya kuandika ujumbe wako huu au ? Inasikitisha mtu mzima kua na mentality ya aina hii.
 
Kuna wakati huwa nawashaa baadhi wa Watanzania kama wewe na kujiuliza huwa umefikiria kabla ya kuandika ujumbe wako huu au ? Inasikitisha mtu mzima kua na mentality ya aina hii.
Hao ndiyo wapigania ccm mitandaoni
 
Wao wanasubiri wanuse harufu ya kiongozi wa CCM anataka kuongezewa muda watalalama mpaka mate yanawakauka na macho kodo kama mjusi.
leo wao hawataki kuwaachia wengine uongozi.
 
Shida yako ni upeo finyu humwoni Prof. Lipumba wa CUF amekaa muda gani?, Cheyo wa UDP, Agustino Mrema TLP, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi unamlenga Mbowe tuu huo ni utoto kuwa fair na useme ukweli
 
Back
Top Bottom