Tatizo la udini: Uaminifu wetu kwa nchi unapozidiwa na dini

Rogate

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
215
45
Nimeshuhudia mara kandaa mijadala yanye mlengo wakidini ikipata nafasi kubwa kuliko mijadala yakitaifa.
Utafiti mdogo nilioufanya nimegundua ""miaka ya hivi karibuni"" mwamko wa waTZ kuzungumza mambo yanayolihusu taifa imeongezeka sanjari na hili la udini likishika kasi.

Udini ulilipata mizizi wakati wa uchaguzi mkuu na kuendelezwa igunga..
Nimejiuliza maswali yafuatayo..
  1. Nini kimetokea kati ya watz tunaofahamika hadi nje ya mipaka yetu kama watu waungwana wanaoishi kama ndugu!!?
  2. Tabia hii ya kinyang'au tumeitoa wapi au imesababishwa na nini?
  3. Kwanini watu wanaokua mstari wambele kutetea mustakabali wa dini zao hawako mstari huohuo kuzungumzia mambo yakitaifa?
Huu unaoonekana kama uaminifu wetu kwa dini zetu ukizidi uaminifu wetu kwa taifa letu ni hatari kwa taifa letu. Tukianza kufarakana (kama bado hatujaanza) kwa mitazamo yakidini itakua kheri na watafaidika hao waliosababisha na kuanzisha huo mzozo kama tu sio waTZ, narudia kama sio WaTZ. Mfano mzuri ni wabeligiji walio wafarakanisha Warwanda kwa Utusi na Uhutu ilihali wanaongea lugha moja na mila zao ni moja.
Wabelgiji walifanikiwa kuwatawala baada ya kuwagomabanisha na walifaidi ugomvi wao bila kujali madhara yaliyowapata warwanda. Mahakama ya Arusha imehukumu Warwanda wengi na sio Wabelgiji waliopanda chuki kati ya hao ndugu.

Kama huu ni mpango wa viongozi wetu (watanzania wenzetu) wanaotaka kutawala kirahisi kwa kutumia divide and rule theory (kutawala kwa jenga uhasama kati ya watawaliwa) ni hatari kwetu tunaoshabikia dini zetu kuliko taifa letu.

Dini ni imani, taifa au nchi inamipaka yake inayoonekana nk.. Tukishindwa kuthamini vinavyoonekana tisidanganywe na dini!
Serikali na vyombo vyake viwe makini katika hili. Waliohikumiwa ICC wengi niviongozi wa serikali baadhi kwa kufumbia macho na baadhi kwa kuhusika moja kwa moja.

Watanzania tuache ushabiki wadini, tuamini dini inachosema tusichukuliwe na ushabiki.
 
Siasa za udini zimeanzishwa CCM mwaka 1999 kwa kuipachika CUF Kashfa hiyo CUF nao kwa kujua au kutojua wakaikubali na kujikita kwenye siasa hizo.
Mtaji wa siasa za udini uliendelea kuinufaisha tena CCM mwaka 2000 dhidi ya CUF
Baada ya CUF Kupungukiwa uaminifu kwa wa tz walio wengi na CDM Kuonekana ni tishio kwa CCM,ccm iliamua kwa makusudi kuitwisha CDM kashfa ya udini.
Kama alivyosema Mwalimu tuukatae udini kwa kuikataa CCM
 
Back
Top Bottom