Tatizo la uchovu kupitiliza, mwili kupata ganzi nikikaa kwa muda mrefu

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
Assalam wana jamvi, nina tatizo ambalo naombeni mnisaidie, hii kwa sasa si kawaida,

mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 sasa, ni mwajiriwa katika taasisi binafsi kwa muda wa miaka minne sasa, sijaoa japo nina mpenz ambae yupo mkoa mwingine.

tatizo langu ni uchovu uliopitiliza, yaani navyorudi baada ya kazi nakua nimechoka sana uchovu ambao sio wa kawaida, kazini naenda saa 12 na kurudi ni jioni, sina kazi nyingi sana za kusema zinanichosha.

kingine ni mwili kupata ganzi mfano nikikaa kwa muda nikisimama viungo vinauma, na wakati mwingine hupata ganzi.

kwa week mbili sasa imekua ni serious kidogo hasa baada ya kupandishwa kitengo kazini huku mkurugenzi akiwa na matarajio makubwa sana na idara yetu, nimekuwa na tafakari nyingi ambazo ndio kama zimezidisha!

Naombeni mnisaidie wajuzi wa mambo, mbinu ambazo ninaweza kuzitumia, kwani inanitisha kidogo!
 
Back
Top Bottom