Tatizo la Tezi ya Kibofu: Mazoezi, Vyakula na njia za kujihami

medisonmuta

JF-Expert Member
Oct 10, 2014
2,324
1,286
Leo wanaume wa makamo na hata vijana wanapatwa na maradhi au matatizo ambayo zamani yalikuwa ya wazee wa miaka 60-70, kuendelea…

Kati ya sababu ni;

1. Namna tunavyokula. Vyakula vyenye sukari, chumvi, visivyopikwa kiasili au nyumbani kama zamani. Tunakula njiani vitu kama "chips" zenye mafuta yaliyoshatumika mara mbili mbili au kulazwa na kutumiwa tena na tena. Muhogo uliopikwa nyumbani kwa mafuta yasiyotumika mara mbili ni bora zaidi…

Shinikizo la maisha ya kutotulia na kupata usingizi wa kutosha. Mtu mzima unatakiwa ulale saa 7 au 8 kila siku. Ukikosa tafuta usingizi mfupi mchana ("siesta" au "nap").

Kutofanya mazoezi ya viungo. Tunatakiwa tukimbize damu na kunyoosha viungo mara 3- 4 kwa juma ili kuhimili afya ya moyo na mapafu. Jambo kubwa linaloangamiza maisha ya mwanadamu ni mapafu kutofanya kazi sawasawa, mifupa kukosa uimara na mzunguko hafifu wa damu.

Haya yanaathiri moyo, ini, figo, utumbo, kizazi, afya ya ngozi, nywele, meno, mifupa, haiba, nk. Mtu kutokuwa na furaha na kuwa mlalamishi kwa kila jambo. Saikolojia ya furaha ndani yako hutokana na utulivu wa hisia na mawazo.

Badala yake twategema uchangamfu "pogo" wa pombe, dawa za kulevya, kahawa nk. Hili ni baya kwa afya ya ubongo, moyo na thamani ya uhai. Huathiri kinga maradhi ya mwili kwa jumla.

Hizi ni baadhi ya sababu.

Tatizo ninaloulizwa mara nyingi ni uume na uuke. Wote tunahusudu kufanya mapenzi na ngono. Bahati mbaya urijali unapungua; wanawake wanalalamika, nguvu zetu za undani hafifu. Moja ya tatizo kuu ni maradhi ya tezi kibofu au Prostate, kwa lugha ya Kitaalamu. Ukubwa wake ni kama wa jicho la mwanadamu.

TEZI KIBOFU
Kazi yake ni kutengeneza na kurusha mbegu za uume (shahawa). Uwezo wake huathiri mengi katika dhakari ya mwanaume, ikiwepo haja ndogo na kubwa, figo, hamu na nyege, nk. Isipoangaliwa mapema yaweza kusababisha Saratani ya tezi kibofu.

Dalili za tatizo hili ni;

1. Kutaka kukojoa (haja ndogo) mara kwa mara
2. Unapokojoa unahisi mkojo bado upo ndani lakini hautoki#
3. Mkojo unatoka kidogo kidogo kwa kubania
4. Nguvu za uume kuanza kupungua

Dalili ni muhimu kuzichunguza. Unachotakiwa mwanaume ni kwenda kwa mganga na kuangalia kama tezi kibofu au figo ziko sawa. Vipimo vinatofautiana …lakini, waganga wanafahamu. Usitumie dawa bila kupimwa kwanza.

Wakati haya yakiendelea unaweza wewe mwenyewe kuwa unajihami kwa kujiangalia na kujihudumia.
Ingawa nimeongelea mambo haya nikilenga wanaume, lakini kina dada hali kadhalika, wanaweza kusoma na kuwasaidia wapenzi wao au ndugu zao. Habari za vyakula chini ni ya faida kwa wanawake vile vile...

Zoezi la Msuli wa PC & Ulaji wa chakula;

1. Kupasha moto mboo
Kama yalivyo mazoezi yeyote ya mwili, ("warm-up") lazima mtu kujipasha moto, kabla ya zoezi lolote, maana musuli hazitaki kustuliwa. Suala la kupasha moto mboo na mapumbu kabla ya kufanya tizi hili ni muhimu sana.

Uwe bafuni, au faragha, bila usumbufu. Kama umeoa au unaishi na mwanamke, mweleze ukweli unachofanya. Usimfiche maana akikufumania siku moja atadhani mumewe unapiga punyeto bafuni kila siku kumbe sivyo. Mazoezi haya si punyeto na wala hayana uhusiano wowote na punyeto. Punyeto si mazoezi.

2. Chemsha maji. Yaweke katika kikarai, beseni au kombe safi na kipya. Usitumie chombo kilichoshatumika kabla au kwa kazi yeyote nyingine.

3. Tumia taulo safi, mpya, ndogo. Lazima iwe mpya shauri ikiwa na virusi yaweza kukudhuru. Hii taulo usiitumie kwa kazi nyingine yeyote.

4. Maji utakayotumia yawe yamechemshwa. Yasiwe na uvugu vugu wala ya moto sana. Uwe moto mkali lakini unaoweza kustahimilika. Lengo la maji haya moto ni kuipasha moto musuli ya sehemu yako ya uume.

Upashaji moto huu watakiwa kufanywa siku za mwanzo kwa mtu usiyezoea dakika tano hadi 7. Watakiwa ufanye upashaji moto, huku mboo imesimama au imedinda, kiasi cha asilimia 50, yaani kudinda angalau nusu nusu.

Kama haisimami, jaribu kutumia njia usimamishe, aidha kwa kuichezea chezea hadi isimame au njia yeyote inayokufaa au uliyoizoea.

5. Fanya mazoezi baada ya kuoga. Usifanye halafu ndiyo uoge. Kama umechoka sana waweza kufanya kifupi. Ukishazoea sana haya mazoezi utagundua kuwa dakika chache tu zinakutosha. Fanya mara moja tu kwa siku.

6. Upashaji moto wa vifaa vyako, unatakiwa ufunike mboo na mapumbu. Hali hii inachangamsha musuli kabla ya kuanza mazoezi na kuleta damu yenye nguvu sana katika uume wako. Kumbuka usizidishe moto wa maji ukajichoma. Kadiria joto la wastani. Lisiwe la chini sana wala baridi sana. Uwe moto wa kutosha kusinga na kuchangamsha mishipa yote…

2. Zoezi la PC.

- Chukua Taulo lililowaba Maji Moto, Jikande sehemu zote za uume, mapumbu, mboo kwa dakika tano hadi kumi (ukitaka), hadi mboo ilainike.

- Kaza na kulegeza musuli wa PC, mara 20. Pumzika kwa kujikanda kwa maji moto tena.

- Fanya mikamuaji 40. Pumzika dakika moja, fanya hizo arobaini mara tatu. Kila ukimaliza arobaini pumzika dakika moja.

Kulegeza na kuacha kunakuwaje?

Kumbuka unapotoa shahawa. Unakumbuka ukamuaji unavyokuwa? Basi huo huo ukamuaji unatakiwa kuufanya lakini pole pole. Endelea hivyo kwa juma moja, ukiwa ukipumzika bila zoezi baada ya kila siku tatu..

Jenga ukamuaji 100, yaani uwe unajikamua mara nne nne kwa kila mipigo hiyo 100. Kumbuka huna haja ya kufanya idadi yote hii toka mwanzo, ila kadri ya uwezo wako. Kumbuka kila aina ya mazoezi yanataka mwili uzoee, na usijiumize wala kufanya zaidi kupita kiasi. Anza na matarakimu machache halafu jenga pole pole.
(Kumbuka pia ziko aina nyingi za kufanya zoezi hili.

Waweza kufanya zoezi mathalani bila kutumia taulo lenye joto au ukiwa uchi. Wakati umekaa tu barazani ukiota jua, ukitazama runinga, ukitazama mpira, ukipiga soga, ili mradi uzoee).

Baada ya zoezi kali la idadi kubwa zaidi ya hamsini hakikisha unamalizia kwa kujikamua kwa taulo la joto.

3. Je, musuli wa PC ni kitu gani na msingi wa zoezi hili ni nini?

Zoezi la PC linatokana na musuli uitwao kwa kitaalamu PUBOCOCCYGEUS au kifupi PC. Wanaume kwa wanawake wanao musuli huu lakini kwa hapa tunaangalia ule wa wanaume. Huu ni musuli ambao husaidia kutoa au kuzuia mkojo, kinyesi na kukamua shahawa au mbegu za uhai toka ndani kwenda nje.

Ukitaka kuufahamu musuli ukoje, jaribu kukojoa, kati kati ya mkojo, zuia mkojo usitoke. Musuli unaofanya kazi hiyo ndiyo huu uitwao PC.

Uko wapi? Uko katikati ya mkundu na mapumbu. Ukiukamua unaweza kuusikia ukiushika kwa kidole.

Kwa wanawake wanaweza kuuhisi kama wakiingiza kidole ndani ya **** kisha wakakibana kidole kwa midomo ya ****. Wanawake wanaosifika kuwa wakamuaji wazuri wa **** aidha wamefanya mazoezi ya musuli huu bila kujua au kufahamu.

Kwa wanawake zoezi ya musuli huu linaweza kusaidia hasa wanawake waliojifungua, ambao wametanuka na kuwa na matatizo ya kukojoa ovyo au kupanuka sana.

Uwezo au udhaifu wa mshipa huu husaidia sana kazi zifuatazo;

1. Kukojoa au kutokojoa haraka kwa mwanaume

2. Kusaidia tezi ya kibofu ambayo hutoa umajimaji unaosafirisha shahawa. Tezi hii ikidhurika husababisha maradhi mbalimbali ikiwepo saratani ya tezi-kibofu yaani "Prostate."

3. Ukiwa na musuli wa PC uliokomaa kutokana na mazoezi mbali na kuzuia maradhi haya ya saratani waweza pia baadaye kuzuia kutotoa shahawa wakati ukifanya mapenzi. Vijana wanaokojoa haraka wanaweza kufaidika.

4. Zoezi linachangia kuongezeka ukakamavu wa mboo.

Asili ya mazoezi haya;

Mazoezi haya ya musuli wa PC yalipangwa miaka hamsini iliyopita na Mganga wa Kiyahudi aliyehamia Marekani kwa jina Alfred Kegel. Dk. Kegel lakini hakuwa wa kwanza. Kwa maelfu ya miaka wananchi wa Bara Hindi na China wamekuwa wakifanya mazoezi haya ambayo yapo katika mila na desturi zao.

Wachina kwa mfano wanaamini si vizuri mwanaume kupoteza shahawa bure. Hata wanamichezo wengi hususan mabondia wanafahamu jinsi ambavyo upotezaji wa shahawa kabla ya mashindano unavyoweza kuchangia udhaifu mwilini na kuchoka haraka.

5. Kwanini basi ufanye zoezi hili?

Kuwa na musuli dhaifu la musuli wa PC kunasababisha yafuatayo:

1. Uhanithi.
2. Kudindisha kusiko na nguvu.
3. Kukojoa haraka haraka wakati wa kufanya mapenzi. Kwa wanawake kutofikia kilele kirahisi wakati wa mapenzi.
4. Kutokuwa na nguvu wakati wa mapenzi au ashki ya kutosha hasa ukikaribia uzee.
5. Kushindwa kuzuia mkojo. Tatizo huwaandama zaidi watu wavuta sigara, walevi sana au watu ambao hawakufanya mazoezi ya mwili.

Kifupi musuli huu unaongoza na kutawala nguvu za kudinda na mfereji unaopitisha shahawa wakati wa mwanaume kufikia kilele cha mapenzi. Musuli huu pia unawezesha shahawa kutoka kwa nguvu au kwa udhaifu. Ni kama mtu ukiwa na mkono wenye musuli ndogo ukimpiga mtu ngumi haisikii kama anayefanya mazoezi ya mwili.

Ukiwa na musuli wa PC maridhawa utasaidia si tu maradhi na kinga ya uume wako bali pia kuwa na uume yenye nguvu na afya. Utakuwa mwanamapenzi wa hakika na jabali.

6. Ukishazoea zoezi.

Zoezi hili ni rahisi ukishalizoea, waweza kuyafanya kwa kuweka PUMZI juu.

1. Vuta pumzi kwa pua
2. Kamua musuli
3. Toa pumzi (kwa mdomo) huku ukiachia musuli.

Rudia tena halafu baada ya kama mara ,kumi au zaidi, jaribu:

1.Vuta pumzi kwa pua
2. Kamua musuli achia musuli
3. Toa pumzi (kwa mdomo) huku ukiwa umepumzisha musuli.

Ni kama kufanya "push-up" au kuinua vyuma kwa mikono. Unavuta pumzi, unafanya kitendo huku ukitoa badala ya KUBANA pumzi. Hapo unasaidia zaidi musuli kujijenga.

Waweza kufanya zoezi hili kwa mboo peke yake.

1. Dindisha mboo : NUSU au ASILIA MIA 70 (Yaani si lazima mboo iwe imedinda kabisa).

2. Iamshe juu na kuteremsha chini. Mwanzoni kwa kuwa musuli wako utakuwa haujazoea mboo italala baada kushusha na kuteremsha mara chache.

3. Ukishazoea chukua taulo ndogo ( au kitambaa kizito ) lenye umaji maji (yaani lepe lepe) liweke kwenye mboo yako iliyodinda. Anza mazoezi ya kuinua mboo juu na chini yaani ukiwa na hiyo taulo iliyolowana juu ya ukuni.

4. Ukishafanya kwa dakika tano hivi, itingishe mboo kulia na kushoto; ipigishe mboo yako mguu mmoja na mwingine, yaani mboo inajichapa yenyewe kulia na kushoto. Unaisukuka suka kwa kutumia kiuno. Hesabu misuko suko kama ishirini hadi hamsini. Pumzika anza tena mazoezi ya taulo mbichi juu ya mboo au "push-up" ya mboo.

Ukishamaliza kanda mboo na mapumbu kwa kitambaa au taulo yenye maji moto.

Ukishazoea baada ya miezi kadhaa;

1. Weka kitambaa cha maji moto katika mboo ILIYOSHADINDA, jikande na kujipasha moto kwa dakika tano.

2. Ukishajikanda vya kutosha, endelea na tizi. Si lazima mboo iwe imesimama.

3. Anza kukamua. Ila sasa badala ya kukaza na kukamua musuli wa PC. Kaza halafu uuache hivyo hivyo bila kuachia. Hesabu seunde 25 hadi hamsini au dakika nzima. Ongeza muda hadi dakika mbili au kwa uwezo wako.

4. Baada ya mikamuaji ya dakika tano, sasa kamua , vuta pumzi,ndani, toa, endelea kushika, ingiza pumzi na kutoa, kisha achia tena.

Huu ukamuaji ni muhimu;

Waweza kuufanya popote, lakini kuwa na siku ambazo unaufanya ukisaidiana na hiyo taulo yenye maji moto.

5. Malizia tizi kwa zoezi la kudinda na kuichezea mboo yenyewe (bila kuishika ) na kuichezea kwa kuisuka suka kushoto na kulia, ;pole pole au haraka haraka. Kisha jikande kwa taulo/kitamba chenye maji moto.

MUHIMU:

Kama yalivyo mazoezi yeyote mapya ya mwili tafadhali zingatia yafuatayo;

1. Anza kidogo kidogo. Endeleza matarakimu kadri unavyozeoa. Ukisikia maumivu yeyote ina maana umejijeruhi wacha, fanya siku nyingine.

2. Kumbuka kupumzisha mboo kila baada ya siku mbili. Au fanya leo, kesho wacha, keshokutwa fanya tena , mtondogoo wacha. Ama fanya siku tatu mfululizo pumzika mbili, na kadhalika. Hii inaipa mboo nafasi ya kukua. Wainua vyuma au wanamichezo wanajua hili. Ukifanya mazoezi au michezo lazima kupumzika ili kuupa mwili nafasi ya kujijenga.

3. Mara baada ya kuanza utaanza kuona mabadiliko fulani fulani. Kati ya haya mabadiliko ni :

1. Kuvimba zaidi mboo na mapumbu
2. Kudinda na kuwa na nyege au ashki zaidi.
3. Mboo kudinda kwa nguvu zaidi wakati wa kufanya mahaba.
4. Kujisikia vizuri, rijali au mwenye nguvu. Mazoezi yanaongeza "tetostorone" ambalo ni chimbuko la uume.
5. Mazoezi yanarutubisha afya ya mbegu zako na kukinga Saratani na maradhi ya korodani (mapumbu).

7. Zingatia afya na VYAKULA MUHIMU;

1. Usifanye zoezi baada ya kukutana na mwanamke. Utauchokesha uume wako na kujiharibu bure.

2. Zingatia kuwa mazoezi haya peke yake hayatoshi. Yabidi pia kuangalia suala la chakula. Kula chakula chenye mseto wa madini, vitamin, protini, wanga na mafuta. Kutozidisha sana pombe, na kunywa maji kama wee mlevi sana. Pombe na sigara huathiri sana nguvu za uume na kuharibu shahawa na ashki au nyege.

Je, vyakula hivi ni vipi?

MATUNDA:
Matunda kwa jumla husaidia nguvu za urijali. Watakiwa kula matunda peke yake, vizuri asubuhi, kabla ya staftai au kama sehemu ya staftai. Usichanganye matunda na vyakula vingine maana matunda huingizwa mwilini (digestion) haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Kula matunda nusu saa KABLA ya kula chakula kingine au kunywa chai. Usile matunda baada ya chakula au na chakula. Nguvu zake zinapotelea chini…

Matunda yote kijumla husaidia afya ya Dhakari; lakini haya yafuatayo yanarutuba kwa tezi kibofu, urijali wa mwanaume. Hata nyege na mbegu za mwanamke pia. Parachichi, Nanasi, Tikitiki maji (hasa matikiti maji mekundu, Tende na Tini.

VINYWAJI:
Chai ya maziwa ambazo huzipenda sana Bongo hazifai sana. Vyema kunywa chai ya rangi iliyotengezwa kwa tangawizi, karafuu, mdalasini na iliki. Ukiweza tumia asali au sukari guru (sukari isiyo nyeupe) na limau. Chai ya ----- (Nettle Tea) ni nzuri sana kwa shughuli hii ya dhakari, tezi kibofu na afya ya kizazi cha mwanamme na mwanamke. ----- unawasha ndiyo lakini faida zake hazisemeki mwilini ukitumiwa sawasawa…

MBOGA ZA MAJANI:
Mboga zote za majani zikiliwa mbichi huongeza nguvu za urijali; lakini mboga zinazoongeza nyege, afya ya tezi kibofu na ngono ni pamoja na vitungu saumu, mchaichai wa "ylang ylang" (sijui zauzwa Bongo jaribu kuulizia ktk masupamaketi; toka bara la Asia na visiwa vya Pacific)…Matango, Nyanya, Karote na Majani ya Salad yaitwayo "watercress"(ambayo siyajui kwa Kiswahili), -----, Mboga za maboga na Saladi kwa jumla. Waafrika tuna tabia kutokula Saladi. Hatari sana.

Mboga muhimu kwa tezi kibofu ni Nyanya, -----, Majani yote mabichi bichi.

MBEGU NA MADINI:
Mbegu zinasaidia sana nguvu za urijali, nyege, mishipa na ngozi. Mbegu bora ZILIWE MBICHI SI KUZIKAANGA…. bila chumvi au kupikwa: Mbegu za Maboga (pumpkin seeds), Nazi mbichi au madafu, Korosho, Mbrazili (Brazilian nuts), Mlozi(almonds), Ufuta au Mafuta ya Uto (sesame).

MAZOEZI YA VIUNGO NA MICHEZO:
Mazoezi ya UUME NA UKE yanasaidiwa pia iwapo unafanya mazoezi ya mwili : kuogelea, kukimbia au mchezo wowote unaokufanya uheme, utokwe jasho kwa wastani mara mbili kwa juma. Mazoezi YA DHAKARI peke yake hayatatosha kukupa afya ya kudumu.

Hutokea pia kwa wasiozoea siku za mwanzo kupata ashki sana nakutaka kupiga Punyeto. Kumbuka, ukipiga Punyeto unaharibu lengo au nia ya zoezi.

Punyeto inapunguza nguvu ya zoezi hili. Ukitaka kupiga Punyeto usahau zoezi hili kwa siku hiyo hadi kesho yake.
 
Back
Top Bottom