...Tatizo la Tanzania siyo sera ni utawala mbovu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

...Tatizo la Tanzania siyo sera ni utawala mbovu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Feb 15, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/2/2012 Mwanakijiji anataka tuamini kuwa sera zinapolingana basi upinzani unatakiwa usiwepo na vyama vinatakiwa kuunganisha nguvu kutekeleza sera hizo. Kwa haraka haraka unaweza kukubaliana naye lakini napenda kumkumbusha Mwanakijiji kuwa pamoja na sera zilizoandikwa kuwa sawa lakini kuna sera zisizoandikwa ambazo zinategemea mtu binafsi.

  Pamoja na kwamba sikubaliani na Mwankijiji kuwa sera za CCM na CHADEMA zinafanana lakini naamini kwa dhati kuwa changamoto kubwa tuliyonayo Tanzania hivi sasa ni UONGOZI MBOVU na siyo sera.
  1. Viongozi tulionao sasa ni wabinafsi na hivyo kupelekea kushindwa kukemea maovu.
  2. Hakuna utawala wa pamoja hivyo kuwafanya kila kiongozi kufanya na kusema anavyoona yeye inafaa.
  3. Viongozi wetu hawaheshimiani na hivyo kuwafanya wananchi kutojua wapi pa kukimbilia wakati wanapokabiliwa na matatizo ya kiuongozi.
  4. Viongozi wetu wanajijengea himaya na hivyo kijimilikisha watu kwa faida yao.
  Hivyo watanzania hivi sasa tunatakiwa kuchagua timu ya viongozi ambao watarudisha heshima ya nchi kwa kuwa na uongozi wenye kujali maslahi ya Taifa na siyo kujenga usultani.
  • Viongozi ambao wataheshimu wananchi na kulinda rasilimali za nchi.
  • Viongozi watakaokuwa tayari kuwajibika na kuwawajibisha wote watakaokiuka maadili ya uongozi na kuliingizia taifa hasara.
  • Viongozi watakaoheshimu haki na usawa wa raia wake
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  mkuu umenena,viongozi wa ccm wamekosa uzalendo,wezi,mafisadi,sio creative,hawana solution,hawajuiprioritie za maendeleo
   
 3. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Mkuu priority waliyonayo viongozi wetu ni kujineemesha wao na familia zao nyuma ya mgongo wa amani na utulivu wa nchi!
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Hivi hii nchi ina viongozi kweli.
   
 5. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwanza nianze kwa kuheshimu mawazo yako. Hoja yako yaweza kuwa sahihi, kwa sababu tu hitimisho - hitimisho ni sahihi. Hata hivyo, unashindwa kutofautisha kati ya dhana mbili "Utawala na Uongozi". Kwa ufupi utawala unaendana na mamlaka aliyopewa mtu ya kuendesha, kusimamia na kuiongoza taasisi au shirika kwa niaba yake au kikundi, watu, au serikali. Uongozi unaendana na uwakilishi, kwa mfano na ushawishi alionao mtu aliye katika nafasi ya kuongoza kwa kuchaguliwa, kuteuliwa, aliyeingia kiimla/mabavu. Hoja yako ni 'Uongozi Mbovu' usichanganye na utawala. Hata hivyo - pamoja ya kuwa sijasoma hoja ya Mwanakijiji - nakubaliana na hitimisho lake kuwa sera zetu ni mbovu. Lakini nikuunge mkono kuwa utawala na watawala wa Tanzania nao ni mbovu. Watawala wetu wameshindwa kutumia ipasavyo nguvu za kimamlaka walizopewa kwa manufaa ya taasisi, na serikali kwa ujumla. Nguvu hizo za kimamlaka wanatumia kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe, rafiki na ndugu zao. Uongozi na viongozi nao ni wabovu. Hatuwezi kujifunza toka kwao. Wananchi (wanaoongozwa na kutawaliwa) nao ni wabovu. Wananyamazia ubovu wa sera, utawala, watawala, na uongozi na viongozi. Mwisho, mfumo mzima ni mbovu. Jiangalie mwenyewe au jirani yako. Je, jinsi unavyoishi, unatuandalia kiongozi mzuri? Unashiriki kuondoa mfumo holela na hoehae wa nchi? Wakati ombwe la uongozi na kufeli kwa watawala kwajionesha dhahiri kwa suala la mgomo wa madaktari Muhimbili, ulichukua hatua gani? Matokeo ya kidato cha nne umeyaona- uwiii, kwani hilo ni matokeo ya shule za kata ambalo kabuli la elimu Tanzania.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Hallow nafikiri kuwa sera na utawala bora vinaenda parallel

  kuna wakati sera inatengeneza viongozi wazuri, mfano naamini kuwa sera ya majimbo ya chadema is the best one. why?

  ikiwa eneo husika litazalisha na kutumia rasilimali zake, basi lazima kutatokea leaders who are creative thinkers, mfano kwenye ukame kama singida lazima viongozi watafikiria wafanye nini ili washindane kipato na maeneo yenye rutuba kama Mbeya!

  Relaxation za viongozi wetu zinatokana na sera ambazo haziwabani kufikia target fulani, sisi si watu wa kuomba, kuhitaji msaada nje ya nchi

  leadership and policy are monozygous
   
 7. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naomba nichangie radically kwenye hii issue. Matumaini yangu ni kwamba mchango wangu utapimwa kwa vigezo vya uchambuzi wa busara na u makini. Pia nakirisijabahatika kuisoma hii article kwa hiyo mchango wangu umejikita kwenyemichango ya wenzangu humu.

  Sera vs Mikakati

  Sera hapa kwetu ni kitendawili kisichoteguka kwa sababu ya matumizi ya lugha (semantics) ya kujikanganya. Kunawatu wanatumia sera mahali pa mikakati na mikakati mahali pa sera. Kwa sababu wananchi hatujafunguka. Kauli za kisiasa kuhusu kwa mfano "sera yetu ya kuiba kura ina tija"wakiwa na maana ya mkakati wao wa kuiba kura una tija ni mfano dhahiri. Mfano mwingina Sera yetuya taifa ya Elimu ni kujenga madarasa na kuwa na shule za sekondari kila katawakimaanisha mkakati usio na msingi wa mwelekeo wala sera wa kujenga shule za kata.

  Ninachokisema hapa kama taifa tumejikita kwenye kauli za kupotosha kuhusu sera kwa sababu hatujatulia na kuchukua hatua shirikishi kuhusu mwelekeo wa taifa letu kwa kuwa na sera elekezi zinazotokana na maono au ndoto ya taifa tulitakalo kufikia muda fulani. Ushahidi ni kuwa tumekuwa tukijitawala toka 1961, hii ni awamu ya nne ya urais lakini kila rais anakuja na lake. La karibuni kabisa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA bila mwelekeo, mkakakati raslimali wala viashiria vya upimaji wa kulifikia hilo. Lakini si bahati mbaya ndivyo wanavyotaka watawala wetu wakati sisi wananchi tumebakia watazamaji.

  Hapa ndipo tuje swala la utawala bila sera, mikakati, usimamizi wenye viashiria na rasilimali. Jibu ni fupi hata wakija malaika hakuna tija bila kufuata misingi isiyoteteleka ya kujiongoza nakujitawala kwa kuwepo Dira, Sera, Mikakati na vipaumbele vya kuelekeza rasilimali.

  Tuna nini katika mstakabali wa sera na utawala?

  Tuna Vision 2025 iliyo na maudhui ya siasa za CCM na baadhi ya mambo ya kitaifa. Ni ya ki CCM kwa sababu hakuna ushahidi kuwa wananchi walishirikishwa na wakapimwa kuwa ni washiriki wa hili jambo.Vision katika lugha ya kawaida ni dira/dhamira ya matarajio ya kufikia mafanikio fulani baada ya muda fulani. Kwa maana nyingine Vision 2025 zaidi ni ya matarajio ya CCM iliyowaengua wananchi wengi kwa kutowashirikisha juu ya taifa walitakalo kufikia 2025.

  Baada ya hiyo vision ndipo kulitakiwe kuje sera za kitaifa kuhusu uchumi, huduma za kijamii, ulinzi na usalama, mahusiano na nchiza nje nk ambayo yanav uka mipaka ya itikadi za vyama. Lakini tuna kila aina ya sera mpaka sera ya uchaguzi kuhakikisha CCM inatawala daima.Mfano mzuri wa sera ya kitaifa ni sera ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu Israel. Hii inatekelezwa na chama cho chote kitakachoingia madarakani nchini Marekani kwa mikakati iliyowaweka madarakani. Je Sera ya CCM kuhusu elimu itawahi kuja kutekelezwa na chama kingine? Jibu ni hapana kwa sababu kwanza si ya kitaifa pili haina misingi ya kisera tatu ni ahadi tu ya wakati wakuomba kura si endelevu na mwisho haina viashiria vya kisayansi vya kuipima kama ina tija.

  Baada ya Sera hufuata Mikakati ambayo inabaini vipaumbele vya kuelekeza rasilimali zote zikliwemo watu na vipindi vya kuipima kwa viashiria vyenye sifa. Hapa ndipo watawala wetu wanajikoroga. Tuanze kwa sasa mikakati na rasilimali watu. Mawaziri na Makatibu wakuu na baadhi ya wakurugenzi nathubutu kusema kwa uhakika na mifano kuwa ni washikaji na waumini wa chama tawala zaidi wasio na sifa za kitaalamu. Hawa hata ukiwapa fedha kiasi gani hawata kuwa na vipaumbele vya kuwanufaisha wananchi na nchi nje ya kuinufaisha CCM.Kwa lugha nyepesi ni utawala mbovu.

  Hitimisho

  Hakuna budi kuwashirikisha wananchi katika kuota (Kuvison) mustakabali wao na taifa lao. Hili litafanikisha kutunga sera za kitaifa mikakati na programu zenye mwelekeo, vipaumbele na viashiria vya mafanikioya utekelezaji. Lakini kikubwa litaweka misingi madhubuti ya matumizi ya rasilimali hasa rasilimali watu. HILI HALIPO NA HALIJANZA.

  Ni matumaini yangu mchakato wa katiba mpya unaweza kutoa fursa ya kuanza hili. Kwa hiyo tatizo tulilo nalo ni kutekwa kwa mstakabali wa taifa na wanasiasa wa chama tawala wasio na dira wala mwelekeo.
   
 8. m

  mharakati JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mh wetu Edward N Lowassa atakua kiongozi wa watu
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mnaopewa mishahara na edo mnamatatizo kweli' acheni ubinafsi bwana mishahara mnayopewa ndo manataka muuze nchi bwana, toeni JIZI lenu hapa!
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli nakubaliana na mtoa hoja.

  lakin msingi mkubwa ni kuwa na katiba mpya. Katiba mpya ambayo:
  1. Inayoruhusu mgombea binafsi
  2. Inayomfanya kiongozi kama mbunge au rais kuwajibika kwa wananchi na sio chama cha kisiasa.

  Kwani watu siku zote wanamchagua mtu kutokana na utashi na uzalendo wake na sio chama chake.

  kila la kheir
   
 11. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Mimibaba

  Nimefurahia uchambuzi wako! Lakini kikubwa ambacho nadhani kama hatutakipiga vita kama Taifa ni tabia inayojengeka ya watu na hasa viongozi wetu kuwa wabinafsi na kutaka utajiri wa haraka haraka kwa kuwadhulumu wananchi wanyonge walio wengi. Hivyo hata tukishirikishwa katika kutengeneza vipaumbele vyetu na kuandaa mkakati bila kuwa na viongozi watakaojitolea kuwatumikia wananchi kwa moyo wa dhati na kwa huruma, hakuna matokeo mazuri ambayo tutatarajia!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Nami nakubaliana na wewe lakini angalizo ambalo ningependa kulitoa ni kuwa katika mchakato wa kuandaa katiba mpya watawala wetu wawaachie watu uhuru wa kutoa maoni yao kwa uwazi bila vitisho. Uzoefu uliopo ni kuwa huku Tanzania Bara wajumbe wa nyumba kumi hutumiwa na chama tawala kutoa vitisho kwa wananchi na hivyo kuishia kukubaliana na hoja za serikali.
   
 13. shadow recruit

  shadow recruit JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2013
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi inahitaji Shahada mbili za Uchumi kujua kuwa sera mbovu za chama tawala zimetufikisha hapa tulipo,sera mbovu ya elimu,sera mbovu katika kulinda rasilimali na sera mbovu za uwekezaji zinazolifanya taifa kuwa sehemu ya kuchota rasilimali za nchi...Tafakari Chukua hatua 2015.
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2013
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa sawa ila hakuna katika maumbile ya wanadamu kiongozi anayejitambua na kujitapa kuwa ni kiongozi. Kwa enzi za Adam Mungu ndiye alitamka viongozi kupitia mitume wake waliowaweka mafuta wafalme.

  Tumeendelea na Demokrasia, utaratibu mzuri ni ule wa waongozwa kumbaini na wanaetaka aongoze siyo kujitangaza. Halafu Katiba ni kitu cha msingi sana; katiba nzuri inazaa sheria nzuri na uongozi mzuri. Hii tuliyo nayo ni ya Kidikteta kwa mtu binafsi au kichama.

  Pamoja na mchakato mbovu kwa sababu misingi ya mabadiriko haukusimikwa kwa ridhaa, lakini ni fursa ambayo itazaa kitu fulani.
   
 15. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2013
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Hakuna sera nzuri toka kwa viongozi wabovu.
   
 16. A

  Asamwa JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2013
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 2,544
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri utendaji wa viongozi unategemea sana utendaji wa kiongozi wa juu yao.

  Kama kiongozi wa juu ni mtu makini na ambaye hataki utani katika kazi, itabidi viongozi wa chini yake waige utendaji wake, la sivyo wawe tayari kuwajibishwa.

  Nchi kama Ruwanda imepata maendeleo ya haraka kutokana utendaje usiotetereka wa Rais wao.
   
Loading...