Tatizo la Tanzania sio umaskini ni uongozi mbovu na kujali maslahi ya kujilimbikizia mali vigogo tu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la Tanzania sio umaskini ni uongozi mbovu na kujali maslahi ya kujilimbikizia mali vigogo tu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jul 19, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG][TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"] Pro! Ibrahim Lipumba Katibu mkuu wa Cuf


  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Kwa hili CUF mmenena


  Shehe Semtawa

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]HIVI karibuni Chama cha Wananchi (CUF) kilitoa taarifa yenye mambo mengi lakini nimeona niandike haya machache.
  Chama hicho kinasema kinyang’anyiro cha kupata mgombea urais mwaka 2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), huenda kikaiweka CCM pabaya.
  CUF ilibainisha hayo wakati baadhi ya viongozi walipokuwa wakizungumza na wanahabari kuhusu mpasuko wa kisiasa ndani ya chama hicho.
  Wanasema kinyang’anyiro hicho kimekuwa kikisababisha athari, kuyumbisha nchi na ustawi wa maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na makundi ya nani awe mgombea wa chama hicho mwaka 2015.
  Kwa mujibu wa CUF, ni jukumu la msingi la chama kinachounda serikali kutambua kuwa wananchi wake wanahitaji mabadiliko.
  Chama hicho na viongozi wake wanaamini wako tayari kuwaongoza Watanzania kuelekea katika mabadiliko ya kweli wanayoyataka.
  “CCM imeshindwa kuiongoza Tanzania na tujiandae kuishughulikia kikamilifu mwaka 2014/15 ili CUF iweze kuunda serikali makini itakayoweza kuweka mipango thabiti ya kiuchumi na maendeleo ya taifa letu,” alisikika mmoja wa viongozi akisema.
  Chama kinaitaka serikali kudhibiti utoaji wa takwimu holela ili kuepusha migogoro isiyo kuwa ya lazima ndani ya nchi.
  Kutokana na mvutano kati ya serikali na Waislamu, wanamtaka Rais Kikwete kukutana na viongozi wa dini zote kuwasikiliza hoja zao na kutafuta maridhiano kuhusu dodoso la dini katika sensa.
  Kinasema ikiwa sehamu ya jamii ikihamasishwa na kususiwa zoezi hilo lenye gharama kubwa na kutofanikiwa nchi itakuwa na takwimu zisizo sahihi.
  Pia kinasema si kweli kuwa chama hicho hakihitaji Muungano na wala haitakuwa rahisi kwa chama hicho kuvunja muungano huo pindi kitakapoingia madarakani.
  Chama kinaitaka serikali kuweka utaratibu mzuri wa mchakato wa matumizi ya rasilimali ili ziweze kuwanufaisha Watanzania wenyewe.
  Inaonesha kuwa nchi nyingi duniani zimeingia katika matatizo makubwa kutokana na ufisadi wa watu wachache kuhodhi rasilimali hizo kwa masilahi yao binafsi.
  Kuhusu suala la kumiliki ardhi, kinatoa wito kwa serikali kuwamilikisha Watanzania ardhi yao hasa ukizingatia kuna mchakato wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na wimbi la kutafuta na kupora ardhi linalofanywa na nchi zenye fedha.
  Mtazamo wangu katika hili, naweza kusema kwamba kuna ukweli ndani yake, hasa katika upande wa kuyumba nchi, ukiangalia baadhi ya viongozi wa CCM wamefikia hatua za kuchafuana wenyewe kwa wenyewe.
  Hali hiyo inadhihirishwa na kauli ambayo imetolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, pale alipopata nafasi ya kuwashughulikia wote wanaomchafua kwa kutumia nguvu ya fedha endapo tu atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.
  Vitendo kama hivyo, kwa kweli vimekuwa vikirudisha nyuma ari ya viongozi na kusababisha kushindwa kufanya vema kazi za jamii.
  Baadhi ya viongozi badala ya kushughulikia zaidi masuala ya jamii, huonekana kulinda vitendo viovu vinavyoshika kasi kila kukicha hapa nchini. Wanashughulikia zaidi mambo binafsi.
  Cha msingi, kwa kuwa CUF wamelibaini hilo, ni wakati wao pamoja na vyama vingine vya siasa nchini kujiimarisha kwa lengo la kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
  Watanzania huko mitaani wamekuwa wakisikika wakisema kuwa wamechoshwa na malumbano yasiyokwisha ya baadhi ya viongozi wa CCM, kwa kuacha kufanya kazi waliyotumwa na wananchi wao.
  Hata hivyo, wananchi wanapaswa kuonesha kweli kama wamechoshwa na serikali iliyopo madarakani kwa kuchukua hatua ya kujitokeza kwa wingi mwaka 2015 kwa kukichagua chama mbadala na si kulalamika mitaani tu.

  Tanzania Daima


  [​IMG]

  ssemtawa@yahoo.com 0719352268
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...