Tatizo la Tanzania ni uongozi na vipaumbele vyetu

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari wana jf poleni kwa ukosefu wa maji, umeme pamoja na jua kaliii

Moja kwa moja niende kwenye mada husika hapo

Pamoja na vyote ambavyo nchi yetu inapitia kwa sasa tatizo naona sio ukosefu wa fedha hapana bali tatizo lipo kwa viongozi wetu ambao tumewaweka madarakani pamoja na vipaumbele vyetu yani viongozi hawajui watanzania tunataka nini na kwa wakati gani

Naomba nianze kama hivi

1) VIONGOZI
- Hawa ndio wa kwanza kwa kutuhumiwa kutokana na upatikanaji mbovu wa huduma za kijamii Tanzania kama vile Afya, Maji safi na salama, Umeme wa uhakika, Barabara na Elimu bora.

KWANINI?

Viongozi wengi ni wapigaji na wapo madarakani na wapo madarakani wanajali matumbo yao na sio kuwatumikia watanzania na kujali maslahi ya watanzania.

Mfano
:-Mikataba mingapi ya hovyo na ya upigaji imesainiwa kama huu wa juzi wa TANESCO
:-Mitambo na bidhaa ngapi feki zimeingizwa Tanzania sababu tu viongozi watapata cha juu

Viongozi wengi waliopo madarakani hawana sifa za kuwa katika vyeo hivyo na matokeo yake husababisha utendaji kazi mbovu sababu hawajui nini wafanye katika nyadhifa hiyo.

Mfano
:-Mtu kasomea mambo ya fedha na uchumi halafu anapewa aongoze wizara ya michezo na bado tunamatarajio ya kwenda Qatar.
:-Mtu kasomea uhusiano wa kimataifa halafu anapewa wizara ya nishati na madini na tunategemea kusiwe na mgao wa umeme.

Viongozi kukosa washauri wazuri hapa naenda moja kwa moja kwa viongozi wa juu ambao wanafanya maamuzi ya mwisho hao viongozi hawashauriwi vizuri na wanadanganywa na wa chini yao.

Mfano
:-Mh Rais anadanganywa na January Makamba kuhusu ukame na mabwawa kukauka maji.
:-Mh Rais anadanganywa na Siro eti Mbowe ni gaidi

Viongozi wanafanya kazi kwa kufuata matakwa ya waliowateua na sio kwa niaba ya waliowachagua na kuwapigia kura hii yote ni kwa kuogopa kutenguliwa

Viongozi wengi hawana msimamo hapa naenda moja kwa moja kwa waziri wa Afya enzi ya Magufuli alisema vingine na sasa hivi kabadilika anasema mengine.

:-Hapa natoa kongole kwa Faustine Ndungulile yeye tangu enzi za Magufuli msimamo wake ulikuwa ni ule ule

2)VIPAUMBELE VYETU

Hapa ndio kwenye mtiti sasa ukiwauliza watanzania 10 vipaumbele vya Tanzania kwa miaka 5 ijayo ni vipi hawajui.

Nchi yetu imekuwa imeweka vipaumbele kwenye mambo ambayo hayana faida ya moja kwa moja kwa watanzania

MFANO

VIPAUMBELE VYA SERIKAKI 2020/2021
"Ujenzi wa Reli ya Kati ya Standard Gauge
Serikali imetenge Sh. trilioni 2.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300); kuendelea na ujenzi wa kipande cha Morogoro – Makutopora (km 422); kuendelea na taratibu za upatikananaji wa mkandarasi kwa vipande vya Makutopora – Tabora (km 376.5).

Pia Tabora – Isaka (km 162) na Isaka – Mwanza (km 311.3); kuendelea na taratibu za upatikanaji wa washauri elekezi na utoaji wa ardhi kwa vipande vya Tabora – Kigoma (km 411), Kaliua – Mpanda – Karema (km 320), Uvinza – Msongati (km 240) na Isaka – Rusumo (km 371).

Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115
Kwenye mradi huu, kazi zitakayofanyika ni kuendelea na ujenzi wa bwawa; ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji; ujenzi wa eneo la kufunga mitambo ya kufua umeme; na ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme ambapo shilingi trilioni 1.44 fedha za ndani zimetengwa.

Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania
Sh. 450 bilioni 450, fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kununua ndege moja ya mizigo na moja ya abiria aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, kukamilisha malipo ya ndege mbili aina ya Airbus A220–300, kununua vifaa vya kuhudumia ndege na abiria viwanjani, kulipa madeni ya Shirika na kukarabati Hangar za KIMAFA (KIA) na JNIA.

Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma
Shughuli zilizopangwa kwenye mradi huu ni kuhakiki mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja na uperembaji na tathmini ya mradi ambapo Sh. 110 milioni, fedha za ndani zimetengwa.

Kiwanda cha kufua chuma cha Liganga
Shughuli zilizopangwa ni kuhakiki mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja na uperembaji na tathmini ya mradi ambapo Sh. 120 milioni, fedha za ndani zimetengwa.

Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania)
Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha majadiliano ya mikataba ikiwemo ya Nchi Hodhi na Wawekezaji, mkataba wa ubia, mkataba wa bandari, mkataba wa pango la ardhi na kulipa fidia ambapo shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia – Lindi
Kwenye mradi huu, shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na tafiti mbalimbali za kitaalam pamoja na majadiliano ya mradi. Sh. 2.6 bilioni, fedha za ndani zimetengwa.

Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi
Jumla ya Sh 5 bilioni, fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya uendelezaji wa kanda maalum za kiuchumi. Shughuli zitakazotekelezwa ni:

Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo:
kukamilisha uandaaji wa nyaraka za kisheria kwa ajili ya mradi; kukamilisha taratibu za umilikishaji ardhi katika eneo lililolipiwa fidia; kufanya usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu wezeshi katika eneo la kituo cha Teknolojia Bagamoyo; kujenga barabara katika eneo lililojengwa viwanda 11, ambapo shilingi bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa.

Eneo Maalum la Uwekezaji la Ukanda Huru wa Bandari ya Mtwara:
kujenga jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma na uzio ambapo shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.
Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini: shilingi bilioni 2.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi watatu ambao awali nyumba zao hazikufanyiwa thamini; kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuliendeleza eneo na tathmini ya athari za kijamii na mazingira.
Shamba la miwa na Kiwanda cha Sukari Mkulazi (I na II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Mkulazi I – kuendelea na upanuzi wa kitalu cha miwa kufikia hekta 250 na maandalizi ya ujenzi wa kiwanda; Mkulazi II – kuzalisha tani 2,300 za sukari; kuendelea na ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji, vyanzo vya maji na barabara katika eneo la shamba; na ujenzi wa mabwawa madogo sita (6) yenye mita za ujazo 250,000 na makubwa matatu (3) yenye mita za ujazo 1,000,000.

Kusomesha kwa wingi wataalam kwenye Fani na Ujuzi Adimu
Kuendelea kugharamia mafunzo kwa wanafunzi katika fani mbalimbali zinazohitajika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya viwanda na watu nchini.

Fani hizo ni pamoja na mafuta na gesi, afya hususan udaktari bingwa kwa ngazi za uzamili na uzamivu katika nyanja zote za magonjwa ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, upandikizaji figo, ini na uboho (bone marrow), tiba za ndani za moyo, na uhudumiaji wa wagonjwa wa dharura na mahututi."

Cha kujiuliza je hapo kuna kitu chochote ambacho kitamnufaisha mtanzania ambaye yupo huko kijijini?

Je, vipaumbele na miradi ambayo tunaitekeleza je inafuata master plan za eneo husika au tunaenda enda tu?

Hadi sasa vipaumbele vya MAMA sijavijua bado labda mnijuze nyie.
 
Back
Top Bottom