Tatizo la Tanzania ni CCM siyo Watanzania!

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Hii mada ni ya kisiasa ingawa nimeitoa bila ya kuwa na msukumo wa kisiasa bali kwa kufuata dhamira yangu ya kuitaka Tanzania njema huko tuendako. Ni uzalendo wangu tu ndiyo umenisukuma kuandika hiki ninachoandika. Kama kuna mtanzania anaona tumekwama basi ajue kwamba kukwama kwetu kunatokana na CCM kuwepo madarakani ama laana inayoiandama CCM kwa jinsi inavyoingia madarakani!

Wazazi wa CCM,TANU na ASP ni vyama vilivyojengwa katika misingi ya kupigania uhuru na haki za Mwafrika lakini baadaye vikageuka kuwa kandamizi kwa uhuru na Haki za waafrika wenzao. Tabia hiyo ndiyo iliifanya TANU ifute kwa hila vyama vingine vya siasa hapo mwaka 1965 na ASP kukaa madarakani kwa miaka zaidi ya 16 bila ya kufanya Uchaguzi hata wa kuigiza huko Zanzibar.

Tabia ya viongozi wa CCM na wanachama wao kutokupenda kupingwa inatokana na Uasili wa chama hicho. Kamata kamata, kupenda kuonesha ukuu wa chama (Party Supremacy) chao ni mambo ambayo CCM haitaacha kuyafanya mpaka ilazimishwe kuacha. Hata mfumo wa vyama vingi uliporudi, CCM haikusajiliwa bali ilijisajili na kujipa upendeleo wa kuwa chama cha kwanza kuwepo kwenye mfumo wa vyama vingi.

Nchi hii haijawahi kutawaliwa na chama kingine chochote cha siasa zaidi ya CCM.Kwa hiyo kama kuna wapiga Dili, kama kuna Elimu duni, Huduma za Afya zisizokidhi vigezo, Kama sehemu kubwa ya Ardhi yetu haijapimwa, kama kuna ujenzi holela mijini na vijijini, kama kuna jambo lolote unaloliona ni tatizo kwenye jamii yetu watanzania basi ujue chanzo chake ni CCM.

Sheria mbovu na kandamizi zoote zimepitishwa ama kuridhiwa na CCM. Kama kuna udhaifu wa Mahakama zetu jua chanzo chake ni sheria zilizotungwa na CCM, kama serikali ni onezi jua inatokana na mfumo unaolelewa na CCM kwa faida ya chama hicho. Hakuna namna kama watanzania tunataka kuibadili Tanzania yetu ni lazima kwanza tuiondoe CCM madarakani. Tuachane na wale watu ambao kila mara wanatuaminisha kwamba bado CCM kuna watu "wema" na "Bora" kuliko Upinzani, lakini baadaye tena hujiunga na sisi kulalamikia wale wale waliotuminisha kwamba ni Bora na ni watu wema!

Tatizo la Tanzania ni CCM na Tatizo la CCM ni CCM yenyewe!!
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,143
2,000
Hizo ni sababu nyepesi mno mwenye uwezo wa kuchanganua mambo hawezi kukubaliana na wewe.
CCM haijajiweka,imewekwa na wapiga na wapiga kura.
Kama kuna upinzani dhaifu na usio makini CCM itatawala milele
Mnafanya utani na wapiga kura halafu unailaumu CCM?
 
Nani kailamu CCM? Hapa nimetoa ufafanuzi wa hali ya mambo ilivyo na chanzo chake!! Kwani Uchaguzi wa Zanzibar CCM ilishinda?
 
Konsciouz

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,823
2,000
Tatizo sio CCM tatizo ni elimu, elimu, elimu.
Wakazi kama wa idodomiya, singida, songea huko, mwanza, shy, nk wangekua wamelimika huu upuuzi uitwao CCM ungekua umesahaulika.
 
Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
Hizo ni sababu nyepesi mno mwenye uwezo wa kuchanganua mambo hawezi kukubaliana na wewe.
CCM haijajiweka,imewekwa na wapiga na wapiga kura.
Kama kuna upinzani dhaifu na usio makini CCM itatawala milele
Mnafanya utani na wapiga kura halafu unailaumu CCM?
Tatizo ni watanzania....Na watanzania wako hivi walivyo kwa sababu wamenyimwa elimu na utawala wa CCM...Mfumo wa elimu umewaharibu watanzania wamekuwa sio self reliant....hawajui kutafuta haki yao.

Kwa sababu ya ujinga huu wa watanzania ndio maana wameendelea kurudia makosa yaleyale miaka nenda rudi

Tatizo lingine ni katiba mbovu tuliyonayo...Kwa katiba hii na mfumo wa uchaguzi tulionao hakuna mtawala ambaye angekubali kukaa pembeni...katiba inamlinda sana mtawala...Yaani CCM kukaa pembeni kwa katiba hii tuliyonayo ni labda iwe na Upendo wa Zaidi ya Upendo wa Yesu.

Opposition wamefanya kazi kubwa sana katika mazingira magumu sana.....Hadi leo hii Opposition wako hii sio jambo limekuja tu au limejitengeneza tu

Kwa manufaa mapana ya taifa....Tunapaswa kurekebisha katiba yetu katika maeneo mengi kama yalivyoainishwa na katiba ya warioba

Ni ukweli usio na shaka failures zote tulizonazo sasa ni matokeo ya inefficiency ya serikali ya CCM kwa maiak yote zaidi ya 50
 
Wamunzengo

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
810
250
Siku utakapojua kuwa Tanzania ni nchi huru, ndio siku Tanzania itapata uhuru kichwani mwako.
 
Aaaaaaa

Member
Dec 9, 2016
39
95
Well say mkuu ila tatazo hakuna chama mbadala ya hicho kwa mtanzania mwelevu na mwenye upeo ukiangalia vyama vyote vya siasa achilia mbali hicho ulicho kitaja hakuna ambacho kinaaminika mbele ya watanzania ni kweli watanzania wanapenda mabadiliko ila vyama pinzani havina mifumo ambayo inaonyesha viko tayari kuwavusha watanzania kutoa sehemu moja kwenda nyingine
 
Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,509
2,000
Siku utakapojua kuwa Tanzania ni nchi huru, ndio siku Tanzania itapata uhuru kichwani mwako.
Tafsiri ya uhuru kwako ikoje. Mwalimu aliposema "Tanzania haiwezi kuwa huru mpaka Afrika nzima imekuwa huru" alikuwa hajui kama Tanganyika ilipata Uhuru wake mwaka 1961 na Zanzibar mwaka 1963?
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,143
2,000
Tatizo ni watanzania....Na watanzania wako hivi walivyo kwa sababu wamenyimwa elimu na utawala wa CCM...Mfumo wa elimu umewaharibu watanzania wamekuwa sio self reliant....hawajui kutafuta haki yao.

Kwa sababu ya ujinga huu wa watanzania ndio maana wameendelea kurudia makosa yaleyale miaka nenda rudi

Tatizo lingine ni katiba mbovu tuliyonayo...Kwa katiba hii na mfumo wa uchaguzi tulionao hakuna mtawala ambaye angekubali kukaa pembeni...katiba inamlinda sana mtawala...Yaani CCM kukaa pembeni kwa katiba hii tuliyonayo ni labda iwe na Upendo wa Zaidi ya Upendo wa Yesu.

Opposition wamefanya kazi kubwa sana katika mazingira magumu sana.....Hadi leo hii Opposition wako hii sio jambo limekuja tu au limejitengeneza tu

Kwa manufaa mapana ya taifa....Tunapaswa kurekebisha katiba yetu katika maeneo mengi kama yalivyoainishwa na katiba ya warioba

Ni ukweli usio na shaka failures zote tulizonazo sasa ni matokeo ya inefficiency ya serikali ya CCM kwa maiak yote zaidi ya 50
Hakuna opposition Tanzania kuna wasanii.Pamoja na kuwatukana watanzania,lakini bado ni watu wenye uwezo wa kujua pumba na mchele.Huwezi kuing'oa CCM kwa mipango ya dharura kwa kubadili gia angani
 
Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
Hakuna opposition Tanzania kuna wasanii.Pamoja na kuwatukana watanzania,lakini bado ni watu wenye uwezo wa kujua pumba na mchele.Huwezi kuing'oa CCM kwa mipango ya dharura kwa kubadili gia angani
again ...wewe ni zao la miaka 50 ya CCM....
 
Konsciouz

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,823
2,000
Konsciouz na Freeland maelezo yenu ni mazuri sana. Lakini ni kweli kwamba CCM imedekezwa na watanzania lakini ukweli mwingine ni kwamba kudekezwa huko kwa CCM na watanzania kunatokana na CCM kuweka mfumo wa kudekezwa!!
Yeah upo Sahihi... Tukianzia kwenye elimu na maneno mengine ya hofu ambayo CCM imekua ikiwajengea raia.
Mfano mtu anawadanganya watu eti kuchagua upinzani kutaleta vita. Sasa Watz wengi walivyokua hawawezi kuchanganya akili za kuambiwa na zao. Pia wachovu kwenye kupambanua mambo wanagwaya na kuwarudisha hawa mapimbi magogoni.
 
Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,856
2,000
Hii mada ni ya kisiasa ingawa nimeitoa bila ya kuwa na msukumo wa kisiasa bali kwa kufuata dhamira yangu ya kuitaka Tanzania njema huko tuendako. Ni uzalendo wangu tu ndiyo umenisukuma kuandika hiki ninachoandika. Kama kuna mtanzania anaona tumekwama basi ajue kwamba kukwama kwetu kunatokana na CCM kuwepo madarakani ama laana inayoiandama CCM kwa jinsi inavyoingia madarakani!

Wazazi wa CCM,TANU na ASP ni vyama vilivyojengwa katika misingi ya kupigania uhuru na haki za Mwafrika lakini baadaye vikageuka kuwa kandamizi kwa uhuru na Haki za waafrika wenzao. Tabia hiyo ndiyo iliifanya TANU ifute kwa hila vyama vingine vya siasa hapo mwaka 1965 na ASP kukaa madarakani kwa miaka zaidi ya 16 bila ya kufanya Uchaguzi hata wa kuigiza huko Zanzibar.

Tabia ya viongozi wa CCM na wanachama wao kutokupenda kupingwa inatokana na Uasili wa chama hicho. Kamata kamata, kupenda kuonesha ukuu wa chama (Party Supremacy) chao ni mambo ambayo CCM haitaacha kuyafanya mpaka ilazimishwe kuacha. Hata mfumo wa vyama vingi uliporudi, CCM haikusajiliwa bali ilijisajili na kujipa upendeleo wa kuwa chama cha kwanza kuwepo kwenye mfumo wa vyama vingi.

Nchi hii haijawahi kutawaliwa na chama kingine chochote cha siasa zaidi ya CCM.Kwa hiyo kama kuna wapiga Dili, kama kuna Elimu duni, Huduma za Afya zisizokidhi vigezo, Kama sehemu kubwa ya Ardhi yetu haijapimwa, kama kuna ujenzi holela mijini na vijijini, kama kuna jambo lolote unaloliona ni tatizo kwenye jamii yetu watanzania basi ujue chanzo chake ni CCM.

Sheria mbovu na kandamizi zoote zimepitishwa ama kuridhiwa na CCM. Kama kuna udhaifu wa Mahakama zetu jua chanzo chake ni sheria zilizotungwa na CCM, kama serikali ni onezi jua inatokana na mfumo unaolelewa na CCM kwa faida ya chama hicho. Hakuna namna kama watanzania tunataka kuibadili Tanzania yetu ni lazima kwanza tuiondoe CCM madarakani. Tuachane na wale watu ambao kila mara wanatuaminisha kwamba bado CCM kuna watu "wema" na "Bora" kuliko Upinzani, lakini baadaye tena hujiunga na sisi kulalamikia wale wale waliotuminisha kwamba ni Bora na ni watu wema!

Tatizo la Tanzania ni CCM na Tatizo la CCM ni CCM yenyewe!!
Sababu za kijinga, kipumbavu na kilofa kuwahi kutolewa na "Kinacholewea"!!
 
Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
5,682
2,000
Hizo ni sababu nyepesi mno mwenye uwezo wa kuchanganua mambo hawezi kukubaliana na wewe.
CCM haijajiweka,imewekwa na wapiga na wapiga kura.
Kama kuna upinzani dhaifu na usio makini CCM itatawala milele
Mnafanya utani na wapiga kura halafu unailaumu CCM?
Uchague mwenyewe mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, utengeneze wewe makaratasi ya kupigia kura na box zake, uyalinde wew, kura zipigwe uzilinde wewe, matokeo asome huyu mwenyekiti wako na hakuna kuyapinga afu washinde wapinzani????
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,324
2,000
Nani kailamu CCM? Hapa nimetoa ufafanuzi wa hali ya mambo ilivyo na chanzo chake!! Kwani Uchaguzi wa Zanzibar CCM ilishinda?
Haikushinda, lakini Hatuwezi Kuvunja Umoja,mshikamano Na Muungano Kwa Tamaa Za Urais Za Mtu Mmoja - Ni Ushetani Uliotukuka
 
mbwea

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
250
500
Halmashauri mnazoongoza wapinzani bure kabsaa alaf mnataka nchi... Sina imani na mtu alyeshindwa sehemu ndogo kma atafanikiwa kokote
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom