Tatizo la Network kwenye ki-simu changu

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
16,239
7,603
Habari zenu wakuu, Nina Nokia E51 huwa natumia kwa Internet na huwa natumia kwa laini ya Airtel. Sasa juzi wakati natumia ghafla mnara wa network ukapotea wote kwenye simu kukawa peupe hakuna mnara, nikajaribu kusearch network lakini ilikataa kabisa.

Nikajaribu kuweka laini ya tigo ikakubali vizuri, baada ya kuangaika sana nikakujua kuwa simu yangu inazingua laini za Airtel tu maana nilijaribu na laini nyingine ya pia inazingua japo sasa mnara unapanda, lakini ili uweze kutumia vizuri basi lazima kule kwenye Network mode uweke GSM lakini ukiweka Dual mode au UMTS network inazingua hupigi wala hupigiwi na hiyo GSM inakuwa network mbaya kwa Internet.

Je, kuna njia ya kutatua tatizo hili wakuu?
 
Maybe network ya 3g ya airtel imepotea eneo lako. Hamna mwenye airtel ambae simu yake nayo ina 3g?
 
Back
Top Bottom