Tatizo la nchi ya Tanzania ni kukosa katiba mpya

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
✳️NAOMBA NISAIDIENI KUMWAMBIA MAMA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, TATIZO LA NCHI HII NI NINI❓

🔵Na:Shujaa Charles Richard Mwaisemba(©️®️Ⓜ️)


Kama ningelipata nafasi ya kukutana na Rais wangu Samia Suluhu Hassan, ningelimwambia ajue hasa Tatizo la nchi hii ya Tanzania ni Nini? Ila nafasi hiyo sina na hata ningepata nafasi hiyo bado kwa sauti yangu pekee asingelinisikia wala kunielewa kwa urahisi maana ni sauti ndogo sana, ndio maana nimetokea kwako, kukuomba mnisaidie kupaza sauti iwe kubwa zaidi kumwambia Mama Samia ajue, ni nini Tatizo la Nchi hii ?Tumwambie kwa upendo ,kwa upole kwa kumshauri na kumuelekeza wala si kwa vita wala ugomvi wala vurugu au maandamano yasiyo rasmi ili tupate muafaka wa kutaifa , kwani yeye(Rais) ni mama, anajua malezi na anasikiliza watoto wanasema nini?

1️⃣Tatizo la nchi hii SI KUWA NA CHAMA KIZURI CHA SIASA ili kuifanya Tanzania iwe na maendeleo ya kudumu

Tangu tupate uhuru wa nchi yetu kutoka kwa wakoloni uliotokana na Vyama viwili vya siasa TANU na ASP ambao ulipelekea kuundwa kwa chama kimoja chenye nguvu ,Chama cha Mapinduzi(CCM) mwaka 1977, ambacho kimeweza kudumu mpaka leo madarakani, na kuziwezesha nchi nyingi za Afrika kupata uhuru wao lakini pamoja na umahiri na ukongwe wa chama hicho bado Chama hicho Cha CCM chini ya katiba iliyoundwa tangu huo mwaka 1977 lakini bado hakijaweza kuondoa Tatizo kubwa lililopo Tanzania ya Sasa

Hata baadae vilipoanza mfumo wa vyama vingi na kuleta changamoto kwa chama tawala cha CCM bado hata hivyo vyama vingi vya siasa vilivyoundwa mwaka 1992 bado havijaweza kuondoa Tatizo la mkwamo wa kimaendeleo wa nchi yetu ya Tanzania

2️⃣Tatizo la nchi hii SI KUTOKUWEPO KWA SERA NZURI KUTOKA KWA VYAMA VYA SIASA CHINI VIONGOZI WAO WAKUBWA

Tangu wakati wa Baba wa Taifa,Mwl Julias Kambalage Nyerere aliyekuwepo na Sera nzuri ya Ujamaa lakini bado haikuweza kuwatoa watanzania kwenye Tatizo tulilonalo, Akaja Rais Mwinyi aliyekuja na Sera nzuri ya Kuruhusu Soko huria(Biashara za watu binafsi) aliyejulikana kama Bwana Fuksa lakini bado sera hizo hazikufua dafu, Akaja Mzee wetu Rais Benjamin Mkapa ambae nae akaja na sera nzuri za kuongeza nafasi za sekta binafsi na kufanya ubinafsishaji wa mashirika ya umma lakini bado hatukufika pale palipokusudiwa

Hatimaye akaja Rais Jakaya mrisho kikwete ambae naye aliweka sera yake ya Kilimo kwanza kama ndio shabaha ya kutukwamua lakini bado ufisadi ndio uliongezeka.Na hatimaye akaja aliyekuwa Rais wetu John Pombe magufuli ambaye nae alikuja na Sera ya Tanzania ya viwanda kama kipaumbele chake lakini bado hata hilo halijaweza kutukwamua kutoka kwenye tatizo tulilo nalo. Hivyo pamoja na uzuri wa sera zilizokuwepo lakini Sera nzuri hazijaweza bado kutukwamua hapa tulipo

3️⃣ Tatizo la nchi hii SI KUKOSA VIONGOZI WAZURI WENYE UWEZO MKUBWA WA KIUONGOZI

Katika awamu zote 5 zilizotangulia,Tanzania imefanikiwa kuwa marais wote wazuri tena wenye radha tofauti tofauti za kiuongozi, wakali, wapole, makatili, wachangamfu, wavumilivu n.k ingawa wanazidiana uwezo

Tulianza kuwa na Rais bora na mzuri ambaye anakumbukwa mpaka leo si kwasababu ndio alikuwa Baba wa Taifa ila ni kwasababu ya uwezo wake mzuri na mkubwa wa kiungozi na hekima kubwa aliyokuwa nayo,Lakini pamoja na yote hayakuifanya Tanzania kutoka katika mkwamo bali siku baada ya siku bado hata thamani ya pesa yetu ilizidi kupungua

Hatimaye walifuata waliofuata kama tulivyowataka yaana mwinyi,mkapa na hata wakati wa Kikwete,pamoja ufisadi uliongezeka ,lakini akaja Rais Magufuli pamoja na kudhibiti mianya ya ufisadi na rushwa bado watu waliendelea kulia Vyuma vimekaza si matajiri mpaka maskini.

Ubora wowote tunaoweza kuusema au kuutaja wa kiongozi yeyote bado hata kama ulifanikisha kwa kiwango fulani lakini baada ya miaka yake kuisha, maisha yalirudi nyuma zaidi au hali ilizidi kuwa mbaya zaidi ya aliyetangulia na hata yule tuliyedhani ndiye atakayetuvusha kutokana na ubora wake lakini bado hatujaweza kupata ufumbuzi wa tatizo tulilo nalo
1650709239516.jpg

Hivyo naomba Nisaidieni kumwambia mama samia, ajifunze kwa waliomtangulia kuwa hata angejitahidi yeye kuwa bora zaidi ya waliomtangulia bado hilo halitaleta ufumbuzi wa tatizo, hata akijitahidi kuja na sera nzuri za kimaendeleo leo, atakuja mwingine baada yake atayaacha yote aliyoyaanzisha na atakuja na mengine yake na hivyo Tanzania itabaki pale pale haitaendelea.Hata kama angetoka Rais kutoka kwenye Chama chochote kizuri cha siasa bado hali ya tatizo halitabadilika kabisa....

Hivyo, Mwambieni Mama Samia, Tatizo sio Kupata Rais Bora, hata Angekuja Rais wa marekani ndio akawa Rais wa Tanzania, bado Tanzania haitatoka kwenye Tatizo tulilo nalo, Au Tatizo sio kupata chama gani bora zaidi kinachoweza kutuongoza kwa haki na amani na uhuru.Pia mwambieni tatizo sio kuwa na sera nzuri kwa kiwango gani?

Ndugu zangu watanzania,Naomba nisaidieni Kumwambia Mama Samia, TATIZO KUBWA LA NCHI HII NI KUKOSA KATIBA MPYA INAYOENDANA NA MAZINGIRA YA SASA, ITAKAYOWEZA KUONYESHA DIRA YA MAENDELEO KWA MIAKA HATA 50 IJAYO

Endeleeni kuongeza sauti ya kumwambia mama kuwa, BILA KATIBA MPYA BADO TUTAENDELEA KUWA KATIKA MKWAMO HUU TULIO NAO SASA.

Ebu tumwambie mama Samia kuwa KATIBA MPYA ndio itatengeneza Sheria nzuri za kumpata huyo Rais bora hata kama akiwa mbovu kwasababu tu muongozo wa katiba nzuri basi itamfanya na kumuongoza kuwa mtu mzuri

Bado Tumwambie mama samia kuwa KATIBA MPYA Ndio itatoa Dira na Miongozo ya Tanzania yetu ya kesho na kesho kutwa iweje?.Tumwambia bila uwoga kuwa Katiba Mpya ndio itaongoza Viongozi wote wanafuata kutengeneza sera zinazoendana na muongozo wa katiba mpya itakayotengenezwa.Sio kila Rais anakuja na sera zake na mipango yake bila kuwa na sera za kitaifa za Miaka hata 50 ijayo ambayo itakuwa imeainishwa kwenye sheria zetu au mipango yetu ya kitaifa...

Naomba tusaidiane kuwambia Mama Samia Kuwa KATIBA MPYA ndio itatuamulia elimu yetu iwe ya mfumo gani?, Katiba mpya ndio itatuamulia tuwe na mfumo upi wa kiuongozi? KATIBA MPYA ndiyo itakayotoa miongozo mizuri tujue tunafanyaje biashara zetu za ndani na nje na kwa utaratibu upi?


Naomba tumwambie mama kwa kutumia haki yetu ya Kikatiba bila vurugu au machafuko kuwa KUKOSEKANA KWA KATIBA MPYA, Ndio kunapelekea kutengeneza mianya ya rushwa na kukosekana udhibiti wa bei za bidhaa, ndio unasababisha kukosekana na uwajibikaji na uwajibishaji kwa viongozi wa umma .Kukosekana kwa Katiba Mpya ndio kunafanya kukosekana kwa maadili kwa watumishi wa umma, Kunafanya kuwepo na mianya mikubwa ya Rushwa na ufisadi.

Tumalizie Kumwambia Mama samia Kuwa, Kukosekana kwa KATIBA MPYA kutasababisha hatari kubwa baadae ikiwa atakuja kuingia Rais kichaa ambaye ikiwa atatumia mamlaka yake ya kikatiba iliyopo sasa, basi anaweza akafanya uharibifu mkubwa na hata kufanya mauaji na asiwepo wa kumuhoji?Anaweza hata akawageuka hata ninyi ambao mpo nae kwenye chake leo

Tumwambie Mama Samia kuwa, Kukosekana kwa Katiba mpya kuna Mfanya Rais kuwa na mamlaka kubwa na anabebeshwa mizigo mikubwa ya kuamua kila kitu na mstakabadhi wa kila jambo katika nchi hii ambayo ingeweza kufanywa na mamlaka nyinginezo bila kuingiliana

Nchi yeyote haiwezi kufanikiwa na kuwa na mandeleo yanayoonekana bila kuwa na mfumo mzuri wa kikatiba na kisheria unaoongoza kila mmoja na unaoweza kumuwajibisha kila mmoja pale anapokosea bila kuangalia cheo au nafasi yake....

🔛TATIZO LA NCHI YA TANZANIA NI KUKOSA KATIBA MPYA...


Naomba Tupaze Sauti zetu pamoja na Mimi Tumwambie Mama Samia, TUNAOMBA KATIBA MPYA WALA TUSISUBIRI 2025!!!

#tusisubiri2025

🔵Na: Shujaa©️®️Ⓜ️
 
Katiba iliyopo ina ufanisi kiasi gani kwa mfano tu utaratibu wa polisi kumkamata raia unazingatiwa kiasi gani

Nadhani tatizo la nchi hii ni raia kutokuwa na elimu ya uraia na tutojua umuhimu ya siasa za nchi katika maisha ya kila siku
 
Back
Top Bottom