Tatizo la nchi ni kudhani kila mmoja anajua

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
watanzania tunahitaji kutatua changamoto zinazotukabili na ili tuweze kuzitatua tunahitaji kupita njia sahihi hasa kwa kuanzia na kuchagua viongozi sahihi.

tutawajuaje viongozi sahihi huo ndio mtihani mkubwa unaotukabili kwa sasa kwani kutokkana na changamoto zinazotukabili tunashuhudia kwa sasa kila mtanzania akijifanya anajua suluhisho la matatizo yetu.

hii ni sawa na masikini anayesumbuliwa na umasikini watamjia wengi wakijifanya wote kila mmoja ana suluhisho la umasikini wake.

wapo watakaokuja na kudai masikini huyu ana mikosi hivyo ili kutoka katika umasikini anahitaji kuondolewa mikosi kwa njia yoyote ile.

wapo watakaodai mtu huyu anahitaji kiungo cha mlemavu wa ngozi ili kufungulia ATM za kipato kwake.

wapo watakaodai mtu huyu anahitaji kufanya kazi kwa kumueleza ni kazi gani anaweza kufanya

wapo watakaodai tatizo si kufanya kazi bali tatizo ni kuibiwa haki hivyo wakapendekeza kuajiri walinzi wa kulinda mali zisiibiwe.

ilimradi kila mmoja anatoa suluhisho kulingana na upeo wake.


ni lazima tutambue kuwa changamoto za maisha yetu haziwezi kuwa na majibu kumi kwa kila moja bali katika mambo kumi unayoambiwa lipo moja ni suluhisho na mengine ni upotoshaji.

jambo la pili la kutambu ni kuwa changamoto za maisha hazina majibu mepesi ya kila mtu kusema hili huyu akasema lile na yote mkadhani ni majibu.

lakini ni jambo lililo bora kusikiliza kila mmoja anasema nini na kuwa na maarifa ya kubaini nani anatoa suluhisho la matatizo yetu.

tunahitaji kujua kuwa kuchagua viongozi katika uchaguzi unaokuja ni kuchagua suluhisho la matatizo yetu.

hapa ni tofauti na ushabiki wa mpira maana kwenye mpira kama hujanunua hisa bali unashangilia tu basi hata timu yako ikiwa mbovu kiasi gani utaishabikia tu maana ushabiki hauna hasara za kipato.

kwa uchaguzi ni mambo tofauti kwa maana kuchagua viongozi ni sawa na kuchagua mwajiri.

siku zote chagua mwajiri ambaye unaona kwake unapata maslahi makubwa zaidi na hiyo ndio kanuni inayostahili kutumika katika uchaguzi wa viongozi kwa maana viongozi ni "indirect employer"
 
Back
Top Bottom