Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,200
4,991
UKOJOZI KITANDANI (Bed-Wetting) –Enuresis

2318828_Kakojoa.jpg


Ukojozi kitandani unaweza kusababisha matatizo ya kitabia kwa sababu mtoto anaweza kuhisi ana makosa na kujisikia aibu. Ni kweli kwamba mwanao anatakiwa kuwajibika kwa kitendo hicho cha kukojoa kitandani (hii ina maana mwanao anatakiwa kufanya usafi). Lakini usimfanye mwanao ahisi kwamba yeye ndio mwenye makosa.Ni muhimu kwa mwanao kujua kwamba ukojozi kitandani siyo kosa lake. Kitendo cha kumuadhibu mwanao kwa kosa la kukojoa kitandani haitasaidia kutatua tatizo.

Itamsaidia mwanao kujua kwamba hakuna anayejua sababu kubwa inayopelekea ukojozi kitandani.Muelimishe kwamba mambo hayo hutokea katika familia (Kwa mfano, kama mwanao akikojoa kitandani, unatakiwa kujadiliana naye na kumhaidi kumsaidia kupambana na hali hiyo).

Msisitizie mwanao kwamba anatakiwa aende msalani wakati wa usiku. Muwekee taa kuelekea msalani ili imuwie rahisi kuona njia ya kuelekea msalani. Unaweza pia kumfunika na blanketi pamoja na tandiko lingine la plastiki ili iwe rahisi zaidi wakati wa kufanya usafi.Endapo mwanao atajaribu kukusaidia, msifie kwa kujaribu na kwa kusaidia kufanya usafi.

Nini maana ya Enuresis?
Enuresis ni neno la kitaalamu linalomaanisha hali ya kutoa mkojo bila ridhaa ya muhusika (involuntary), aina mojawapo tuliyoizoea ni ukojozi kitandani wakati mtu akiwa amelala hasa wakati wa usiku.

Ukojozi kitandani
Huwapata zaidi watoto na mara nyingi ni hali ya kawaida tu katika ukuaji wao. Ukojozi kitandani hutokea zaidi kwa watoto wa kiume kuliko wa kike.

Vitu gani husababisha ukojozi kitandani?
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha ukojozi kitandani. Baadhi ya njia hizo ni hizi zifuatazo:

Kurithi (Katika familia)Kushindwa kuamka kutoka usingiziniMsongo wa mawazoUkuaji wa taratibu wa mishipa za fahamu kutofanya kazi inavyotakiwa ( hali ambayo humpunguzia mtoto uwezo wa kuzuia kibofu kutoa mkojo)Matatizo ya homoni (kuzalishwa katika kiwango kidogo kwa homoni zinazopunguza kuzalishwa kwa mkojo wakati wa usiku)Maambukizi katika njia ya mkojoMatatizo katika mrija wa mkojo kwa wavulana au kwenye njia ya mkojo kwa wavulana na wasichana.Matatizo kwenye uti wa mgongoKibofu cha mkojo kuwa kidogo

Ukojozi kitandani sio tatizo la akili au tabia. Tatizo hili halitokei eti kwa sababu mtoto ni mvivu kiasi kwamba hawezi kuamka kitandani na kwenda msalani.

Je, ni kipindi gani watoto wengi huweza kudhibiti hali ya mahitaji ya kukojoa?
Watoto huweza kudhibiti kibofu cha mkojo katika umri tofauti. Wakifikia umri wa miaka 6, watoto wengi huacha kukojoa kitandani. Ukojozi wa kitandani hadi katika umri wa miaka 6 siyo kitendo cha ajabu, ingawa inaweza kuwanyima amani wazazi na walezi wengi.Kama mtoto yuko chini ya umri wa miaka 6, tiba kwa tatizo la ukojozi kitandani kwa kawaida siyo mara nyingi watoto wengi huacha kukojoa bila aina yoyote ya matibabu.

Daktari anaweza kusaidia lolote?
Ingawa watoto wengi wanaokojoa kitandani hawana tatizo lolote la kiafya, daktari anaweza kusaidia kugundua kama tatizo la mtoto wako kukojoa kitandani linasababishwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Kwanza daktari atakuuliza iwapo mwanao hukojoa mchana na usiku. Halafu daktari atampima na anaweza kuchukua vipimo vya mkojo kuangalia kama kuna maambukizi au kisukari au matatizo mengine.

Daktari anaweza kutaka kujua mwenendo wa kimaisha wa mwanao anapokuwa nyumbani na hata shuleni.Ingawa unaweza kuogopa mtoto wako anapokojoa kitandani, tafiti zimeonyesha kuwa sio rahisi kwa watoto wanaokojoa kitandani kuwa na matatizo ya hisia tofauti na watoto wengine wasio kojoa kitandani.Daktari pia atakuuliza jinsi mnavyoishi katika familia kwa sababu m matibabu yanaweza kuhusisha mabadiliko kadhaa ya kimaisha hapo nyumbani.

Je, kuna matibabu yoyote kwa tatizo la ukojozi kitandani?
Watoto wengi huacha kukojoa kitandani bila kupata matibabu yoyote.Ingawa wakati mwingine wewe na daktari wako anayemuona mtoto wako mnaweza kuamua kwamba mtoto anahitaji tiba fulani.Kuna aina 2 za tiba: kumbadili mtoto kitabia, na kumpatia dawa. Kumbadili mwanao kitabia husaidia kumfanya mwanao aache tabia ya kukojoa kitandani.Baadhi ya njia za kumbadili mwanao kitabia ni hizi zifuatazo:

Mzuie mwanao asinywe vinywaji/maji kwa wingi kabla ya kulalaHakikisha mwanao anenda msalani kila mara kabla ya muda wa kulala na pia mara tu anapo anza kusinzia.Tumia kengele itakayolia pindi kitanda kinapolowa ,hii humfundisha mtoto kufahamu pindi kibofu kinapojaa wakati wa usikuMpe zawadi mtoto anapoamka bila kukojoa kitandaniMwambie mtoto wako kubadili matandiko mwenyewe kila anapokojoa kitandaniMpe mwanao mazoezi ya kibofu: muelekeze mwanao akae muda mrefu bila kukojoa kipidi cha mchana, ili kibofu kiwe na uwezo wa kutunza mkojo mwingi zaidi .

Ni dawa gani zinazotumika kutibu ukojozi kitandani?
Daktari wako anaweza kumpa mwanao dawa kama ana umri wa miaka zaidi ya saba(7) iwapo njia za kumbadilisha kitabia zilizotajwa hapo hazijasaidia. Hata hivyo dawa hazitibu ukojozi kitandani, Aina mojawapo ya dawa husaidia kibofu kutunza mkojo zaidi, na dawa nyingine husaidia figo kutengeneza kiwango kidogo cha mkojo. Dawa hizi zinaweza kuwa na madhara kiafya kwa mfano, mdomo kukauka na mashavu kuwa na rangi nyekundu.

Mafuta ya mzaituni
Kama mwanao ana tatizo hilo, chukua mafuta haya yapashe kidogo kisha mlaze mwanao, umpake yakiwa na vuguvugu chini ya kitovu kisha umfanyie masaji.

Mdalasini
Hakikisha mwanao anatafuna mdalasini kwa siku hata mara moja, kama hawezi kuutafuna chukua unga wake, changanya na sukari kisha weka kwenye mkate wenye mafuta mpe mwanao.

Ni tiba nzuri ambayo inasaidia haraka tatizo hilo.

Matunda damu
Mpe mwanao glasi ya juisi ya matunda damu saa moja kabla ya kulala, tumia tiba hii kila siku angalau kwa wiki kadhaa.

Kama ataendelea, mpe nusu kikombe kwa siku mara tatu, iwe kama dozi ya vidonge.

Asali
Matumizi ya asali mbichi husaidia sana kuondokana na tatizo hili

MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
MAMBO HAYA YAWEZA KUSAIDIA
1. Kabla ya kulala aende kukojoa

2. Ikifika jioni na kuendelea asinywe maji mengi au vitu vya maji maji mengi.

3. Usiku muamshe akakojoe.

4. Nenda hospital ukapewe dawa au kama unaweza kupata dawa inaitwa IMIPRAMINE kanunue atumie 25mg kila cku ucku kwa muda wa mwezi 1 kwanza
MAANDALIZI YA KABLA YA KULALA YANAWEZA KUWA MSAADA
Nadhani hii inaweza saidia. Hakikisha hanywi maji kuanzia mida ya saa 11 jioni. kisha wakati anaenda kulala hakikisha anakojoa kabisa. pia jaribu kumjenga kisaikolojia kuhusu kutokukojoa kitandani. Siamini katika kumletea marafiki zake manake inamdhalilisha na hiuenda ikam-haunt maishani mwake. Dhana hii inasumbua saikolojia yake na kumfanya usiku ashikwapo na mkojo aamke lakini ni sawa pia na wewe kumjenga kisaikolojia ili bado aweze kuamka na kwenda kujisaidia. Kwa kuanzia unaweza kuwa unamwamsha mida ya saa 9 huko. mara nyingi kukojoa kitandani huja mida hiyo kuelekea asubuhi.
UZOEFU WANGU
Mmmh sidhani kama kuna dawa ya kusaidia hili.

- Kamcheki Hsp kama hana tatizo la kibofu,inawezekana wakati wa baridi anaumia,hawezi kukontrol mkojo etc
Mimi nilikuwa na tatizo hilo,nilikojoa mpaka darasa la 8, yani nilikunywa maji ya mchele wapi, nashkuru wazazi wangu hawakuwa na imani za ajabu ajabu, nilivyoanza darasa la kwanza boarding haikuwa shida coz wengi walikuwa wanakojoa but nilivyofika darasa la 5 nikaanza kuona aibu, nilikuwa na rafiki yangu huyu dada alinisaidia sana nilitengeneza sala nikaweka kwenye kitanda ukuta pale kitandani kila siku naosoma kabla sijalala(with that faith + aibu) Mungu aliskia sala zangu ghafla tu niliacha,yani naanza form 1 sikukujoa tena.

Sala yangu ilikuwa hii:

"Eeeeh Mwenyezi Mungu, nashkuru kwa kunilinda mchana kutwa,naomba unilinde usiku huu mimi na rafiki zangu pamoja na familia yangu huko nyumbani, naomba tuepushe na njaa, magonjwa na vita,walinde na kuwapigania wooote walio ktk hali ngum ya maisha,Mungu nakuomba sana unisaidie nisikojoe kitandani maana naona aibu sana, rafiki yangu Eunice, Grace, Irene wooote hawakojoi basi na mimi naomba niwe kama wao, naona ibu asb kutoa godoro langu nje, najiskia vibaya matroni anavyonisema, namuonea huruma mama kila term ananinunulia godoro jipya Mungu naomba niepushe na aibu hii,na amini utatenda sawasawa na mapenzi yako. Amina

Very serious, hii ilikuwa sala yangu mpaka niliikariri, kwa imani kila kitu kinawezekana.

Kumzuia kunywa maji kuanzia jioni si mbaya inasaidia kwa kiasi kikubwa sana. Kumwitia watoto wamcheke huo ni ulimbukeni matatizo yako unaanzaje kutangaza nje mapungufu ya mtoto wako?

 
Psychiatrists sio kwa wagonjwa wa akili tu lakini hata kama matatizo kama hayo yanayohusu brain vile vile wanaweza kutibu.

Mtoto wa dada yangu (wa kiume) alikuwa na matatizo kama hayo tulishauriwa kumpeleka huko na alipata dawa akapona kabisa. Wakati huo alikuwa ameshapita 16.
 
Mimi nilikuwa na shemeji yangu ameacha akiwa na miaka 18 na hakutumia dawa ila ni kumweka sawa kiali na kutotumia kimywaji chochote kuanzia saa kumi, na mtu anae lala nae awe anamwamsha mara kwa mara baada ya muda utaona amepunguza na baadae ataacha kabisa.
 
Nimeona kesi nyingi za namna hiyo kupitia Emmanuel tv. unaweza pitia huko na ukapata jawabu la hilo tatizo.
 
Mimi nilikuwa na shemeji yangu ameacha akiwa na miaka 18 na hakutumia dawa ila ni kumweka sawa kiali na kutotumia kimywaji chochote kuanzia saa kumi, na mtu anae lala nae awe anamwamsha mara kwa mara baada ya muda utaona amepunguza na baadae ataacha kabisa.

Kuacha kunywa maji kuanzia saa 10 ni hatari kwa afya yake. Kama chakula cha jioni ni saa 1 usiku na kulala ni kuanzia saa 3 usiku basi around dinner time ndio muda muafaka kupunguza vinywaji.

Kwa kawaida ukishakunywa maji/chai etc within half an hour to one hour utayapoteza. Tumia alarm imuamshe at least mara mbili usiku.
 
Nimechukua mawazo yenu. Kwanza ni kumwona daktari. Pili asinywe vinywa, nitaanza na muda wa saa 1 jioni. I will let you know of the progress.
 
Muhimbili kitengo kinaitwa psy unit nenda watakushughulikia.kule kuna vichaa lakini usiogope na haina maana kwamba na huyo mtoto ni kichaa ila ndipo tiba yake ilipo.
 
Mhimbili kitengo kinaitwa psy unit nenda watakushughulikia.kule kuna vichaa lakini usiogope na haina maana kwamba na huyo mtoto ni kichaa ila ndipo tiba yake ilipo.

Ok giraffe, nimechukua mawazo yako.
 
Kuna dawa za kienyeji zinazonywewa - za kihaya to be specific - zilimtibu ndugu yangu alikuwa na tatizo hilo akiwa sekondari. Alipona kabisa.
 
(Dawa ya Mtoto wako anakojowa kitandani si umkamate umpeleke Polisi tu nakutania ) Dawa ya Mtoto kukojowa Kitandani Fanya hivi Mkuu Polisi

Pata Kwato la N'gombe tiya ndani yake kaa la Moto kisha huyo Mtoto wako alinuse hilo kwato lililo na Moto kisha Avue nguo awe uchi apande juu ya Mti kisha huko juu ya Mti akojee Mkojo na akisha maliza kukojowa ashuke avae nguo zake Afanye hiyo Dawa kwa muda wa siku 7 atapona inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu . Fanya hivyo Mkuu Polisi kisha utanijibu baada ya Siku 7 Hakuna Dawa ya Kutibu mtoto anaye kojowa Kitandani Mahospitalini.

Usikose kunipa (Thanks)

Bonyeza pembeni hapo.

Asante Phd. MziziMkavu.
 
Mchukue mdogo wako au kama ni mwenyewe nenda porini tafuta mti mrefu na mkubwa ukwee hadi juu then kojoa ukiwa hukohuko juu huku ukiwa umeshikilia uume au uke wako na ukitazama jinsi mkojo unavyoruka hadi chini.

Fanya hivyo mpaka mkojo uishe. Baada ya hapo teremka endelea na shughuli zako, utakuwa umepona. Hutakojoa tena ukiwa usingizini.
 
Mimi nilitaka kuliandika hili la kutegesha alarm ili imuamshe labda kati ya saa sita za usiku hadi saa 7 ili aende chooni na kingine ni kupunguza sana kunywa chochote baada ya saa moja usiku.
 
Mchemshie ndizi mbichi (ndizi bukoba) pamoja na ndevu za mahindi. Hii ni dawa sahihi kabisa kwa tatizo hilo. Aidha waweza kumzoesha kuamka na kujisaidia haja ndogo au kubwa usiku akishazoea tatizo hilo litaisha kinamna!

Pia mara nyingi hali ile husababishwa na baadhi ya maradhi hususan lile lisilokubalika (Malaria) je anapokuwa na malaria hali yake huwaje?

Maneno mengine ni magumu sana kuandka hapa lakini ikibidi twaweza kuyaandika (uwezekano mkubwa wa kuacha kukojoa kitandani ni mkubwa pia pindi akianza kujua kukojolewa!) tatizo hilo litakoma. kwani hawezi kukubali kuwa kinuka mkojo.
 
Anywe maji yalioosha mchele, achemshe nywele za mahindi anywe maji yake, atapona ataacha mara moja.
 
Wewe mwenyew husika kwa kumuamsha kila baada ya ya masaa 2 aende kukojoa. Fanya ivo kwa wki tatu atazoea na atakua anaamka mwenyewe.
 
Wadau naomba ushauri na tiba kama ipo kwa binti yangu mwenye umri wa miaka 10 sasa.

Amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kukojoa kitandni tangu alipokuwa mdogo, mbaya zaidi ni kwamba sasa hivi tumempeleka Boarding school-shule ya msingi.

Tatizo hili linaonekana kumuathiri kiakili na nina waswasi na maendeleo yake kwa sababu nilipomtembelea kwa mara ya mwisho anaona aibu kutoa godoro kulianika.

Nimeongea na Matron wake anasema hilo tatizo wanalo wengi ila yeye 'frequence' yake ni kubwa kulinganisha na wengine.

Je, tatizo hililinatibika wadau?
 
Back
Top Bottom