Tatizo la mtu mzima kukojoa kitandani - Ushauri, Tiba na dawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la mtu mzima kukojoa kitandani - Ushauri, Tiba na dawa

Discussion in 'JF Doctor' started by Polisi, Dec 10, 2010.

 1. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mdogo wangu bado anakojoa kitandani. Ana miaka 15

  Nisaidieni watalaam.

  ==== Majibu kutoka kwa wanaJF====

   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, ukimuuliza huwa anasema kwanini anakojoa kitandani au nini huwa kinamtokea kabla ya kukojoa....
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Ni mwanamke au mwanamme?

  Ikiwa ni wa kiume basi huchelewa sana kuacha. Jaribu kumpeleka kwa psychiatrist (ndiyo!) kuna dawa kule atapewa na kwa asilimia kubwa zinaweza kumtibu.
   
 4. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ni wa kike. Wife alijaribu kumdodosa, huwa hajijui nashtukia tu na anagundua akiamka. Kuna wakati alikuwa analala na wife ikawa kila ikifika saa 7 au 8 usiku anamwamsha anakwenda kukojoa. Akawa hakojoi kabisa kitandani
   
 5. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Psychiatrists sio kwa wagonjwa wa akili tu lakini hata kama matatizo kama hayo yanayohusu brain vile vile wanaweza kutibu.

  Mtoto wa dada yangu (wa kiume) alikuwa na matatizo kama hayo tulishauriwa kumpeleka huko na alipata dawa akapona kabisa. Wakati huo alikuwa ameshapita 16.
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Fata ushauri wa binti mkongwe, mimi nilikuwa na shemeji yangu ameacha akiwa na miaka 18 na hakutumia dawa ila ni kumweka sawa kiali na kutotumia kimywaji chochote kuanzia saa kumi, na mtu anae lala nae awe anamwamsha mara kwa mara baada ya muda utaona amepunguza na baadae ataacha kabisa....
   
 7. J

  Jikombe Senior Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Pole sana mkuu. Nimeona kesi nyingi za namna hiyo kupitia emmanuel tv. unaweza pitia huko na ukapata jawabu la hilo tatizo.
   
 8. Mdau Mkuu

  Mdau Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nasikia ndevu za mahindi ni dawa bt cjui unafanyaje!Pole na huyo mtoto
   
 9. Simonsica

  Simonsica Member

  #9
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaweza kuwa anakibofu kidogo, ila kwa uhakika zaidi ni vizuri umwone daktari.
   
 10. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kuacha kunywa maji kuanzia saa 10 ni hatari kwa afya yake. Kama chakula cha jioni ni saa 1 usiku na kulala ni kuanzia saa 3 usiku basi around dinner time ndio muda muafaka kupunguza vinywaji. Kwa kawaida ukishakunywa maji/chai etc within half an hour to one hour utayapoteza. Tumia alarm imuamshe at least mara mbili usiku.
   
 11. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nimechukua mawazo yenu. Kwanza ni kumwona daktari. Pili asinywe vinywa, nitaanza na muda wa saa 1 jioni. I will let you know of the progress
   
 12. giraffe

  giraffe JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 504
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Hanza kwa dactari kwanza kabla ujamkataza kunywa maji.
   
 13. giraffe

  giraffe JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 504
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Mhimbili kitengo kinaitwa psy unit nenda watakushughulikia.kule kuna vichaa lakini usiogope na haina maana kwamba na huyo mtoto ni kichaa ila ndipo tiba yake ilipo.
   
 14. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  ok giraffe, nimechukua mawaqzo yako.
   
 15. P

  Puza Senior Member

  #15
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu tuwe serious ktk mambo ya msing ili tujenge kizazi bora
   
 16. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna dawa za kienyeji zinazonywewa - za kihaya to be specific - zilimtibu ndugu yangu alikuwa na tatizo hilo akiwa sekondari. Alipona kabisa.
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  (Dawa ya Mtoto wako anakojowa kitandani si umkamate umpeleke Polisi tu nakutania ) Dawa ya Mtoto kukojowa Kitandani Fanya hivi Mkuu Polisi

  Pata Kwato la N'gombe tiya ndani yake kaa la Moto kisha huyo Mtoto wako alinuse hilo kwato lililo na Moto kisha Avue nguo awe uchi apande juu ya Mti kisha huko juu ya Mti akojee Mkojo na akisha maliza kukojowa ashuke avae nguo zake Afanye hiyo Dawa kwa muda wa siku 7 atapona inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu . Fanya hivyo Mkuu Polisi kisha utanijibu baada ya Siku 7 Hakuna Dawa ya Kutibu mtoto anaye kojowa Kitandani Mahospitalini. Usikose kunipa (Thanks) Bonyeza pembeni hapo asante Phd. MziziMkavu.
   
 18. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Inawezekana umemtumia mdogo wako kwa niaba yako. Anyway, ngoja nikupatie dawa itakayoondoa tatizo hilo milele. Mchukue mdogo wako au kama ni mwenyewe nenda porini tafuta mti mrefu na mkubwa ukwee hadi juu then kojoa ukiwa hukohuko juu huku ukiwa umeshikilia uume au uke wako na ukitazama jinsi mkojo unavyoruka hadi chini. Fanya hivyo mpaka mkojo uishe. Baada ya hapo teremka endelea na shughuli zako, utakuwa umepona. Hutakojoa tena ukiwa usingizini.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Umeniwahi ndugu yangu na mimi nilitaka kuliandika hili la kutegesha alarm ili imuamshe labda kati ya saa sita za usiku hadi saa 7 ili aende chooni na kingine ni kupunguza sana kunywa chochote baada ya saa moja usiku.

   
 20. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mchemshie ndizi mbichi (ndizi bukoba) pamoja na ndevu za mahindi. Hii ni dawa sahihi kabisa kwa tatizo hilo.
  aidha waweza kumzoesha kuamka na kujisaidia haja ndogo au kubwa usiku akishazoea tatizo hilo litaisha kinamna!

  Pia mara nyingi hali ile husababishwa na baadhi ya maradhi hususan lile lisilokubalika (Malaria) je anapokuwa na malaria hali yake huwaje?

  maneno mengine ni magumu sana kuandka hapa lakini ikibidi twaweza kuyaandika (uwezekano mkubwa wa kuacha kukojoa kitandani ni mkubwa pia pindi akianza kujua kukojolewa!) tatizo hilo litakoma. kwani hawezi kukubali kuwa kinuka mkojo.
   
Loading...