kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,871
Habari za asubuhi wadau!
Leo nilikuwa nasikiliza radio nikiwa kwenye daladala kwa kweli takwimu za wanafunzi wanaopata mimba ni kubwa sana. Huko mkoani Mwanza hali inaonekana ni mbaya zaidi. Kwa kweli takwimu inawezekana ni kubwa zaidi kwa sababu maeneo mengine ya nchi haya mambo hayaripotiwi hata polisi maana mambo humalizwa nyumbani. Lakini pia huenda kuna mimba zinanyofolewa zikiwa hazijaonekana kwa wengine. Lakini hata kwa takwimu hizi ambazo serikali inazo bado hali si nzuri.
Sababu ziko nyingi sana za hawa wanafunzi kupata mimba na tukisema tuzitaje tunaweza kutaja sababu lukuki , kwa hiyo hapa natamani tungejadili namna gani tunaweza kumaliza tatizo hili. Wadau karibu sana tutoe mchango wetu ni kivipi tunaweza kuondokana na hii tabia ya dada zetu , wadogo zetu na shangazi zetu na mama zetu wadogo kupewa ujauzito wangali wadogo na kukatishwa haki yao ya kupata elimu.