Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Naomba kupewa elimu juu ya kupata ganzi kunakoenda sambamba na kuwaka moto miguuni kuanzia kwenye vidole vya miguu ( Kanyagio la mguu) ambapo Nusu ya kanyagio kuishia vidoleni napata ganzi sana kiasi kwamba hata nikichomwa au kukatwa na kitu sihisi maumivu zaidi ya kuona damu tu ndio naweza kutambua kwamba nimeumia. Sambamba na hilo sehemu hiyo inayopata gazi inakuwa kama naungua moto kabisa. Naomba ushauri juu ya hili tafadhalini
Mdogo wangu na dada yangu walipata hli tatizo, yani mdogo wangu ilikuwa analia usiku kucha, ila walikuja kutumia neurobics zikawasaidia na leo wako sawa ila kipindi cha baridi ni mwendo wa kuvaa soksi
 
Huu ushauri umeshiba ndio maana naipenda jf.pengine ushauri kama huu ili uupate pesa lazima ikutoke

unapendekeza hospitali gani na gani ambapo wataalamu wa hivyo vipimo wanapatikana
Kwa hospital kubwa mikoa yote Tanzania vipi. Hofu ni kuwa mikoa yote haina hospital za maana. Kwa walio DSM ni Muhimbili, Regency, Hindumandal, TMJ ndiyo angalao. Ukiwa na Bima ya Afya ya kulipiwa na mwajiri utapata vipimo vingi hapo ila cha nerves kuna kimoja atalipia.

KAMA una bima ya kifurushi ni majanga maana vipimo vya maana wamevitoa ila sijui kwa nilivyojitaja ni vipi vipo kwa vyote ila Thyroid Function (T.S.H) na Cortisol AM na PM atalipia 115,000 -120,000. Ni gharama lakini kama uwezo upo ni bora afanye hivyo vipimo agundue tatizo apambane nalo mapema.

Ndiyo maana tunahitaji Rais ambaye anajua jinsi watanzania wanadhalilika na Bima ya NIHF. Utalipia kifurushi cha Timiza ambacho ni kikubwa mfano mtu mmoja na mtoto ni 888,000 kwa mwaka ila ukienda hospital huduma ni duni mno. Vipimo vya bei wameondoa na quality medicine wameondoa. Ni mateso makubwa.
 
Chemsha maji changanya na kitunguu saumu na chumvi loweka miguu kwa nususaa kila siku kwa siku saba
Dr M shana katika ubora wake. Tupe kipimo kitunguu saumu punje ngapi? Unavisaga au vizima? Chumvi na maji kiasi gani?
 
Ahsante mkuu,gharama za vipimo kwa ufupi zipoje?
Bahati mbaya sana hata Neurologists nchi hii ni wachache tena unakuta hospital kubwa aliyepo ana Bsc.Neurology pekee hata vifaa vya kupimia tu hakuna zaidi ya yeye kukuchomachoma visindano huko unyayoni...
 
za mihangaiko mabibi Na mabwana,Mimi ni kijana mwenye miaka 31 ni me nimekubwa na tatizo la miguu kuwaka moto hata kwenye vidole vya mguuni

Baada ya tatizo nilikwenda hospital Na kupima pressure Na Sukari lakini majibu ya vipimo yalionesha kwamba sikuwa na tatizo kwa iyo nikapewa kutumia dawa za neurobin forte zenye mkusanyiko wa vitamin b12.

dawa zilinisaidia kutuliza maumivu lakini bado hali inatokea mara moja moja .naomba msaada wa taarifa kwa mdau yeyote anayeweza nisaidia nini nifanye.

Napatikana ilala nitashukuru kwa michango yenu
 
Nasubiri majibu mie nikiwa misele sisikii dalili hizo ila nikiwa nimelala ndo nasikia japo kwa mbaaaaali
 
Mdogo wangu aliwah kupatwa na hilo tatizo, miguu ilikua inawaka moto + homa usiku halali hadi ikafikia kipind viatu vya kufunika hawezi kuvaa.

Tulihangaika hospital akipimwa tatizo halionekani, kuna mtu akatushauri tujaribu tiba ya natural herbs akatuelekeza kinondoni kulikua na kituo cha afya cha wasabato tukampeleka akapatiwa dozi na tatizo likapona halijawahi kurudi.

Sina uhakika kama bado wapo hadi leo maana ilikua 2011/12
 
za mihangaiko mabibi Na mabwana,Mimi ni kijana mwenye miaka 31 ni me nimekubwa na tatizo la miguu kuwaka moto hata kwenye vidole vya mguuni,baada ya tatizo nilikwenda hospital Na kupima pressure Na Sukari lakini majibu ya vipimo yalionesha kwamba sikuwa na tatizo kwa iyo nikapewa kutumia dawa za neurobin forte zenye mkusanyiko wa vitamin b12.dawa zilinisaidia kutuliza maumivu lakini bado hali inatokea mara moja moja .naomba msaada wa taarifa kwa mdau yeyote anayeweza nisaidia nini nifanye.Napatikana ilala nitashukuru kwa michango yenu
Nenda Hospitali kapime Damu yako itaonyesha huenda una upungufu waVitamin na Madini mwilini huenda una upungufu wa Madini ya chuma Au upungufu wa Vitamin B12 au Vitamin C utakapo pima ndipo itakapo onyesha Sababu ya maradhi yako unayo umwa.

Dawa zipo za asili lakini huwezi kwanza kupewa dawa za asili pasipo kujulikana chanzo cha maradhi yako uguwa pole Mkuu.
 
Back
Top Bottom