Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

Body mass index yangu ni 36,Nahitaji kujua pia ni aina gani ya mazoezi nahitaji kufanya,Kwani physician wamenishauri nisianze mazoezi makali kwanza.Nimewaona wataalam mbali mbali na dawa nimetumia lakini nafuu haipo kabisa.
TEMBEA HARAKA HARAKA KWA MUDA WA DK 30 KILA SIKU KWA SIKU TANO ZA WIKI.HIVYO UTAKUWA UMETUMIA DK 150 NDANI YA WIKI 1,
JINSI YA KUFANYA MAZOEZI HAYO:
AMKA MAPEMA KABLA JUA HALIJA TOKA, SWAKI KINYWA,KULA CHOCHOTE KIDOGO KISHA NENDA ZOEZINI.FANYA HIVYO KWA WIKI 4 MFULULIZO HALAFU LETA MREJESHO MKUU
 
wapendwa
Baba yangu anasumbuliwa na ganzi mguuni, kila anaposimama mguu unashikwa ganzi wote, mguu mmoja. ametumia dawa kadhaa lakini hatuoni mabadiliko yo yote. any idea of medicine/tiba will be helpful.

Thanks
DAWA YA KWANZA MCHUE SEHEMU ZINAZO PATA GANZI KWA MAFUTA YA MKARATUSI NA HABAT SODA AU MZAITUNI. AU TAFUTA MAGOME YA MTI WA MLONGE YAPONDE YALAINIKE KISHA MFUNGE ENEO LENYE GANZI KWA DAKIKA 5-10 KISHA ONDOA.BAADA YA HAPO AANZE MAZOEZI TATIZO LISIJIRUDIE TENA
 
Mazoezi yanasaidia kupunguza maradhi nyemelezi yanayoambatana na tatizo la kisukari kama vile mgonjwa ya moyo, mishipa ya damu nk, uchunguzi wa afya kila mara hususani ukiona tatizo bado lipo ni muhimu Sana
 
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.

Pole sana ndugu... binafsi nilishawahi kupatwa na hili tatizo, nilikuwa na umri wa miaka 21, na nilikuwa bording school advance, ilinipa shida sana maana nilikuwa siwezi kuvaa viatu wala soksi.

Na nikikanyaga chini kwa mda bado nahisi moto. Nilipata shida kwa mda ila nakumbuka nilirudi nyumbani nikapelekwa kwa dactari, sikumbuki nilitumia dawa gani lakini ilikuwa ni sindano tano, moja kila baada ya siku 7. Hiyo sindano maumivu yake siwezi yasimulia maana ni hatari.

Ukichomwa lazima ulale kitandani kama nususaa kwa maumuvu. Ila namshukuru mungu baada ya hapo nilipona. LAKINI KAMA UNATUMIA PILIPILI ACHA, MAANA NAYO HUWA INAONGEZA TATIZO. Nasema hivyo maana nilipokuwa ninatumia pilipili baada ya mda nahis moto.

So nakushauri umwone doctor, pili acha kutumia pilipili nanpia jaribu kupunguza uzito ingawa sijui kama kuna connection
 


Habarini wadau wa JF doctors Leo nimewa letea somo fupi linalo eleza kuhusu miguu kuwaka moto ( burning foot)!!

Lengo la somo ni kuwapa uelewa wa nini hasa maana ya ugojwa, visababishi na Tiba kwa ufupi ambayo hasa inategemea kisababishi cha tatizo. Hilo la moguu kuwaka moto!!

Na wale ambao wanatatizo hili pia itawasaidia kujua nini cha kufanya!!!
Somo lipo kwa namna ya video click link hapo juu na utazame!!!

[HASHTAG]#subscribe[/HASHTAG] to get more videos !!!!
 


Habarini wadau wa JF doctors Leo nimewa letea somo fupi linalo eleza kuhusu miguu kuwaka moto ( burning foot)!!

Lengo la somo ni kuwapa uelewa wa nini hasa maana ya ugojwa, visababishi na Tiba kwa ufupi ambayo hasa inategemea kisababishi cha tatizo. Hilo la moguu kuwaka moto!!

Na wale ambao wanatatizo hili pia itawasaidia kujua nini cha kufanya!!!
Somo lipo kwa namna ya video click link hapo juu na utazame!!!

[HASHTAG]#subscribe[/HASHTAG] to get more videos !!!!


Dr hii Channel yako inapatikana youtube?? Je ni kwa jina gani??
 
pole sana mi mwaka jana niliumwa huo ugonjwa mpaka nikawa siwezi kukanyaga nilizunguka hospitali kubwa zote unazozijua hapa mjini nikatumia kama milioni mbili sijapona uzuri nilikuwa na bima so sikutoa hela mfukoni,nilienda Aga Khan kuna dk mmoja mwanamke wa kihindi nimesahau jina lake nikummushe kesho nicheki vyeti vyangu,alinichoma sindano inaitwa neorobin injectiobn na nyingine siikumbuki na nikapewa food supliment ginsomin sasa nikikwambia nina uwezo wa kucheza mpira na kuruka kama ndama huwezi amini wakati nilikuwa nadhani naelekea kuwa mlemavuunaitwa peripheral neuropath

Vipi Mkuu hiyo nyingine umeshaikumbuka nina mtu ana tatizo hilo hilo ILA dawa anazotumia hazimsaidii.
 
Ndugu zangu ninaomba ushauri wenu nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la miguu kufa ganzi na kuwaka moto kwa muda mrefu pia wakati mwingine huwa napatwa na maumivu makali sehemu ya kifuani nawakati mwingine mate yangu huwa mazito mithili ya makohozi mf wa ute mweupe.

Nimepima labda nikajua nina Tb lakini vipimo vikaonesha negative maana yake sina
 
Una umri wa miaka mingapi?? Tatizo lina muda gani?? Maumivu yanakua ya aina gani??
Miaka 33 tatizo ni la miaka 2 maumivu makali kifuani mfano wa MTU aliyekaa karibu na moto. Lakini hayo maumivu huwa yanadumu kwa kipindi tu si wakat wote
 
Hapo tiba ni chakula bora,matunda,maji mengi ya kunywa na mazoezi hasa ya kutembea kwa miguu sio kaumbali kadogo unataka kupanda gari tembea tembea kwa miguu damu ijisukume vizuri sehemu zote za mwili.
 
Ndugu zangu ninaomba ushauri wenu nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la miguu kufa ganzi na kuwaka moto kwa muda mrefu pia wakati mwingine huwa napatwa na maumivu makali sehemu ya kifuani nawakati mwingine mate yangu huwa mazito mithili ya makohozi mf wa ute mweupe. Nimepima labda nikajua nina Tb lakini vipimo vikaonesha negative maana yake sina
Ongeza maelezo kidogo kwny hayo maumivu ya kifua...
...yanaanzia upande gan wa kifua!!?? Kama yanazungukia upande wa kulia ama kushoto na kuelekea mgongon au yanaishia hapohapo kifuan...
...ukifanya nn maumiv yanaongezeka/yanapungua eg ukilala chali/ukisimama unapata nafuu
...Mara nyng yanakutokea ukiwa umekaa, unatembea, umelala au unafanya mazoez!!??
 
Back
Top Bottom