Tatizo la meno kufa ganzi na chanzo chake

Nina tatizo kama lako na bado sijapona. Epuka kutumia nguvu wakati unapiga mswaki au epuka kupiga mswaki kwa muda mrefu. Wanagoogle wanasema ukiona umeanza kuhisi ganzi ktk meno ujue kuna layer ya juu kwenye meno umeiondoa, layer ya chini inayobaki ni very sensitive-ndo maana unapata ganzi. Hii sio suluhisho la tatizo, lakin itasaidia kuepuka matatizo zaidi.

Ukipata matibabu nifahamishe inbox.
Pole sana miss S bado naendelea kutafuta suluhu pengine ntapata.
 
Kama unatumia whitedent nalo ni tatizo
Mimi nilishindwa kabisa hata kutafuna muwa baada ya kuacha hiyo dawa hivi sasa mambo si mabaya sana
 
Habari zenu wanajamvi,mnamo mwanzoni mwa mwaka jana nilianza kusumbuliwa na meno na hali ya kuwa na ukakasi kama mtu aliyekula ndizi mbichi au limao mdomoni,yaani kuna wakati nakuta kinywa ni kikavu hata nashindwa kuongea vizuri.Tena siwezi kukaa eneo lenye kelele nahisi meno yanakela kama mtu anaposugua kitu chenye kelele mfano wa bati kwenye sakafu.Naomba nisaidiwe ni nini hii jamani?
Mimi nilikuwa na matatizo ya meno Sana nimen'goa meno manne Kuna doctor akanishauri nitumie sensodyne nihakikishe ni original,nimetumia mwaka wa tatu Sasa nimesahau matatizo ya meno kabisa yani ulikuwa ndiyo ugonjwa wangu mkubwa jaribu
 
Nina tatizo kama lako na bado sijapona. Epuka kutumia nguvu wakati unapiga mswaki au epuka kupiga mswaki kwa muda mrefu. Wanagoogle wanasema ukiona umeanza kuhisi ganzi ktk meno ujue kuna layer ya juu kwenye meno umeiondoa, layer ya chini inayobaki ni very sensitive-ndo maana unapata ganzi. Hii sio suluhisho la tatizo, lakin itasaidia kuepuka matatizo zaidi.

Ukipata matibabu nifahamishe inbox.
Nimetoka kwa mganga wa meno wiki iliyopita. Ni kweli, unatakiwa kutumia miswaki soft. Kuna aina tatu hivi za miswaki, soft, medium na hard.
 
Hili tatizo na mie limenianza hivi karibuni aliepata tiba atujuze
 
Habar madakri ...Kuna sehem nilikuwa na nasoma faida mbal mbali za ndimu/ limao ...sasa nina siku kama 5 Hiv nikiwa natumia limua kwa kukamulia kwenye maji kila cku asubuhi lakin cha ajabu naona meno yangu yamwanza kufa ganzi ...sababu ni nini hasa? Naombeni ufafanunuz tafadhal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa na matatizo ya meno Sana nimen'goa meno manne Kuna doctor akanishauri nitumie sensodyne nihakikishe ni original,nimetumia mwaka wa tatu Sasa nimesahau matatizo ya meno kabisa yani ulikuwa ndiyo ugonjwa wangu mkubwa jaribu
Utajuaje ni original!?
Mi huwa natumia med oral tooth paste.
 
Kichwa hapo juu ndicho cha husika.
Naombeni msaada wa namna yoyote.
Yapata wiki tatu sasa meno yangu yanapata ganzi au inakuwa kama nimekula kitu chenye uchachu vile! Tatizo hili ni nini? Au ni dalili za ugonjwa gani? Ila hayaumi kabisa! Tafadharini wadau nifanyeje?
 
Fika clinic yoyote ya meno iliyo karibu na we wewe, ni kama tu unajali Afya yako
 
Kwa kitaalamu hilo tatizo linaitwa hypersensitivity, mara nyingi huwa linatokea hasa pale ambapo ,mmhusika anatumia mswaki ambao kitaalamu hautakiwi kwa matumizi ya meno , yaani mswaki wenye brash ngumu ambao hujilia kuondoa lea ya nje ya jino yaani enameli , na mara nyingi huwa inatokea hasa kwenye shingo ya jino ,pale ambapo ufizi unaanzia , sehemu hii pamoja na lea ya ndani ya jino yaani dentine, inavitundu vidogo dogo sana ( stomata poles) ambavyo huruhusu upenyo wa kitu chochote chenye tindikali ,umaridi ,pamoja na umoto kupenya kiurahisi na kusababisha hali ya ganzi,
Lkn pia hali hii huwatokea watu ambao , wanapolala usiku huwa na tabia ya kutafuna meno na hvy kuondoa ile lea ya juu ya jino (enamel) lakin pamoja na hayo pia huwatokea watu ambao meno yao yanakuwa wiki , hasa kutokana na ukosefu wa madini , calcium, fluoride,
TIBA
Mwone daktari akujuze kama kuna meno yaliyotoboka
Zingatia namna ya upigaji mswaki hasa muda usizidi dakika 15.
Daktari atafanya matibabu yameno yako kulingana na yalivyoathirika.
Mwisho daktari atakuelimisha ni dawa gani inafaa kwa meno yako.
asante mkuu
 
Wakuu meno kupata ganzi wakati hujala wala kunywa kitu kinachopelekea hali hiyo ni nini tatizo?
Je matibabu yapoje katika hili?
 
Habari wakuu. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada

Naomba msaada, Kuna wakati nikiwa napiga mswaki nahisi meno yanakuwa na ukakasi kama ule mtu akiwa amekula matunda kama vile limao au maembe machachu, hasa kwenye magego.

Lakini pia nikitafuna vitu vigumu sana hiyo hali inajitokeza.

Naombeni kujuzwa tatizo ni nini? Na je tiba yake ni nini?

Asanteni
 
Back
Top Bottom