Tatizo la Mawe Kwenye Figo

Aisee hayo mawe maumivu yake si mchezo!

Miaka miwili iliyopita niliyapata.

Nilishika adabu.

Kwa vile yangu hayakuwa makubwa [chini ya MM 3], niliandikiwa dawa mbili: Flomax - ya kuyayeyusha na Percocets - za kupunguza maumivu.

Ila pia, kuna mambo kadhaa waweza kufanya ili kujikinga au kuyazuia yasikutokee.

Wanashauri kunywa maji mengi ya kutosha.

Kunywa juisi ya makomamanga yenyewe tu [yaani 100% pomegranate juice], 100% cranberry juice [sijui Kiswahili chake], na kadhalika.
 
Hospitali ya Mloganzila kuna mashine inatibu hayo mawe bila upasuaji. Uliza kwa dakari wako akupe rufaa utibiwe.
 
Hizo Dawa Kaka Zilikusaidia Kabisa??
Ndiyo!

Maumivu yaliisha kabisa na nikarudia hali yangu ya kawaida.

Ila haina maana siwezi tena kuyapata.

Wataalamu wanasema kwamba ukishayapata mara moja basi uwezekano wa kuyapata tena ni mkubwa.

Ila, unaweza kuupunguza uwezekano huo kwa kunywa maji mengi na kupunguza kula au kunywa baadhi ya vitu na kunywa maji mengi ya kutosha pamoja na juisi ya mkomamanga.
 
Mawe kwenye figo au Calculi inaweza kusababishwa na

1 Unywaji mdogo wa maji
2. Utumiaji wa dawa bila maji ya kutosha
3. Kuzidi kwa kiwango cha chumvichumvi kwenye figo
4. Na mengineyo

Ushauri uliotolewa hapo juu unakutosha kupona na kuendelea kuunga mkono awamu hii kwenye uchumi wa kati
KUMBUKA. Mungu pekee ndiye wa kuaminiwa na kuabudiwa ndio DAWA
 
Yalinipata pia kidogo nitage mayai. Yanauma balaa. Nilipewa dawa yakayeyuka.

Ushauri kunywa maji kama samaki. Punguza nyama hasa nyekundu katika mlo wako ,hospitali wanaweza kuyapasua na mashine ikishindikana wakakata kuyatoa
 
Mwanzisha mada nakuomba ungeweka dalili ulizonazo ili na wengne wapate somo maana wengne wanakuwa na dalili za mawe kwenye figo lakin hawaelew kama ndo IPO ivo pia na nyie mliopona ingekuwa vizuri na nyie muweke dalili zenu ili wengi tujifunze?

Dalili Ni Maumivu Makali Sana Sehemu Ya Tumbo Eneo la figo Husika
 
Kuna jamaa yangu alipona alitumia juis ya tangawi asubuh na jion kwa muda wa mwez tu


Juice ya tangawizi na limao unaweka sukari kidogo ili uweze kuinywa kwa wale wasioweza kuinywa kwani ni kali kiasi fulani kinywani.
 
Back
Top Bottom