Eberi M. Manya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 743
- 280
Wanajamvi, kumekuwa na tatizo kubwa sana sugu ya maji kwa takriban mwaka mmoja sasa katika Manispaa ya Moshi na hasa zaidi katika viunga vya Manispaa hiyo kama vile Kariwa, Rau, Njiapanda, KCMC na maeneo mengi yanayozunguka Manispaa hiyo.
Tarizo hili sasa limekuwa sugu na dondandugu lisiloisha na sasa kwa wiki iliyopita na na wiki hii wananchi wa maeneo tajwa wananunua maji kwa ndoo shilingi 1000, pamoja na bei hiyo ya maji kuwa kubwa sana, bado maji hayo pia hayapatikani tena.
Mamlaka ya maji mjini humo imekuwa haiambiliki, na hata wakipigiwa simu hawapokei na hata wakipokea wamekuwa hawatoi majibu yanayoridhisha.
Moshi ni mji wa Mlima Kilimanjaro yenye vyanzo vingi vya maji, lakini watawala wamekuwa wakitumia vyanzo vile vile vya zamani huku idadi ya watu na matumizi ya maji yakiongezeka kila kukicha. Mamlaka ya maji mjini humo wamekuwa si wabunivu na wamekuwa ni watu wa kukaa maofisini miaka nenda rudi pasipo kutafuta uvumbuzi wa tatizo hilo sugu la maji.
Ni aibu kubwa na fedheha kwa wakazi wa Moshi na hasa moshi mjini na viunga vyake kulilia tatizo la maji miaka nenda rudi huku kukiwa na vyanzo lukuki vya maji ya kutosha.
Narudia tena ni aibu kubwa na fedheha kwa wakazi wa Moshi mjini hasa Maeneo ya Kariwa, Rau, KCMC, Njiapanda na maeneo mengi ya jirani kununua ndoo ya maji kwa shilingi 1000. Hiyo ni fedheha kubwa sana lisiloweza kuvumiliwa.
Hivi sasa katika maeneo hayo tajwa wakazi wa maeneo hayo wanajipanga kuandamana kwenda kudai maji katika ofisi ya mkuu wa mkoa. Wamechoka kulipia bili za maji yasiyoonekana kila mwezi, tena bili hiyo ikiwa linakuja kubwa sana kupita kawaida.
Namwomba mkuu wa mkoa mpya anayekuja sasa Mhe Meck Said Sadick aanze na tatizo hilo kubwa la maji ambayo imekuwa ni kero kubwa kwa Manispaa hiyo na hasa maeneo tajwa hapo juu.
Pili, namwomba Mkuu wa mkoa mpya anapokuja aanze kutumbua majibu yaliyokwishaiva tayari katika mamlaka ya maji ya manispaa hiyo(MUWSA). Huko MUWSA kuna majibu ya kutumbuliwa mengi sana. Naomba yatumbuliwe haraka sana.
Mwisho, namkaribisha Mkuu wa mkoa mpya katika mkoa huu wa Kilimanjaro na hususan Manispaa ya Moshi, amalize kabisa tatizo hili sugu la maji.
KARIBU SANA MKUU WA MKOA Mhe Meck Said Saidick. Anza na tatizo hili sugu la maji na kutumbua majipu haraka sana.
MUNGU IBARIKI MOSHI, na MUNGU ibariki Tanzania.