Tatizo la maji: Kila nchi ina kilio chake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la maji: Kila nchi ina kilio chake

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Oct 18, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mwasu Sware

  UKOSEFU wa maji katika maeneo mbalimbali nchini umekuwa sugu katika maeneo mbalimbali na kwa kiwango kikubwa, waathirika wakubwa wamekuwa ni wanawake.

  Wamekuwa wakipoteza muda wao mwingi wa kufanya kazi za kujiletea maendeleo kwa kuyafuata umbali mrefu hasa kwa wale wanaoishi vijijini na kwa wale wa mijini nao wamekuwa wakipoteza muda wao mwingi kwenye foleni kupata huduma hiyo muhimu.

  Akiwasilisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2009/10, Waziri wa Maji na Umwangiliaji, Profesa Mark Mwandosya alisema serikali inatambua kuwepo kwa tatizo kubwa la maji nchini na kwamba inalitafutia ufumbuzi.

  Alizungumzia ujenzi wa mabwawa na kusema serikali inatambua umuhimu wake na kwamba itayajenga katika mikoa kame ili kuvuna maji na kuongeza uwezekano wa kuendelea na kilimo hata mvua zinapokatika.

  Kwa Tanzania unapouzungumzia shida ya maji, moja kwa moja unalenga sehemu za vijijini na baadhi ya maeneo machache ya mijini. Lakini hali ni tofauti kwa nchi jirani kama Zambia, Kenya, na Uganda ambazo kwao tatizo la maji lipo mijini na siyo vijijini.

  Hivi karibuni, nilizungumza na wawakilishi kutoka nchi hizo waliokuwa wakishiriki Tamasha la Jinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Dar es Salaam.

  Kenya, kwa mfano, Mwanaharakati wa haki za wanawake nchini humo, Slyvia Achieng' anasema maji ni tatizo kubwa katika maeneo ya mijini kwa kuwa asilimia kubwa ya maji yanayotumika yanatoka kwenye misitu.

  "Hali ya maji katika maeneo ya vijijini ni nzuri huwezi kulinganisha na hali ilivyo maeneo ya mijini. Maeneo mengi ya mijini yanategemea maji kutoka kwenye misitu, maji ambayo ni machafu," anasema.

  Anatoa mfano wa eneo la Korogosho nchini humo sehemu ambayo kuna makazi ya watu wengi lakini hayajapimwa. Anasema kuna shida kubwa maji na tegemeo lao kubwa la maji ni kutoka kwenye misitu.

  Anasema maji ni haki ya msingi kwa kila binadamu lakini wanawake ndiyo wamekuwa wakiteseka zaidi kuyatafuta yanapokuwa adimu.

  "Pamoja na kuwa maji ni tatizo, bado mzigo mkubwa anakuwa nao mwanamke kwa kuwa amekuwa akiyafuata katika umbali mrefu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ya kila siku," anasema Achieng".

  Ofisa kutoka Kituo cha Wanawake Kusini mwa Afrika kinachoshughulikia Haki za Ardhi na Maji (WLWRSA) Zambia, Grace Gurira anasema ni jambo la kawaida nchini humo kuona watu pamoja na wanyama wakitumia maji ya aina moja.

  Gurira anatoa mfano wa kisima kikubwa kilichipo Mashariki mwa Lusaka akisema wastani wa watu wapatao 1.2milioni wanaoishi kwenye nyumba 480 hivi, wanakitumia kwa ajili ya huduma ya majisafi. Anasema tatizo linakuwa kubwa zaidi kinapokauka kwani huwalazimu wanawake kuyafuata umbali mrefu aghalabu kilometa 16.

  "Kisima hicho kikubwa kinafahamika kama Katavi Dam, na maana halisi ya katavi ni kitu kichafu, lakini hayo ndiyo maji yanayotumika kwa ajili ya kunywa, kupikia, kufulia, kumwagilia mboga na pia hutumika kwa ajili ya kunyweshea wanyama," anasema Gurira.

  Kutokana na hali hiyo ya ukubwa wa matumizi, upatikanaji wake ni mgumu hivyo kuwafanya wanawake wengi kuacha kufanya kazi nyingine za kiuchumi na badala yake kujishughulisha na utafutaji wa maji umbali mrefu.

  Ili kukabiliana na shinda hizo, anasema kituo chake kimekuwa kikifanya jitihada mbalimbali akitoa mfano wa ununuzi wa matanki tisa kilichofanya ambayo tayari yamewekwa kwenye baadhi ya nyumba ili kuhakikisha upatikanaji wa majisafi.

  “Hali ni mbaya kwa kuwa wakazi walio wengi vyoo vyao ni vya shimo ambavyo ni vifupi na hakuna maji. Ndiyo maana hata milipuko ya magonjwa kama kuharisha, kipindupindu, malaria, ugonjwa wa matumbo unapotokea watu wa maeneo yasiyo na maji wanaathirika kirahisi.”

  "Ndiyo maana hivi sasa tunahangaika kutafuta wafadhili angalau tuweze kuweka tanki moja katika kila nyumba zilizopo Zambia. Huenda tukasaidia kupunguza tatizo hili," anasema Gurira.

  Kwa upande wake Ofisa wa Kikundi cha Maendeleo ya Wanawake cha Katosi (KWDT), kilichopo Uganda, Bavuma Rehema anasema asilimia kubwa ya maji katika eneo wanaloshughulikia yanatoka katika Ziwa Victoria ambayo anasema yanatumika kabla ya kusafishwa hivyo kuwa hatari kwa afya za watu kutokana na mchanganyiko wa takataka zilizopo katika ziwa hilo.

  "Wanawake ndiyo wenye jukumu la kutafuta maji kwa ajili ya matumuzi mbalimbali ya nyumbani. Kwa mfano, wanawake wanaoishi katika Wilaya ya Mkono wamekuwa wakitumia zaidi maji kutoka Ziwa Victoria maji ambayo si mazuri kwa matumizi ya binadamu," anasema Rehema.

  Anasema KWDT imeanzisha utaratibu maalumu wa kuvuna maji ya mvua na kuweka matanki 134 katika nyumba za wanawake waliopo katika kikundi hicho.

  "Tunachokifanya ni kuwawekea matanki wanawake waliopo kwenye kikundi chetu halafu wanalipa fedha kidogo ambazo zinatuwezesha kununulia matanki mengine kwa ajili ya kuwawekea wengine," anasema Rehema.

  Akizungumzia hali ilivyo wilayani mwake, Ofisa Afya kutoka Manispaa ya Temeke, Juhudi Nyambuka anasema tatizo la maji ni kubwa licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na asasi zisizokuwa za kiserikali kuhakikisha hali hiyo inatoweka.

  "Ili kukabiliana na tatizo hilo tumeanzisha kikundi kinachojulika kama WAHECO, chenye lengo la kuhamasiha jamii kutambua tatizo na kisha kulipatia ufumbuzi," anasema Nyambuka.

  Anasema katika kukabiliana na hilo tayari visima zaidi ya 20 vimeshachimbwa na hivyo kurahisisha upatikanaji wa maji...

  "Kabla ya visima hivyo kuchimbwa ka kweli hali ilikuwa mbaya maana mwanamke alilazimika kuyafuata umbali mrefu. Kwa mfano, mtu anatoka Kurasini inamlazimu kuyafuata maji Mtoni Darajani na huo ni mwendo wa saa tatu mpaka nne."

  Hata hivyo, anasema hivi sasa hali ni nzuri kwa kuwa tayari kuna visima vingi ambavyo vimechimbwa pamoja na kuwepo kwa huduma ya majisafi ya bomba yanayotolewa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco).

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15361
   
Loading...